Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 1 0 9
K U T A F S I R I B I B L I A
Mungu ametupa ahadi za uhakika na za kweli kuhusu nguvu ya maombi ya kutubadilisha, kututia nguvu, na kutupatia mahitaji yetu na maelekezo kutoka kwa Bwana. Kama tulivyoona katika somo hili, haiwezekani kulielewa na kuliishi Neno laMungu pasipomaisha yenye bidii katikamaombi, tena aina ile yamaombi ambayo kwa bidii kubwa na toba tunamwomba Mungu atupatie hekima inayohitajika ili kulijua na kuliishi Neno lake. Chukua muda na wanafunzi wenzako kuyainua maombi yako mbele za Bwana, bila fadhaa na kwa moyo wa shukrani, ukizifanya haja zako (na sio madai yako!) zijulikane na Mungu. Ameahidi kwamba riziki na amani yake vitahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu (Flp. 4:6-7). Kumbukaneni ninyi kwa nyinyi katika siku za katikati ya wiki, na mchukulie kwa uzito maombi yenu na ya wengine, na mtaona jinsi Mungu anavyojibu maombi yenu kwa habari ya hekima, nguvu, na baraka zake.
KAZI
2
Ezra 7:10; Matendo 17:11; Zaburi 1:1-3.
Kukariri maandiko.
Ili kujiandaa kwa ajili ya kipindi, tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata kazi ya kusoma ya wiki ijayo, au muulize mkufunzi wako.
Kazi ya usomaji.
Kama ilivyokuwa katika kipindi cha lililopita, utakuwa na mtiahani kuhusiana na yote ambayo yamefundishwa katika somo hili, kwa hivyo hakikisha kwamba unapitia kwa umakini dhana mbalimbali zilizojadiliwa hapa. Kumbuka, pia, kwamba unapaswa kukamilisha kazi ya usomaji uliopewa kama inavyoonyeshwa hapo juu, na kama ulivyofanya wiki iliyopita, tafadhali andika muhtasari mfupi kwa kila eneo ulilopewa kusoma. Leta muhtasari huo kwenye kipindi chetu kijacho (tafadhali tazama “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” mwishoni mwa somo hili). Pia, sasa ni wakati muafaka wa kuanza kufikiria kuhusu aina ya kazi ya huduma, na pia kuamua ni kifungu gani cha maandiko utakachochagua kwa ajili ya kazi ya ufafanuzi. Usichelewe kufanya maamuzi kuhusiana na kazi yako ya huduma na ya ufafanuzi. Kadiri utakavyofanya maamuzi hayo mapema ndivyo utajipatia muda wa kutosha wa kujiandaa na kutekeleza kazi zako.
Kazi nyingine.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker