Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 5 1
K U T A F S I R I B I B L I A
uundaji wa kanoni za maandiko, yote haya yanahusiana na kipengele cha kihistoria cha uhusiano kati ya mpeleka ujumbe na ujumbe husika. ~ Bernard c. Lategan. “Hermeneutics.” The Anchor Bible Dictionary . D. N. Freedman, Ed. Vol. 3. Doubleday: New York: Doubleday, 1997. k. 152-153.
Dhana zifuatazo ni muhtasari wa kweli muhimu ambazo tumejadili na kutafakari katika somo hili juu ya asili, mamlaka, na uvuvio wa maandiko. Kabla hatujaweza kufafanua hemenetiki yetu wenyewe kwa ajili ya kuielewa Biblia, ni lazima tuwe na ujasiri kabisa wa kukiri kwamba maandiko ni Neno la Mungu, na kwamba yanastahili heshima kubwa, uangalifu, umakini, na kujifunza kwa kina kama andiko lililovuviwa na Mungu. Kweli zilizoorodheshwa hapa chini zinakupa fursa nzuri ya kupitia maarifa uliyoyapata katika somo hili. ³ Hemenetiki ni taaluma na tawi la maarifa linahusika na ufasiri, hasa ufasiri wa maandiko. Hemenetiki ya Biblia inajikita hasa katika mbinu na sayansi ya kufasiri Biblia. ³ Kwa namna yoyote ile Biblia lazima ifasiriwe kama kitabu cha kimungu (cha kiroho) na cha kibinadamu, huku tukizingatia kwamba namna zote mbili za kuitazama Biblia (kiroho na kibinadamu) ni za muhimu ili kufahamu na kuelewa kikamilifu asili ya maandiko. ³ Tangu mwanzo, imani ya Kikristo ya kweli imezingatia madhanio fulani ya msingi kuhusu asili ya maandiko, ikijumuisha asili yake ya kimungu, ulazima wa andiko kufasiri andiko, dhana ya ufunuo endelevu ambao unafikia kilele katika ufunuo wa Mungu katika nafsi ya Kristo, na ulazima wa utendaji wa Roho Mtakatifu ili kulielewa Neno la Mungu. ³ Mbinu ya Hatua Tatu ya ufasiri wa Biblia, inayolenga kuchukulia kwa uzito tofauti ya kihistoria na kiisimu (kisarufi) kati ya ulimwengu wa nyakati za Biblia na ulimwengu wetu wa sasa, inahusisha jitihada za kuelewa ujumbe kwa kuzingatia muktadha wake wa asili, kugundua kanuni za Biblia kutoka katika andiko husika, na hatimaye kuhusianisha maana ya andiko na maisha yetu. ³ Ili kulitafsiri Neno la Mungu kwa usahihi, ni lazima tuandae mioyo yetu, akili zetu, na nia zetu kulisoma kwa unyenyekevu na kwa uthabiti, kulichanganua kwa uangalifu, na kulitii kwa moyo wote, yote haya kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
1
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker