Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 6 1
K U T A F S I R I B I B L I A
Hemenetiki ya Biblia Mbinu ya Hatua Tatu
S O M O L A 2
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, kujadili, na kutumia maarifa yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kutoa ushahidi kuonyesha ni kwa namna gani Mbinu ya Hatua Tatu ni njia fasaha ya ufasiri wa Biblia iliyotengenezwa kutusaidia kuelewa kweli ya maandiko na kuziba pengo kati ya ulimwengu ule wa kale na huu wa sasa. • Kutoa maana ya Mbinu ya Hatua Tatu ya ufasiri wa Biblia, na kuinukuu pasipo kutumia zana saidizi: “Kuelewa maana iliyokusudiwa katika mazingira ya kwanza ya andiko ili tuweze kugundua kanuni za jumla za Kweli ya Neno ambazo zinaweza kutumika katika maisha yetu binafsi ndani ya uhuru wa Roho Mtakatifu.” • Kuonyeha njia ambazo uchambuzi wowote wa Neno la Mungu lazima ufunue maana na ujumbe wa ufunuo wa mwisho wa Mungu kwetu kupitia maisha na kazi ya Yesu Kristo. • Kudhihirisha ujuzi wako juu ya namna Mbinu ya Hatua Tatu inaendana na mbinu ya sarufi ya kihistoria katika kutafsiri maandiko, ambayo inathibitisha maana ya wazi ya andiko, ufunuo endelevu wa Mungu katika Kristo, umoja wa Biblia, na uadilifu na ukweli wa maandiko. • Kuelezea sababu muhimu za kila hatua ya Mbinu ya Hatua Tatu , na kwanini kila hatua husika ni muhimu, ugumu unaoambatana na kila hatua, mtazamo muhimu unaohitajika kuwa nao katika kila hatua, shughuli zinazohusiana na kila hatua, na mfano wa kila hatua katika maandiko. • Kutofautisha kati ya aina za mitazamo inayohitajika kwa kila hatua ya kujifunza Biblia kwa kutumia Mbinu ya Hatua Tatu: unyenyekevu, bidii, na uhuru katika kila hatua. • Kuelezea Mbinu ya Hatua Tatu kwa kutumia 1 Wakorintho 9:1-4 kama kielelezo cha matumizi yake, ukitumia kila hatua ya mbinu hiyo kwa vitendo unapopitia kifungu hiki. • Kuona jinsi uchambuzi wa kifungu fulani cha maandiko lazima ufanyike kwa kuzingatia ujumbe wa sura nzima, sehemu ya kitabu au kitabu kizima cha Biblia, na hatimaye, kwa kuzingatia ujumbe wa Biblia kwetu katika Kristo.
Malengo ya somo
2
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker