Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
1 1 2 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
³ Leo katika ulimwengu na enzi hii, Kanisa la Yesu Kristo ni ishara na kionjo cha Ufalme uliopo, unaokaliwa na Roho Mtakatifu, dhamana ya urithi kamili. Kanisa sasa, kama wakala na naibu wa Kristo, limepewa mamlaka ya kutangaza na kudhihirisha ushindi wa Kristo dhidi ya Shetani na laana. ³ Athari kuu za taswira ya Utume kama Vita vya Milki ni kwamba Mungu kwa sasa anasimika na kuimarisha tena utawala wake juu ya ulimwengu wake katika Yesu Kristo, na kupitia wakala wake, Kanisa. Mungu ndiye Shujaa ambaye kupitia mpakwa mafuta wake amezishinda nguvu za shetani na madhara ya laana. Utume ni udhihirisho na tangazo la utawala wa Mungu hapa na sasa, na kufanya mataifa kuwa wanafunzi ni kuendeleza utawala wa Mungu kwa kushuhudia kuja kwake katika nafsi ya Yesu wa Nazareti. Sasa ni wakati wa wewe kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu taswira hizi muhimu za utume katika Maandiko. Maswali yafuatayo yameundwa ili kukusaidia kuchunguza kwa kina yale ambayo somo hili linazungumza na maisha yako binafsi na maeneo ambayo somo hili linakupa changamoto binafsi unazopaswa kutendea kazi. Kwa hiyo jitahidi kuwa wazi iwezekanavyo unapochunguza maswali haya na mengine yanayohusiana na somo hili. * Je, umewahi kusoma kwa kina na kwa uwazi taswira ya mapenzi ya kiungu au ile ya Vita vya Milki katika Maandiko, na ikiwa ndivyo, ni mambo gani muhimu uliyogundua kuhusu mada hizo? Je, kuna taswira yoyote kati ya hizi ambayo inakupa ufahamu wa wazi kuhusu “kile ambacho Biblia inazungumza,” hasa kuhusiana na umoja kati ya Agano la Kale na Agano Jipya? * Je, unafikiri mojawapo ya taswira hizi ni muhimu kwa uzoefu wa maisha ya mijini? Kwa nini kuvunjika kwa familia na kukosekana kwa uaminifu katika mahusiano ya mwanamume na mwanamke kunaweza kuathiri vibaya mitazamo ya watu kuhusu taswira ya mapenzi ya kiungu ? * Je, unadhani tunapaswa kushughulika tu na mada ambazo watu hupendezwa nazo au kuzipenda, au tunapaswa kufundisha mambo yote makuu ya Biblia, hata iweje? Elezea jibu lako vizuri. * Je, uhusiano wa Israeli na Bwana unalinganaje na uhusiano wako mwenyewe na Bwana? Je, wewe ni kama Waisraeli au ni tofauti nao? Kwa namna gani?
2
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi
Made with FlippingBook - Online catalogs