Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
1 2 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
ukweli kwamba Biblia yenyewe ni kitabu cha fasihi, ambacho kimepangiliwa kwa umakini mkubwa na kinapaswa kutafsiriwa kwa kuongozwa na kanuni za fasihi kama vitabu vingine vya fasihi, na kwamba Mungu alitumia aina na mbinu za kifasihi za kibinadamu ili kuwasilisha Neno lake kwetu. • Kuna aina na miundo mingi muhimu ya fasihi katika maandiko. Hizi ni pamoja na matumizi ya masimulizi (ya kihistoria na ya kutunga), Sheria (maandiko ya kisheria), nyaraka (barua), unabii, fasihi ya hekima (methali, monolojia, vitendawili, hekaya, mafumbo, istiari, n.k.), na uwepo wa kazi za kishairi. • Tanzu hutokea kwa sababu ya madhumuni mahususi ya kifasihi ya waandishi ya kushughulikia mahitaji na masuala mahususi kwa hadhira zao husika, na pia kuongeza uelewa wetu wa msingi wa maisha ya mwanadamu. Elimu juu ya tanzu pia huturuhusu kuufahamu ukweli kwa kuuona ukiwasilishwa katika muundo wake halisi, na pia kuonyesha ustadi wa waandishi wa Biblia kama walivyoongozwa na Roho, na kufunua utajiri wa siri ya Mungu na kazi yake katika dunia. • Kuzingatia kwa umakini matumizi ya tanzu na kanuni za kuzitafsiri kunaweza kutupatia manufaa makubwa katika jitihada zetu za kutafsiri Biblia; ufahamu kuhusu tanzu unaweza kutuwezesha kugundua nia ya asili ya mwandishi, kutujenga tunapotambua maana ya maandiko kwa ajili ya maisha yetu, kututajirisha na kutuburudisha katika uzuri wa maandiko yenyewe, na kututia nuru katika ujuzi wa kusudi na mapenzi ya Mungu. Kwa nini ni muhimu kuainisha maandiko ya Biblia kulingana na muundo wake wa kifasihi? Kwanza, muundo wa fasihi ya maandiko mara nyingi ni kidokezo cha maana yake. Kwa mfano, jinsi tunavyotafsiri Mwanzo 1-3 inategemea kama inasomwa kama hadithi ya uumbaji, istiari, au historia ya kisayansi. Maana tunayoona katika kifungu mara nyingi hutokana na mtazamo wetu wa awali kuhusu muundo wake wa kifasihi. Pili, umbo la fasihi mara nyingi ni kidokezo cha muktadha wa maisha katika andiko husika. Tukiweza kugundua kwamba kifungu kiko katika muundo wa wimbo, tunaweza kukihusisha na mpangilio wa kiliturujia ambamo kilitoka. Tatu, kutambua kwa usahihi muundo wa kifasihi hutuwezesha kulinganisha andiko husika na aina zinazofanana za kifasihi katika maandiko mengine ya Biblia na yasiyo ya kibiblia. Ulinganifu huo mara nyingi hutuwezesha kuona mambo mengi katika maandiko ambayo tusingeweza kuyaona. Umuhimu wa tanzu katika kujifunza Biblia.
3
~ Carl R. Holladay. “Biblical Criticism.” Harper’s Bible Dictionary . P. J. Achtemeier, ed. (1st ed.) Harper & Row: San Francisco, 1985. p. 131.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker