Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

1 5 4 /

K U T A F S I R I B I B L I A

(5) Tatizo la mateso ya mwanadamu na uhusiano wake na haki na upendo wa Mungu ( theodicy )

c. Imeandikwa chini ya jina bandia (jina tofauti na jina halisi la mwandishi) kwa kawaida mtu muhimu katika historia ya kale ya Biblia (k.m., Henoko, Ezra).

d. Hutolewa kwa kawaida kupitia ndoto, maono, au ufunuo maalum ambamo uwakilishi tajiri wa taashira hufasiriwa kwa “mwonaji” (yaani, mpokeaji wa maono hayo) na malaika.

4. Aina kuu mbili za apokalipsi za Kiyahudi

a. Apokalipsi za kikosmolojia – hujihusisha zaidi na siri za ulimwengu na mbingu ambazo zinafunuliwa katika safari za ulimwengu mwingine.

3

b. Apokalipsi za kihistoria-eskatolojia – (k.m. Danieli) – hujihusisha zaidi na makusudi ya Mungu katika historia, ikijumuisha muhtasari wa historia ya mwanadamu ambapo Mungu ameweka katika vipindi maalum. (1) Zinajikita zaidi katika kuja kwa mwisho wa historia ya wanadamu. (2) Zinazungumza kuhusu ushindi unaokuja wa Mungu juu ya mamlaka na mataifa maovu yanayoharibu na kuwakandamiza watu. (3) Zinazungumza juu ya uharibifu kamili ambao Mungu atauleta juu ya matokeo yote ya nguvu za kishetani, uovu, na mateso yanayohusiana na anguko. (4) Zinazungumza kuhusu Mungu kusimamisha Ufalme wake wa milele, pamoja na ufufuo wa wafu, hukumu ya waovu na wasiotubu, na baraka inayokuja kwa ulimwengu mzima na waadilifu.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker