Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
1 8 2 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Vipi kuhusu kutafsiri Biblia katika lugha ambayo ina rangi tano tu? Unatafsirije neno “zambarau,” kama askari walipomvisha Yesu vazi la zambarau? Muhimu zaidi, tafsiri inawekaje maana ya asili, kwa kuwa wasomaji wote wa Agano Jipya walielewa kwamba rangi ya zambarau iliwakilisha watu wa kifalme na kwamba askari walikuwa wakidhihaki madai ya Yesu kuwa ni mfalme? Vipi ikiwa kuna rangi nyingine tofauti inayowakilisha hadhi ya kifalme? Ikiwa zambarau inawakilisha wafanyabiashara? Ni halali kwa mtafsiri kubadilisha neno hilo, ingawa si neno ambalo maandiko yalitumia?
b. Herufi kubwa au ndogo badala ya viunganishi : Kiyunani hakina neno la kawaida la Kiswahili “ya” (au Kiingereza “ of ”).
c. Maneno mengi kwa dhana ya umoja : Kiingereza kina neno moja tu linalomaanisha upendo, Kiyunani kina maneno kadhaa.
d. Maneno yenye jinsia tofauti na maana tofuati kutemeana na jinsia ya neno husika : lugha nyingi zina miundo ya kiume, ya kike na isio na jinsia, Kiingereza hakina.
4
2. Tofauti za kiisimu na kitamaduni hufanya tafsiri kuwa muhimu.
a. Kilimo, taashira ya kale : baadhi ya tamaduni hazijawahi kuona kondoo lakini hufuga nguruwe kama tu ambavyo Waebrania walivyofuga kondoo. Je, ni sahihi kutumia mnyama kutoka katika utamaduni wao wakati wa kutafsiri?
b. Kutokuwepo kwa dhana fulani katika tamaduni fulani . Katika tamaduni fulani, inaaminika kwamba ni watu wanaosema uongo tu wanaojitetea kwamba hawasemi uongo. Je, unawezaje kutafsiri maneno ya Paulo katika Warumi 9:1 – “Nasema kweli katika Kristo, sisemi uongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu.”
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker