Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
1 8 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Maandiko yamefafanua sababu kadhaa za umaskini, kutia ndani majanga ya asili na misiba (k.m., njaa, ukame, vimbunga, n.k.), uvivu na uzembe wa watu binafsi (k.m., maamuzi mabaya, tabia mbaya, uvivu, mioyo migumu, n.k.), na uonevu na matendo ya ukosefu wa haki yanayotendwa na watu wenye nguvu (k.m., unyanyasaji, unyonyaji, nk). Neno “maskini” katika Maandiko linahusianishwa na dhana mbalimbali zinazotumika kama visawe, kutia ndani “mjane,” “yatima,” na “mgeni.” Viwango au maagizo ya agano la Mungu yanaakisi moyo wake kwa ajili ya maskini na wahitaji, kutia ndani mambo kama vile maagizo ya Sheria (Torati) kuhusu mavuno na masazo yake, haki katika mahakama ambapo mambo yote, hatua zote, na shughuli zote zilipaswa kufanyika kwa uaminifu na kwa haki, bila kujali hali ya mtu; na rasilimali zilipaswa kugawanywa katika mwaka wa Sabato, na maskini walipewa sehemu ya mazao ya mashamba na mizabibu. Maana ya viwango hivi kwa jamii ya agano la Mungu iko wazi: katika shughuli zao zote, Watu wa Mungu walipaswa kuakisi moyo wa Mungu kwa maskini, kwa msingi wa ukombozi wa Mungu kwao wakati wa “Kutoka”, na walipaswa kuonyesha shalom ya Bwana katika mahusiano yao yote na kushughulika kwao na watu wengine. Lengo letu la sehemu hii, Shalom katika Jamii ya Agano , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Dhana ya maskini imejengwa juu ya maono ya kibiblia ya shalom, au ukamilifu: shalom ni neno la Kiebrania linalomaanisha «ukamilifu wa jamii ya wanadamu katika ushirika na Mungu na baina yao mmoja kwa mwingine.» • Vipengele vya kibiblia vya shalom ni pamoja na uzima na afya njema, usalama na ulinzi, maelewano kati ya majirani, ustawi na utoshelevu wa mali, na kukosekana kwa uovu na migogoro – Amani ya kweli na kamilifu. Hili pia linajumuisha wazo la shalom kama utoaji wa Mungu kwa msingi wa neema yake, unaohusishwa na ujio wa Masihi ambaye ni Mfalme wa shalom, pamoja na shalom kama kiwango cha maisha kwa watu wa Mungu. • Umaskini ni kunyimwa shalom ya Mungu; baraka na upaji wake vilitolewa ili kuzuia kutokea kwa umaskini, na amri na maagizo ya Mungu kwa jamii ya agano zilikusudiwa kuhakikisha haki na uadilifu kati ya watu wa Yehova. Uaminifu kwa agano ulikusudiwa kwa ajili ya kuendeleza shalom kati ya Waisraeli kwa sababu ya kule kutii sauti yake na kutimiza masharti yake. • Mungu anajitambulisha na maskini, yaani, ni mpango wake kuwainua na kuwabariki kutoka katika hali zao, kuwaadhibu wale wanaowadhulumu, na kuwataka watu wake waonyeshe hali ya kujali ile ile aliyo nayo kwa niaba ya waliovunjika moyo, maskini, na waliokandamizwa. Kutoka ni
4
Made with FlippingBook - Online catalogs