Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

2 2 4 /

K U T A F S I R I B I B L I A

K I A M B A T I S H O C H A 2 Tuna amini: Tamko la Kanuni ya Imani ya Nikea (8.7.8.7. Mita*) Mch. Dkt. Don L. Davis, 2007. Haki zote zimehifadhiwa. *Wimbo huu umetengenezwa kutoka katika Kanuni ya Imani ya Nikea na unaweza kuimbwa katika ala hizi zenye mita 8.7.8.7. Mita, kama: Shangwe, shangwe, tuna kuabudu wewe, nitamwimbia Mtetezi wangu; Yesu kwetu ni rafiki; njooni, wenye kumngoja Yesu.

Mungu Baba anatawala, yeye aliyezifanya mbingu na nchi. Naam, vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, kwa yeye, viliumbwa na kwa yeye, vilitolewa.

Tuna amini katika Yesu Kristo, Bwana, Mwana pekee wa Mungu, Aliyetolewa, wala hakuumbwa, yeye na Mungu Baba ni mmoja!

Aliyetolewa kutoka kwa Baba, mwenye asili moja naye, kama Mungu na kama nuru; Kwa yeye vitu vyote viliumbwa na Mungu, katika yeye vitu vyote vilipewa uzima. Ambaye kwa ajili yetu sisi sote, kwa ajili ya wokovu, alishuka kutoka mbinguni kuja duniani, Alifanyika mwili kwa uweza wa Roho, kwa kuzaliwa na Bikira mariamu.

Ambaye kwa ajili yetu pia, alisulibiwa kwa mkono wa Pontio Pilato Akateseka, na akazikwa, lakini siku ya tatu, akafufuka.

Kama Maandiko matakatifa yalivyosema, yote yaliyotokea yalikusudiwa kuwa hivyo. Akapaa juu mkono wa kuume wa Mungu, na sasa ameketi katika utukufu mbinguni.

Kristo atakuja tena katika utukufu kuwahukumu walio hai na wafu. Utawala wa ufalme wake hautakuwa na mwisho, kwa kuwa atatawala na kuongoza kama Kiongozi. Tuna mwabudu Mungu, Roho Mtakatifu, Bwana na mpaji wa uzima; Pamoja na Baba na Mwana ametukuzwa, yeye ambaye alinena kupitia manabii.

Na tunaamini katika Kanisa moja, watu watakatifu wa Mungu kwa nyakati zote, Katoliki katika upeo wake, lililojengwa katika msingi wa mitume! Tunatambua ubatizo mmoja, kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu, Tunatazamia siku ya ufufuo – wafu wataishi tena.

Tunatazamia siku hizo zisizokoma, maisha ya Enzi ijazo, Wakati Utawala Mkuu wa Kristo utakapokuja duniani, na mapenzi ya Mungu yatakapo fanyika.

Sifa kwa Mungu, na kwa Kristo Yesu, kwa Roho-Bwana katika utatu. Tunakiri mafundisho ya Kale, tukiling’ang’ania Neno takatifu la Mungu!

[Imetafsiriwa kutokana na shairi la Kiingereza]

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker