Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
9 8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
3. Ruhusu utofauti katika namna za kutendea kazi na kuliishi andiko: Yesu yu hai!
a. Si kila jambo linafaa kila mahali, kila wakati na kwa kila mtu: hatuwezi kujua kwa usahihi namna Bwana anavyoweza kutaka mtu mwingine atendee kazi Neno lake, Yohana 21:20-22.
b. Tunapaswa kutumia uhuru katika utendaji wetu, lakini ndani ya mipaka ya upendo wa Kristo na kwa faida ya kujengana.
(1) 1 Wakorintho 6:12 (2) 1 Wakorintho 10:23 (3) 1 Wakorintho 8:13
2
c. Katika matumizi yako ya Kanuni za Biblia, jifunze kutofautisha kati ya mapendekezo na maagizo (k.m., Mungu ananiagiza kumpenda mke wangu kama Kristo anavyolipenda Kanisa, lakini andiko hili halina tafsiri inayoniamuru kumletea maua na kwenda naye sinema kila wiki!).
E. Kumbuka kwamba kila utendaji wa Neno ni njia tofauti ya kutendea kazi ujumbe mmoja : mambo muhimu.
1. Upendo kwa Mungu na jirani ni amri ya kwanza na ya pili, Mt. 22:36-40.
2. Tunapaswa kutumia uhuru wetu si kama kibali cha kutenda dhambi, bali kama fursa ya kuwapenda wengine, Gal. 5:13.
3. Yote tunayofanya yanapaswa kufanywa kwa manufaa ya jirani zetu, kwa ajili ya kuujenga Mwili, 1 Kor. 10:24.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker