Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 1 6 9

K U T A F S I R I B I B L I A

Mafunzo ya Biblia Kutumia zana za kujifunza katika masomo ya Biblia

S O M O L A 4

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki mijadala, na kutumia maarifa yaliyomo katika somo hili, utaweza: • Kutambua na kuelewa kazi ya zana za kitaalamu katika jitihata zetu za kuelewa maana ya matini. • Kunukuu dhumuni la kutumia zana katika ufasiri wa Biblia, ikijumuisha uwezo wa zana hizo wa kutusaidia kuziba mapengo mbalimbali yaliyopo kati ya ulimwengu wa Biblia na ulimwengu wetu wa sasa, ili kutumia vyema fursa ya uwepo wa zana nyingi bora ambazo zimeibuka katika siku zetu, na thamani ya zana hizo katika kutusaidia kuwa waaminifu zaidi kwa Neno la Mungu kwa kutuwezesha kugundua kwa upya maana halisi ya maandiko katika muktadha wake wa asili. • Kutambua na kuelezea kile kinachochukuliwa kuwa zana za msingi na muhimu katika ufasiri wowotewa kibiblia ikijumuisha upatikanaji wamatoleo ya tafsiri nzuri za Biblia, leksimu za Kiyunani na Kiebrania zilizowekwa kwenye mfumo wa nambari wa Strong , kamusi thabiti ya Biblia, konkodansi, na vitabu vya ufafanuzi wa kieksejesia ( exegetical commentaries ) vinavyoaminika na ambavyo vinajikita zaidi katika maana za kibiblia za kifungu. • Kutambua na kuelezea zana ambazo zinaweza kutoa ufahamu wa ziada katika maana ya maandiko ya Biblia, ikijumuisha tafsiri kadhaa tofauti za Biblia, atlasi ya Biblia na kitabu cha mwongozo wa Biblia, Biblia yenye mada, kamusi ya theolojia, na hatimaye vitabu vya ufafanuzi wa kitheolojia ( thelogical commentaries ) ambavyo vinajikita zaidi katika muktadha wa kitheolojia wa kifungu. • Kuelezea kuhusu lugha tatu ambazo zilitumika katika uandishi wa Biblia (Kiebrania, Kiaramu, na Kiyunani), na kutambua changamoto hasa zinazohusiana na kufanya tafsiri nzuri, ikiwa ni pamoja na ugumu wa matumizi ya maneno, tofauti za kitamaduni, kuzingatia muktadha, na tofauti zilizopo mingoni mwa watafsiri wenyewe. • Kuelezea maana ya konkodansi, leksimu, kamusi, na vitabu vya ufafanuzi, na kuonyesha namna ya kutumia zana hizo katika muktadha wa ufasiri

Malengo ya Somo

4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker