Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 1 3 7
K U T A F S I R I B I B L I A
maandiko yenyewe. Jibu maswali yafuatayo kuhusu tanzu na umuhimu wake katika kutafsiri Biblia ukizingatia umuhimu wake katika kutengeneza hemenetiki sahihi ya maandiko. Jitaidi kupangilia mawazo yako vizuri na kwa mtiririko unaoeleweka. 1. Fafanua neno “tanzu” na eleza namna linavyohusiana na uelewa wa fasihi kwa ujumla? Kwa nini ufafanuzi huu unaweza kutusaidia kuelewa jukumu la tanzu katika kujifunza Biblia? 2. Ni zipi baadhi ya dhana kuu ambazo ni msingi wa uelewa sahihi wa matumizi ya tanzu katika ufasiri wa Biblia? Kwa nini ni muhimu sana kuitambua Biblia kama kitabu cha fasihi, na hili linsaidia nini kuhusiana na namna tunavyoshughulika na maandiko kwa kuzingatia aina na miundo yake tofauti? 3. Tunajuaje kwamba Mungu alichagua kutumia aina hizi za mbinu za kifasihi za wanadamu ili kuwasilisha Neno lake kwetu? Kwa nini ukweli huu unapaswa kututia moyo kugundua kanuni na mbinu za tanzu kama zilivyojumuishwa katika Maandiko Matakatifu? 4. Orodhesha baadhi ya aina na miundo muhimu ya fasihi katika maandiko. Tunapata ujumbe gani kuhusiana na Biblia tunapoona aina mbalimbali za fasihi katika Maandiko Matakatifu? 5. Katika tathmini yako ya tanzu mbalimbali za Biblia, unafikiri kuna aina fulani ambazo ni muhimu zaidi kuliko nyingine, na ikiwa ndivyo, ni zipi na kwa nini? 6. Tunawezaje kuelezea uwepo wa aina nyingi tofauti-tofauti za fasihi katika Biblia? Ni kwa njia gani ufahamu juu ya tanzu unatusaidia kuelewa vyema zaidi viwango mbalimbali vya “ufahamu wa msingi wa maisha ya mwanadamu?” 7. Mtu fulani alisema kwamba fasihi husema ukweli kwa kuuonyesha . Elimu ya tanzu inatusaidiaje kuelewa ukweli kwa kuuona katika taswira ya umbo lake halisi? 8. Kwa nini inaweza kuwa muhimu kwa wanafunzi wa Biblia kufahamu ustadi wa waandishi wa Biblia kama waandishi waliovuviwa na kuongozwa na Roho Mtakatifu? Ni kwa jinsi gani, pia, elimu ya tanzu inafunua utajiri wa siri ya Mungu na kazi yake ulimwenguni? 9. Orodhesha faida kuu za elimu ya tanzu katika ufasiri wa Biblia. Kati ya manufaa yote yanayozungumziwa katika sehemu hii, ni manufaa gani unayoamini yatachochea moja kwa moja jitihada zako za kujifunza Biblia? Eleza.
3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker