Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
7 4 /
K U T A F S I R I B I B L I A
3. Tambua na uchukulie kwa uzito ukweli kuhusu umbali, yaani tofauti kubwa ya nyakati: Sitz im Leben (hali katika maisha).
4. Pata na ujifunze kutumia zana zinazofaa za kujifunza Biblia ambazo zitakusaidia kukupa picha ya muktadha asilia.
E. Mfano: Pasaka, 1 Wakorintho 5:7, 8
III. Hatua ya Pili: Gundua na bainisha kanuni za Jumla.
2
A. Kwa nini tunahitaji kugundua kanuni za jumla?
1. “Kweli za Biblia ni mambo yaliyofichwa”: kweli za kibiblia zinahitaji kufasiriwa , na ufasiri huleta ufahamu.
2. Pasipo kanuni tunabaki na vipande vya kweli visivyo na mpangilio: tunakabiliana na maelfu ya kweli zisizo na muunganiko katika Biblia.
3. Kanuni za jumla huturuhusu kuchota hekima kutokana na uzoefu wa wengine: nguvu ya mifano ya kibiblia, Mit. 24:30-34.
a. Uchunguzi binafsi makini wa hali fulani.
b. Kutafakari na kupembua maana ya mambo hayo.
c. Kutengeneza kanuni (methali) ambayo inaweza kutumika katika mazingira tofauti lakini yanayohusiana.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker