Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 3 5

K U T A F S I R I B I B L I A

Uhakiki huu unalenga kufuatilia ujumbe wa Mungu tangu tukio halisi lililorekodiwa na muktadha wake hadi tafsiri ya maandiko tuliyo nayo leo. • Vipengele muhimu vya uhakiki wa kisasa wa Biblia vinahusisha uhakiki wa muundo (kufuatilia mapokeo simulizi), uhakiki wa chanzo (kutafuta vyanzo vya maandiko), uhakiki wa lugha (lugha, maneno, na sarufi), uhakiki wa maandishi (nakala za maandishi), uhakiki wa kifasihi (kanuni za fasihi), uhakiki wa kikanoni (jinsi vitabu vilivyochaguliwa), uhakiki wa uandishi (madhumuni ya waandishi), uhakiki wa kihistoria (historia na utamaduni), na uhakiki wa tafsiri. • Bila kujali madai yanayotolewa na wasomi wengi leo, tunaweza kuwa na uhakika kwamba maandiko kwa kweli ni Neno la Mungu linaloishi na kudumu milele.

1

I. Ingawa Imeandikwa na waandishi wanadamu, Biblia imeandikwa na Mungu.

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

A. Majina na vyeo

1. Neno “Biblia” linatokana na neno la Kiyunani biblos (Mt. 1:1) na biblion (Luka 4:17) linalomaanisha “kitabu.”

2. Vitabu vya kale vilivyoandikwa kwenye biblus au mwanzi wa mafunjo ( papyrus reed ), ambacho ndicho chanzo cha neno biblos, ambacho hatimaye kilihusishwa na vitabu vitakatifu vya maandiko (taz. Mk. 12:26; Lk. 3:4; 20:42; Mdo. 1:20; 7:42).

3. “Andiko” au “Maandiko” (yaani, Maandiko Matakatifu ) ( Mk. 12:10; 15.28; Yoh. 2:22; 10:35; Lk. 24:27; Mdo. 17:11; 2 Tim. 3:15; 2 Pet. 3:16 ).

4. Neno la Mungu ( Mk. 7:13; Rum. 10:17; 2 Kor. 2:17; Ebr. 12; 1 Thes. 2:13 )

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker