Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

1 6 0 /

K U T A F S I R I B I B L I A

³ Wanatheolojia wa hadithi hujikita katika simulizi za hadithi katika maandiko, na kuanza kazi yao ya kufasiri kwa dhana ya jumla ya theolojia ya hadithi, ambayo ni pamoja na wazo kwamba njia ya kuu ambayo Mungu ameitumia kuelezea asili yake na kazi yake ni kupitia simulizi ya hadithi katika maandiko. Dhana nyingine ni pamoja na wazo kwamba theolojia yote ni tafakuri ya hadithi za Biblia, kwamba hadithi za Biblia zinazorejelea simulizi za kihistoria ni za kuaminika na sahihi, kwamba hadithi zimeandikwa kwa ustadi wa kisanii, kwamba tunakutana na Mungu kupitia hadithi za Biblia, na kwamba mara nyingi Mungu hutoa ufafanuzi wake mwenyewe kuhusu maana ya simulizi za hadithi za Biblia. ³ Theolojia ya hadithi imejengwa juu ya msingi wa dhana muhimu kuhusu hadithi, Biblia, na Kanisa. Hizi ni pamoja na dhana kwamba hadithi hutuleta katika uwepo wa kisakramenti, ni muhimu zaidi kuliko maelezo ya kawaida, zinakubalika kama msingi wa maongozi katika jamii ya Wakristo. Tamaduni za Kikristo hukua na kujifafanua zenyewe kwa njia ya hadithi, ambazo hutangulia na kuzaa jumuiya, maonyo na uwajibikaji, na huzalisha theolojia, liturjia na sakramenti. Hadithi ni historia. ³ Kama fasihi nyingine, vipengele vya jumla vya simulizi katika maandiko ni pamoja na mazingira, wahusika, mtazamo wa mwandishi, mtiririko (ploti), na dhamira ya hadithi. ³ Unabii ni tanzu nyingine kuu ya maandiko, aina ya fasihi ambayo inawasilisha ukweli kuhusu Mungu na ulimwengu, unatokana na Roho na ni njia maalum ya ufunuo kutoka kwa Mungu ambayo inajidhihirisha kupitia mtu au kwa njia ya fasihi. ³ Apokaliptiki ni kijitanzu (tawi) cha unabii, na inajumuisha aina mbili kuu za apokalipsi za Kiyahudi, kitabu cha Agano la Kale cha Danieli, na kitabu cha apoliptiki kilicho dhahiri zaidi katika maandiko, yaani kitabu cha Ufunuo.

3

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker