Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

1 8 0 /

K U T A F S I R I B I B L I A

A. Biblia iliandikwa katika lugha tatu

1. Kiebrania (Agano la Kale)

a. Ni lugha ya kale (Mizizi ya lugha hiyo ilifuatiliwa hadi mwaka 2400 KK au takriban miaka 4,400 iliyopita). (1) Kwa mtazamo wetu inasomeka “kinyumenyume” (kutoka kulia kwenda kushoto). (2) Ina alfabeti yake, tofauti.

b. Ni lugha thabiti na inatumia lugha za picha (hutumia picha kuwakilisha dhana kama vile “pembe” kuwakilisha nguvu).

c. Ni lugha ya kiuchumi (1) Neno moja la msingi linaweza kuwa na maana nyingi na matumizi tofauti. (2) Katika Kiebrania, Zaburi 23 ni maneno 55 pekee huku KJV katika Kiingereza inatumia maneno 119.

4

2. Kiaramu

a. Ina matumizi ya muda mrefu zaidi ya lugha yoyote inayojulikana. Ilizungumzwa wakati wa Ibrahimu na ingali inazungumzwa na makundi machache leo.

b. Ni lugha ya pili ya Agano la Kale; imetumika katika Mwanzo 31:47; Ezra 4:8-6.18, 7:12-26; Yer. 10:11; Dan. 2:4b-7.28.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker