Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

1 9 0 /

K U T A F S I R I B I B L I A

2. Pia ina orodha ya kila kitabu cha Biblia (kama vile Warumi) ambayo mara nyingi hukielezea kitabu: inatoa taarifa kuhusu tarehe, mwandishi na hadhira asilia na inatoa taarifa za kihistoria au kiutamaduni ambazo ni muhimu kwa ajili ya kuelewa ujumbe wa mwandishi.

B. Matumizi ya zana

1. Maelezo na taarifa za utangulizi : Hii ni sehemu moja ya kuanzia ya kujua ni nani aliyeandika kitabu, kiliandikwa lini, na kinashughulikia masuala gani yaliyokuwepo baina ya mwandishi na hadhira asilia.

2. “Nomino” nyingi (watu, mahali, au vitu) unazokutana nazo unaposoma mstari wa maandiko zinaweza kutafutwa katika kamusi ya Biblia ili kukupa ufahamu zaidi wa mahali zilipo, zilimaanisha nini, au jinsi zilivyotumiwa wakati wa Biblia.

C. Uchaguzi wa zana: The New Bible Dictionary (Eerdmans Publishing Co.)

4

VII. Vitabu vya ufafanuzi wa kieksijesia

A. Maelezo kuhusu zana

1. Hiki ni kisaidizi cha kazi ya ufasiri wa Biblia kinachotoa ufahamu wa maana ya maandiko kwa kutoa maoni ya kitaalamu kuhusu sarufi, maana za maneno, masuala muhimu ya juu zaidi na ya chini zaidi.

2. Vitabu vya ufafanuzi wa kieksijesia pia hutoa uelewa wa njia ambazo ukweli wa kihistoria na ufahamu wa utamaduni wa ulimwengu wa Biblia vinaweza kuathiri uelewa wetu wa matini.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker