Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

1 5 2 /

K U T A F S I R I B I B L I A

4. Unaweza kuwasilishwa ili kuficha ukweli na pia kufunua nafsi na nia ya Mungu, Hes. 12:6-8.

5. Nabii hawezi kuwa mwamuzi wa mwisho wa uhalali wa ujumbe wake.

a. Manabii na jumbe zao katika Agano la Kale na Agano Jipya walipingwa na kukataliwa (ona 1 Wafalme 22; Yer. 23; 28; na 2 Kor. 11:4, 13; 1 Yoh. 4:1-3).

b. Maneno ya kinabii yalijaribiwa: (1) Kuhakiki sifa na uhalali wake wa kinabii, 1 Kor. 14:29. (2) Kuhakiki kukubaliana kwake na mafundisho ya Musa, Kumb. 13:1-5. (3) Kuhakiki kutimia kwake katika historia, Yer. 23. (4) Kuhakiki kukubaliana kwake na nafsi na mafundisho ya Yesu, Mt. 7:15; 24:11; 2 Pet. 2:1. (5) Na yalikubaliwa mara yalipothibitishwa kuwa kweli, 1 Thes. 5:19-21.

3

IV. Apokaliptiki kama tanzu ya kibiblia

A. Ufafanuzi wa fasihi ya apokaliptiki

1. Inatokana na neno “ apocalypse ” a·poc·a·lypse (-pk-lps) n. “kufunua”

2. Sehemu za Danieli na kitabu cha Ufunuo.

3. Idadi yoyote ya maandishi ya Kiyahudi au ya Kikristo yasiyojulikana kutoka karibu karne ya pili K.K. hadi karne ya pili B.K yenye maono

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker