Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 5 3

K U T A F S I R I B I B L I A

Uwezo wako wa kutafakari taratibu na kwa umakini na kufanyia kazi maarifa ni muhimu kwa maendeleo yako endelevu na ustawi wako kama kiongozi wa kikristo. Sehemu hii ya somo inakupa fursa ya kujadili na wanafunzi wenzako maswali mahususi ambayo yameibuka katika ufahamu wako kuhusu chimbuko na mamlaka ya maandiko. Dhana ya uvuvio wa maandiko ni msingi wa uwezo wako wa kukua katika Kristo pamoja na kuzitangaza ahadi zake na maneno yake kwa ujasiri katika huduma yako. Fikiria sasa maswali ambayo yamekuja kwenye ufahamu wako kuhusiana na mambo ambayo umejifunza, na mjadili kwa pamoja. Maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuibua maswali yakomwenyewe, wasiwasi au hoja nyingine yoyote. * Je, ni muhimu kwa kila Mkristo kuwa na aina fulani ya “hemenetiki” anapotafuta kuelewa maana ya Biblia? Kwa nini masuala haya ni muhimu kwa walei na pia kwa viongozi (wachungaji, n.k), kwa Wakristo wa kawaida na pia kwa wanazuoni? * Je, kuna njia yoyote ya mwisho ya kujua kwa hakika uhusiano mahususi kati ya viwango vya kimungu na vya kibinadamu vya namna Biblia ilivyoundwa? Nini kinatokea ikiwa hatuwezi kuelezea jambo hili kwa ufasaha; yatupasa kuwa na hofu kupita kiasi? Elezea jibu lako. * Kwa nini ni muhimu sana kuanza kujifunza asili ya Biblia na kweli ambazo Wakristo wameshizikilia na kuziamini katika historia ya Ukristo? * Eleza kwa nini mikakati yote ya kihemenetiki kimsingi ni majaribio ya kuziba pengo kati ya ulimwengu wa nyakati za maandiko na ulimwengu wetu wa sasa? Je, hii kweli inawezekana au ni lazima, ikizingatiwa kwamba kuna karne nyingi zinazo tutenganisha sisi na waandishi wa Biblia? * Ni hatua gani ninazopaswa kuchukua ili kuandaa moyo wangu, akili na utashi wangu kwa ajili ya kulielewa na kulitumia Neno la Mungu? Je, ni changamoto gani kubwa niliyo nayo katika eneo hili? * Je, ni lazima uamini kwamba maandishi ya awali ya Biblia yalikuwa “yasiyo na makosa” na “yasiyoweza kukosea” ili kuamini kwamba yamevuviwa na Mungu na yamepuliziwa “pumzi ya Mungu”? Elezea jibu lako. * Kati ya nadharia zote ulizosoma katika somo hili, ni ipi inayokushawishi zaidi kuhusu asili ya uungu na ubinadamu katika Biblia? Ni ipi isiyostahili kuaminiwa hata kidogo, na kwa nini? * Je, unadhani ni kwa kiwango gani viongozi wa Kikristo wa mijini wanahitaji kuwa na ufahamu kuhusu nadharia za jumla zinazohusiana na uhakiki wa kisasa wa Biblia? Je, elimu hizi huongeza au hufanyika kikwazo kwa

Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi

1

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker