Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 1 7
K U T A F S I R I B I B L I A
Kumbukumbu la Torati 32:4 – Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili . Kutoka 34:6 – Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli . Zaburi 98:3 – Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. Zaburi 100:5 – Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi. Isaya 25:1 – Ee Bwana, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli. Yohana 6:63 – Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. 1 Petro 1:23-25 – Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. 23 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. Ukiongeza kwenye orodha hii ndogo maandiko mengi yaliyopo kuhusu uaminifu wa Mungu, kwa hakika yatakuleta kwenye hoja za msingi za Isaya 55. Mungu analinganisha uhakika wa utimilifu wa Neno lake, kwa maana ya unabii na ahadi zake, na nguvu ya kikaboni ya mvua kutoka mbinguni, ambayo ikishachanganyika na mbegu na ardhi, huzaa matunda mengi. Kimsingi Mungu anamaanisha kwamba Neno lake lina matokeo, ni hakika, linafanikiwa, na lina nguvu kama vile mvua inavyochanganyika na chembe za ardhi. Ni kitu gani kinachotupa uhakika huu wa matokeo? Ahadi hii kwamba Neno la Mungu litaleta matokeo na ustawi inamsingi gani? Uhakika huu umejikita katika tabia yake, ndani ya nafsi yake, katika ukweli wake kama Mungu mwaminifu, Mungu asiyeweza kusema uongo (Tito 1:2), ambaye Neno lake ni kweli na hakika, limethibitishwa milele mbinguni. Daudi aliimba kuhusu uaminifu wa Mungu na kutegemeka kwa Neno lake katika Zaburi 89: “Fadhili za Bwana nitaziimba milele; Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako. 2 Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele; Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.” (Zab. 89:1-2). Katika andiko hili Mungu anatuhakikishia kwamba Neno lake ni kweli. Kwa sababu yeye ni Mungu mwaminifu, Neno lake litatimiza yale ambayo Mungu ameyakusudia na kufanikiwa katika kila jambo, na kila jukumu na kazi ambayo ameliagiza kufanya.
1
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker