Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

1 0 /

K U T A F S I R I B I B L I A

Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa kutumia mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi zako za ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako, hivyo ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika kusoma moduli hii ya Kutafsiri Bibliaya mtaala wa Capstone , utahitajika kufanya kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (kujifunza kutokana na Maandiko yenyewe) kwa kutumia andiko mojawapo kati ya Maandiko yafuatayo ya Neno la Mungu:  Zaburi 19:7-11  2 Timotheo 3:14-17  1 Wakorintho 2:9-16  Zaburi 1:1-3  Mathayo 22:34-40  Yakobo 1:22-25  Isaya 55:8-11  2 Petro 1:19-21  Mithali 2:1-5 Dhumuni la kazi hii ya ufafanuzi ni kukupa fursa ya kujifunza kwa kina andiko mojawapo muhimu linalozungumzia asili na kazi ya Neno la Mungu. Unaposoma mojawapo ya maandiko yaliyopo hapo juu (au andiko ambalo wewe na Mkufunzi wako mtakubaliana ambalo linaweza kuwa halipo kwenye orodha hii), matumaini yetu ni kwamba utaweza kuonyesha jinsi andiko hilo linavyoangazia au kuweka wazi umuhimu wa Neno la Mungu katika kuimarisha maisha yetu ya kiroho na kwa faida ya maisha yetu pamoja katika Kanisa. Pia ni maombi yetu kwamba Roho akupe ufahamu wa jinsi unavyoweza kuhusianisha moja kwa moja maana ya andiko hilo na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, pamoja na jukumu la uongozi ambalo Mungu amekupa kwa sasa katika kanisa na huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya ufafanuzi, ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika ? Kazi za Ufafanuzi wa Maandiko

Dhumuni

Muhtasari na Muundo

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker