Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 2 6 7
K U T A F S I R I B I B L I A
K I A M B A T I S H O C H A 2 6 Hadithi, Thilojia, na Kanisa William J. Bausch. Storytelling: Imagination and Faith . Mystic, Ct: 23rd Publications, 1984. K. 195-199.
Mpaka hatua hii katika kitabu chetu, ukitazama kwa umakini, inaweza kuwa vyema kukiweka pembeni kidogo kwa muda na kuruhusu hadithi na kielelezo (hayo mengine hata hivyo yatarejeshwa tena, katika sura mbili za mwisho) na kuorodhesha mapendekezo kumi ya asili ya kitheolojia. Zoezi hili natumaini halitakuwa zito wala gumu. Litatumika kama njia ya kupata maarifa zaidi, kwa ajili ya kueleweka na kuweka msisitizo kwa maana za kitheolojia ambazo zimetajwa hapa na kule katika sura zilizopita. Hivyo hii ni sura fupi sana na ni aina ya muhtasari wa kitheolojia, mtazamo wa jumla wa namna hadithi zinavyohusiana na theolojia na miundo wa Kanisa. Hadithi zimetungwa kutulazimisha kufikiria uwezekano wa jambo. Kwa kigezo hicho zimewekewa misingi katika tumaini. Hata kwa mfano, hadithi ambayo ni ya kigeni kabisa, bado inafufua uwezekano na kuinua matumaini yetu. Hadithi za kibiblia zinafanya vivyohivyo, ila ni kwa uwazi zaidi kidogo. Dhumuni lake kubwa ni kutushawishi kutazama zaidi ya mipaka yetu na hali ya vikwazo vyetu na kufikiri uajabu uliopo kwa namna ya ajabu. Hadithi zinatukumbusha kwamba mambo tunayo chukulia kuwa ya kawaida kila siku yanaweza kuwa ya kushangaza sana. Katika hadithi kama “Rumors of angels” na Grace abounding, kama chura angeweza kuwa Mwana wa Mfalme, baharia aliyepotea akawa malaika, msafiri akawa Kristo, basi uumbaji wote ungekuwa na uwepo wa sakramenti ukielekeza kwenye hadithi ya “Something more.” Hadithi zinaonyesha kwamba hii inaweza tu kuwa ndivyo ilivyo. Kweli, kuhusiana na hadithi, ni ajizi. Ni jukumu la ubunifu wa hadithi kupangilia kweli na kueleza habari njema kuzihusu. Kwa mfano,” Kweli” ya msingi, kuhusu ufufuo kimsingi ina umuhimu kidogo katika maelezo yake na uthibitisho wake kama kauli ya Yesu wa Nazareti kufufuka kutoka kwa wafu, kuliko nafasi ya msingi ya tumaini. Kilicho muhimu ni matokeo ambayo hadithi ya ufufuo inatupa katika maisha yetu na mtazamo wetu juu ya uzima na kifo. La si hivyo, basi hiyo ni ripoti tu na sio Injili. Hoja ya Kwanza: Hadithi zinatufahamisha kuhusu uwepo wa sakramenti. Hoja ya Pili: Hadithi mara zote huwa ni muhimu kuliko kweli.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker