Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 1 4 5

K U T A F S I R I B I B L I A

A. Thibitisha muktadha wa hadithi.

1. Ni nani anayesimulia hadithi, anayesimuliwa, wapi, na kwa sababu zipi?

2. Mazingira ya kijiografia ya hadithi ni yapi?

3. Kulikuwa na hali gani ya kitamaduni-kidini-kihistoria-kimahusiano baina ya watu mahali ambapo hadithi inasimuliwa?

B. Tambua wahusika wa hadithi.

1. “Shujaa” ni nani? “Mwovu” ni nani? Je, mikutano na maingiliano yao yanaathiriana vipi katika hadithi?

3

2. Wahusika wameonyeshwaje kwetu?

a. Maelezo ya moja kwa moja kuhusu wahusika (maelezo kuhusu mitazamo yao, vitendo na mwonekano wao).

b. Ubainishaji usio wa moja kwa moja (k.m, mwonekano, kwa maneno wanayosema, mawazo na mitazamo wanayochukua, kwa athari waliyo nayo kwa wengine, kwa matendo yao [wema au maovu]).

3. Wahusika wanajaribiwaje, na wanafanya maamuzi gani?

4. Je, wahusika waliendelea na kukua katika maendeleo yao ndani ya hadithi hii?

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker