Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
1 7 8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
3. Kuepuka kufanya makosa ya kihistoria, kisarufi na kiutamaduni tunapotafuta kutafsiri Neno la Mungu kwa ajili ya maisha yetu wenyewe.
Ujumbe Mkuu wa Biblia
Ujumbe mkuu wa Biblia ni hadithi ya wokovu, na katika Agano maagano yote mawili tunaweza kubainisha mitazamo mitatu katika hadithi hii inayoendelea kujifunua: mleta wokovu, njia ya wokovu na warithi wa wokovu. Hili linaweza kubadilishwa kulingana na dhana ya agano kwa kusema kwamba ujumbe mkuu wa Biblia ni agano la Mungu na wanadamu, na kwamba mitazamo hiyo ni mpatanishi wa agano, msingi wa agano na watu wa agano. Mungu mwenyewe ndiye Mwokozi wa watu wake; ndiye anayethibitisha rehema ya agano lake na wao. Mleta wokovu, Mpatanishi wa agano, ni Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Njia ya wokovu, msingi wa agano, ni neema ya Mungu, inayotoa wito kwa watu wake kuitikia kwa imani na utii. Warithi wa wokovu, watu wa agano, ni Israeli wa Mungu, Kanisa la Mungu. ~ F. F. Bruce. “Bible.” New Bible Dictionary . D. R. W. Wood, ed. (3rd ed). (electronic ed.). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1996, pp. 137-138.
4
II. Zana katika ufasiri wa Biblia
A. Zana za msingi
1. Tafsiri nzuri ya Biblia katika lugha yako ya asili.
2. Leksimu za Kiyunani na za Kiebrania zilizowekwa kwenye mfumo wa nambari wa Strong.
3. Kamusi ya Biblia.
4. Konkodansi yenye mfumo wa nambari wa Strong.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker