Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 9 1

K U T A F S I R I B I B L I A

II. Hatua ya Pili: Kupata Kanuni za Jumla.

A. Lengo la hatua hii: kutafuta ujumbe muhimu, kweli, agizo, au kanuni ya msingi inayofundisha kweli na kusudi la Mungu kwa watu wote .

1. Andika kwa muhtasari kile unachoamini mwandishi anajaribu kusema.

2. Kuweka taarifa nyingi katika muhtasari ni jambo la kibiblia: Biblia yenyewe inathibitisha mara kwa mara uhalali wa kuweka maelezo katika muhtasari. Mungu hakuweka tu sheria yake yote katika muhtasari wa amri kumi (Kut. 20:1-17; Kum. 5:6-21), bali pia alitoa mihtasari mingine saba ya sheria pia. Zaburi 15 inahifadhi sheria ya Mungu katika kanuni kumi na moja, Isaya 33:15 huiweka katika amri sita; Mika 6:8 inaifupisha katika amri tatu, Isaya 56:1 inaipunguza zaidi kuwa amri mbili; na Amosi 5:4, Habakuki 2:4, na Kumbukumbu 19:2 kila moja imeiweka sheria nzima katika kauli moja ya jumla. Yesu Mwenyewe aliendeleza mapokeo haya kwa kufupisha sheria yote katika kanuni mbili: “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.... Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.” ~ Walter C. Kaiser. An Introduction to Biblical Hermeneutics . p. 276.

2

B. Ufafanuzi wa kanuni ya kibiblia.

1. Tamko katika sentensi rahisi (au msemo, methali) ( ujumbe wa hadithi katika hekaya ndio kanuni yake ).

2. Tamko hilo linaonyesha ukweli ulio wazi unaopatikana ndani ya kifungu cha Biblia.

3. Linakubaliana na mafundisho ya Biblia nzima.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker