Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

This is the Swahili edition of the Cornerstone Student Workbook

Kinajumuisha Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini cha Dk. Alvin Sanders

Mtaala wa Cornerstone

The Urban

Mini s t r y I ns t i tute ni huduma ya Wor ld Impac t , I nc .

Toleo Rasmi la Ithibati

Alvin Sanders | Mch. Dk. Don L. Davis Mch. Terry G. Cornett | Mch. Ryan Carter

u

b

c

a

t

h

i

a

K

M

i

z

w

n

a

u

n

f

a

SWAHILI

Mtaala wa Cornerstone Toleo Rasmi la Ithibati Kitabu cha Mwanafunzi

Mtaala wa Cornerstone: Toleo Rasmi la Ithibati – Kitabu cha Mwanafunzi

© 2023. The Urban Ministry Institute. © 2024. Toleo la Kiswahili. Haki zote zimehifadhiwa. Kimetafsiriwa na Sam Gripper. Kimehaririwa na Eresh Tchakubuta.

Hairuhusiwi kunakili, kusambaza na/au kuuza vitabu hivi, au matumizi mengine yoyote pasipo idhini, isipokuwa kwa matumizi yanayo ruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Haki Miliki ya Mwaka 1976 au kwa idhini ya maandishi kutoka kwa mmiliki. Maombi ya idhini yatumwe kwa maandishi kwa taasisi ya:

The Urban Ministry Institute 3701 East 13th Street North Suite 100 Wichita, KS 67208

ISBN: 978-1-62932-071-7

Kimechapishwa na TUMI Press Kitengo cha World Impact, Inc.

The Urban Ministry Institute ni huduma ya World Impact, Inc.

Nukuu zote za Maandiko, isipokuwa kama imeonyeshwa vinginevyo, zimechukuliwa kutoka katika SWAHILI BIBLE UV050(MCR) series® Haki Miliki © 1997, iliyochapishwa na The Bible Society of Tanzania. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote za kimataifa zimehifadhiwa.

K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Mtaala wa Cornerstone

T h e U r b a n

M i n i s t r y I n s t i t u t e

n i h u d u m a y a W o r l d I m p a c t , I n c .

Toleo Rasmi la Ithibati

Alvin Sanders | Mch. Dr. Don L. Davis Mch. Terry G. Cornett | Mch. Ryan Carter

Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.

~ Waefeso 2:19-22

TUMI Press 3701 East 13th Street North Suite 100 Wichita, Kansas 67208

Yalioyomo

Muhtasari

9

Kuhusu Wakufunzi

13

Utangulizi wa Mtaala wa Cornerstone, Toleo Rasmi la Ithibati

15

Maelezo ya Kozi

17

Mahitaji ya Kozi

Sehemu ya I: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini

29

Utangulizi wa Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini

Somo la 1 Tafakari Fupi ya Kitheolojia

31

Somo la 2 Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini Somo la 3 Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini

41

51

Somo la 4 Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini

61

Sehemu ya II: Biblia & Theolojia

Fungu la Kwanza: Masomo ya Biblia

79

Utangulizi ya Fungu la Masomo ya Biblia

Somo la 1 Uongofu na Wito: Neno Liumbalo Somo la 2 Kutafsiri Biblia: Mbinu ya Hatua Tatu

83

101

Somo la 3 Ushahidi wa Agano la Kale kuhusu Kristo na Ufalme Wake: Kutolewa kwa Ahadi Somo la 4 Ushahidi wa Agano la Kale Kuhusu Kristo na Ufalme wake: Kupingwa kwa Masihi

133

159

Fungu la Pili: Theolojia na Maadili

181

Utangulizi wa Fungu la Theolojia na Maadili

Somo la 1 Ufalme wa Mungu: Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu Somo la 2 Mungu Baba: Mungu katika Utatu – Ukuu wa Mungu Somo la 3 Mungu Mwana: Yesu, Masihi na Bwana wa Wote – Alikufa Somo la 4 Mungu Roho Mtakatifu: Nafsi ya Roho Mtakatifu

185

201

223

245

Sehemu ya III: Huduma na Utume

Fungu la Kwanza: Huduma ya Kikristo

267

Utangulizi wa Fungu la Huduma ya Kikristo

Somo la 1 Theolojia ya Kanisa: Kanisa katika Ibada

271

Somo la 2 Misingi ya Uongozi wa Kikristo: Kiongozi wa Kikristo kama Mchungaji – Poimenes Somo la 3 Kutekeleza Uongozi wa Kikristo: Uongozi Bora wa Ibada

295

319

Somo la 4 Huduma ya Kukamilisha Watakatifu Huduma ya Mahubiri – Kerygma

339

Fungu la Pili: Utume katika Miji

367

Utangulizi wa Fungu la Utume katika Miji

Somo la 1 Misingi ya Utume wa Kikristo: Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo

371

Somo la 2 Uinjilisti na Vita ya Rohoni: Kufungwa kwa Mtu Mwenye Nguvu Somo la 3 Mkazo kuhusu Uzazi: Ukuaji wa Kanisa – Kuongezeka katika Idadi na Ubora

405

419

Somo la 4 Kutenda Haki na Kupenda Rehema: Haki na Ishuke – Maono na Theolojia ya Ufalme

445

Viambatisho

475

Kiambatisho cha 1: Kanuni ya Imani ya Nikea

477

Kiambatisho cha 2: Orodha ya Kukagua Kazi za Sehemu ya I: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini Kiambatisho cha 3: Orodha ya Kukagua Kazi za Sehemu ya II na ya III: Mafungu ya Cornerstone

478

479

Kiambatisho cha 4: Sampuli ya Fomu ya Ripoti ya Usomaji

480

Kiambatisho cha 5: Sampuli ya Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko

481

Kiambatisho cha 6: Kuandika Kazi Yako

485

Kiambatisho cha 7: Orodha ya Hati Muhimu na Chati za Theolojia katika Picha

Mpango wa Tathmini ya Huduma (MAP)

489

Mchakato wa MAP: Wanafunzi wa Stashahada

491

C3-303 Kazi ya Tathimini ya Huduma: Makubaliano ya Mpango wa Huduma Chini ya Uangalizi

492

Mpango wa Mafunzo ya Kozi: C3-303 Kazi ya Tathmini ya Huduma

505

Mwongozo kwa ajili ya Mahojiano ya Kwanza Na Mshauri wa Taaluma, Mwanafunzi, na Mchungaji Msimamizi Mwongozo kwa ajili ya Mahojiano ya Mwisho Na Mshauri wa Taaluma, Mwanafunzi, na Mchungaji Msimamizi

507

MUHTASAR I / 9

Kuhusu Wakufunzi

Wakati ambapo watu katika jamii ambazo hazina rasilimali za kutosha wanafadhaishwa na hali ngumu za maisha, kanisa la mahali pamoja linaweza kuwa mwanga wa matumaini. Alvin Sanders alijifunza hili kutokana na uzoefu wa maisha yake binafsi. Wakati akihudumu kama kiongozi wa mjini katika kitongoji cha pili kwa vurugu nchini, msiba ulitokea. Ufyatulianaji risasi wa polisi ulioambatana na kauli za ubaguzi wa rangi ulitikisa mtaa huo. Kama jawabu, Alvin alianzisha kanisa bunifu ambalo linaendelea kutunza, kuhudumia, na kutia moyo watu kutoka katika matabaka yote ya maisha. Kupitia uzoefu huu aligundua utume wake binafsi: kumfuata Mungu kwa bidii, kupenda familia yake, na kuwekeza kwa wale wanaowekeza kwenye maisha ya watu maskini. Alvin ni mtu wa kanisa kutoka moyoni. Baada ya upandaji kanisa na uchungaji, alihudumu kama kiongozi wa dhehebu katika Kanisa la Evangelical Free Church of America (EFCA) kwa miaka saba. Akiwa huko aliongoza EFCA All People Initiative . Chini ya uongozi wake EFCA ilikua kutoka 13% ya makutaniko yao yaliyoainishwa kama ya mijini, ya kikabila, au yenye makabila mchanganyiko hadi 22%. Pia aliandika kitabu chake kiitwacho Bridging the Diversity Gap . Kutokana na mapenzi yake kwa viongozi wa kanisa, kuhamia kwake World Impact mwaka 2015 lilikuwa jambo la kawaida ambalo kila aliyemfahamu angelitarajia. Historia yake kitaaluma ni pamoja na Shahada ya Sayansi katika Masomo ya Biblia kutoka Chuo Kikuu cha Kikristo cha Cincinnati na Shahada ya Uzamili katika Dini na Huduma ya Mjini kutoka Chuo cha Trinity Evangelical Divinity . Alihitimu ngazi ya Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) katika Uongozi wa Kielimu kutoka Chuo Kikuu cha Miami. Tangu 2004 amehudumu kama profesa msaidizi katika seminari mbalimbali nchini kote. Katika wakati wake wa kupumzika, Alvin ni msomaji mwenye bidii na anapenda kufuatilia timu za michezo anazozipenda. Anamshukuru mke wake wa pekee sana, Caroline, ambaye amedumu katika huduma ya ushauri katika mji wao wa Cincinnati. Wamebarikiwa kuwa na binti wawili wazuri ajabu. Mnamo Novemba 2017, Alvin aliteuliwa kuwa Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa World Impact.

10 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Mchungaji Dkt. Don L. Davis ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Urban Ministry Institute na ni Makamu wa kwanza wa Rais wa World Impact. Alisoma katika Chuo cha Wheaton College na Chuo cha Uzamili cha Wheaton na kuhitimu kwa ufaulu wa kiwango cha juu, yaani Summa Cum Claude, katika ngazi ya Shahada (1988) na Shahada ya Uzamili (1989) katika Masomo ya Biblia na Theolojia ya Utaratibu. Alipata Shahada yake ya Uzamivu katika Masuala ya Dini (Theolojia na Maadili) katika chuo kikuu cha Iowa School of Religion. Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi na Makamu wa Rais Mwandamizi wa World Impact , anasimamia mafunzo ya wamishonari wa mijini, wapanda makanisa, na wachungaji wa majiji, na kufanya uwezeshaji kupitia fursa za mafunzo kwa watendakazi Wakristo wa mijini katika uinjilisti, ukuaji wa kanisa, na umisheni wa upainia. Pia anaongoza Mpango wa Mafunzo huria kwa wale wanaosoma wakiwa mbali, vilevile anawezesha Mafunzo ya Kiuongozi kwa mashirika na madhehebu kadhaa kama Prison fellowship, The Evangelical Free Church of America na The Church of God in Christ. Dkt. Davis, ambaye ametunukiwa tuzo nyingi za ualimu na za kitaalamu, amewahi kuwa profesa na Mkuu wa vitivo katika taasisi kadhaa za kitaalamu zenye hadhi ya juu, baada ya kuhadhiri na kufundisha kozi za dini, theolojia, falsafa, na mafunzo ya Biblia katika taasisi za elimu ya juu kama vile Chuo cha Wheaton, Chuo Kikuu cha St. Ambrose, Programu ya Shahada ya Uzamili ya Theolojia ya Chuo Kikuu cha Houston, Kitengo cha Dini cha Chuo Kikuu cha Iowa, na Taasisi ya Mafunzo ya Ibada ya Robert E. Webber. Ameandika idadi kubwa ya vitabu, mitaala, na nyenzo za kujifunzia ili kuwaandaa viongozi wa mijini, ikijumuisha mtaala wa mafunzo wa Capstone (hii ni programu mama ya TUMI yenye moduli 16 za hadhi ya mafunzo ya seminari, yanayotolewa kupitia mfumo wa elimu ya masafa), Mizizi Mitakatifu: Kidokezo cha Namna ya Kurejesha Mapokeo Makuu , ambayo inaangazia namna makanisa ya mijini yanavyoweza kufanywa upya kupitia kugundua upya imani halisi, sahihi ya kihistoria; na Mweusi na Mwanadamu: Kumgundua Upya M.L. King kama Nyenzo ya Theolojia na Maadili ya Weusi . Dkt. Davis pia ameshiriki katika mihadhara ya kitaalamu kama the Staley Lecture series, makongamano ya kufanywa upya kama Promise Keeper Rallies na miungano ya kithiologia kama The University of Virginia Lived Theology Project Series. Vilevile alipokea tuzo ya heshima ya mwanafunzi mashuhuri ( Alumni Fellow Award ) kutoka Chuo Kikuu cha Iowa cha Sanaa na Sayansi za Kiliberali mnamo 2009. Dkt. Davis pia ni mwanachama wa The Society of Biblical Literature, na The American Academy of Religion .

MUHTASAR I / 11

Mchungaji Terry Cornett (B.S., M. A., M.A.R.) ni Mkuu wa Taaluma wa Heshima wa The Urban Ministry Institute huko Wichita, Kansas. Ana digrii kutoka Chuo Kikuu cha Texas huko Austin, Chuo cha Uzamivu cha Wheaton, na Chuo cha Theolojia ya C. P. Haggard katika Chuo Kikuu cha Azusa Pacific. Terry alihudumu kwa miaka 23 kama mmisionari wa mjini chini ya World Impact kabla ya kustaafu mwaka wa 2005. Wakati huo alihudumu Omaha, Los Angeles, na Wichita ambako alihusika katika huduma za upandaji makanisa, elimu, na mafunzo ya uongozi. Mchungaji Ryan Carter ni Mkuu wa Taaluma wa The Urban Ministry Institute. Yeye ni mzaliwa wa Houston, Texas. Kabla ya kujiunga na wafanyakazi wa World Impact Wichita mwaka wa 2008, yeye na mke wake, Amber, walihudumu miongoni mwa jamii maskini za mijini huko Houston na Dallas. Mnamo Septemba 2018, baada ya miaka kumi ya kuhudumu kama mmishonari huko Wichita, Ryan alijiunga na jopo la wafanyakazi wa TUMI kama Msanidi wa Nyenzo zetu. Ryan ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Houston (BA katika Falsafa) na Seminari ya Theolojia ya Dallas (ThM katika Mafunzo ya Agano la Kale na Elimu ya Kikristo). Uzoefu wake wa huduma unajumuisha huduma za kimishenari, watoto na vijana, mchungaji mshiriki, upandaji makanisa, na mchungaji. Carter na mkewe wana watoto wawili wa kiume, Benjamin (3/10/09) na Nathaniel (12/09/10).

MUHTASAR I / 13

Utangulizi wa Mtaala wa Cornerstone , Toleo Rasmi la Ithibati

Karibu kwenye Mtaala wa Cornerstone , fursa yako mpya ya kuandaliwa kwa ajili ya huduma bora katika Kanisa!

Changamoto: Uhitaji Mkubwa, Hakuna Muda , Fedha Chache Ukweli mchungu anaoukabili mtu yeyote anayewaandaa wachungaji na wahudumu walei wanaotumika katika jamii zilizo hatarini, ni ule wa uhaba. Pesa na muda ni adimu na finyu sana kwa viongozi hawa hodari wanaomtumikia Mungu katika jamii maskini kuweza kujihusisha katika masomo ya muda marefu katika mfumo ulio rasmi. Wanafanya kazi isiyo ya kawaida huku mara nyingi wakiwa katika ajira za kudumu na wakipambania huduma inayokua. Maelfu ya wafanyakazi wa Kikristo walioko mijini ambao wangenufaika na mitaala yetu bora na yenye kina cha kiwango cha seminari kama Mtaala wa Capstone, hawana ama muda au fedha za kuikamilisha. (Muda wa wastani kwa wanafunzi wanaosoma na kufanya kazi kumaliza moduli kumi na sita za Capstone ni miaka mitatu hadi minne). Kukabiliana na Changamoto: Mtaala wa Cornerstone Ili kukabiliana na hitaji hili kuu, tumebuni mtaala huu wa kipekee, Mtaala wa Cornerstone. Ukiwa umechaguliwa kutoka kwenye masomo maalum ya kimkakati ya Capstone, na kuongezewa moduli ya “ Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini ” ya Dkt. Alvin Sanders, tuliunda kozi hii kwa ajili ya wale ambao hawana uhakika wa kuwa na muda au fedha za kukamilisha mtaala wetu mkubwa zaidi wa Capstone. Muda wa kukamilisha sehemu tatu za Cornerstone ni sawa na moduli tatu pekee za Capstone. Tuliunda nyenzo hii ili kuwasaidia wanafunzi hawa kuzifikia nyenzo muhimu pasipo kudhabihu ubora au fursa za huduma zao. Cornerstone itapunguza kwa kiasi kikubwa muda na gharama zinazohitajika kwa ajili ya shule ya kawaida ya Biblia au masomo ya seminari au hata Mtaala wa Capstone, pasipo kupoteza uaminifu wetu ama kwa Kweli ya kibiblia au kwa mafunzo ya huduma kwa vitendo. Kuandaliwa Kupanda, Kuchunga, na Kutumikia Kanisa! Nyenzo za mtaala wa Cornerstone zinajumuisha kozi ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini na nyenzo zilizotolewa moja kwa moja kutoka kwenye moduli za Capstone, zikitoa kweli zake muhimu

14 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

kutoka kwenye maeneo manne ya idara zake (Masomo ya Biblia, Theolojia na Maadili, Huduma ya Kikristo, na Utume katika Miji). Tumeweka pamoja masomo ya Cornerstone ili kukupatia utaratibu thabiti wa mafunzo kwa wakati unaofaa na gharama nafuu. Mafunzo yetu yatakupatia ithibati, yataboresha ujuzi wako wa Maandiko, na kukuwezesha kuhudumu vyema kama mchungaji, kiongozi mlei, au Mkristo mtenda kazi mahali unapoishi na kufanya kazi. Mungu amekuita na kukupa karama, na tunatumaini kukuona ukitimiza wito wake kwenye maisha yako, ili upate kumletea heshima Mwokozi wetu katika kila jambo ulifanyalo. Kwa hiyo, ninakupa changamoto ya kutimiza huduma ya Bwana kwa ajili yako, yote katika nia ile ile kama ya Paulo anapomuasa Timotheo, “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” (2 Tim. 2:15). Fahamu kwamba ukijitoa kwa Mungu kama mtu aliyekubaliwa, utatimiza wito wake na kuzaa matunda ya kiroho ambayo yatamtukuza Kristo na kumpendeza Mungu. Mungu akubariki sana katika masomo yako, ufuasi wako, na huduma yako! Kwa ujasiri mkubwa katika Neno la Mungu la milele lenye kuponya

na kubadilisha, Dkt. Don Davis Wichita, Kansas Februari 1, 2023

MUHTASAR I / 15

Maelezo ya Kozi

Mtaala wa Cornerstone ni mafunzo ya hali ya juu kwa viongozi wa Kikristo ambao huenda wasihitaji au wasiwe na muda wa kupata mafunzo ambayo huchukua miaka kadhaa. Mtaala huu unatoa maarifa na ujuzi kuhusu uongozi wa Kikristo katika muundo mfupi. Mafunzo haya bora yanajumuisha sehemu kuu tatu. Sehemu ya I: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini inatoa mtazamo mpya wa jinsi ya kuwawezesha wale wanaoishi katika hali ya umaskini. Wanafunzi wanapata nafasi ya kuchunguza mawazo yao kuhusu wale wanaoishi katika hali ya umaskini na kujifunza jinsi ya kufanya kazi ya kimungu na yenye matokeo kati yao. Sehemu ya II: Biblia na Theolojia Fungu la Mafunzo ya Biblia linalenga kuwaandaa wanafunzi kuhudumia Neno la Mungu kwa usahihi na ufanisi. Mtumishi wa Kristo lazima awe na umahiri katika mambo yaliyomo katika Biblia, ajinyenyekeze kwa maagizo yake, na afundishe kweli yake. Fungu la Theolojia na Maadili linalenga kuwaandaa wanafunzi kueleza na kutetea kweli za msingi za Imani ya Kikristo. Somo alilopenda zaidi Yesu mwenyewe lilikuwa Ufalme wa Mungu. Ulikuwa ni ujumbe wake wa wokovu, mpango mkuu, na theolojia yake pendwa. Sehemu hii inaangazia hadithi ya ufalme – Mfalme na Ufalme wake – na kuona umuhimu wake katika maisha ya ufuasi binafsi na huduma. Sehemu ya III: Huduma & Umisheni Fungu la Huduma ya Kikristo linalenga kuwaandaa wanafunzi kuchunga kwa ustadi kundi la Mungu, yaani Kanisa. Yesu wa Nazareti ameinuliwa kama kichwa juu ya watu wake wapya, Kanisa. Tunazingatia jukumu muhimu la Kanisa katika ufuasi binafsi na wa jumuiya. Hakika, hakuna ufuasi au wokovu nje ya kazi ya Mungu ya kuokoa kupitia Kanisa. Fungu la Utume katika Miji linalenga kuwaandaa wanafunzi kumwakilisha Kristo kama mabalozi wa Ufalme wake. Tunazingatia imani ya Kikristo kama mwitikio wa utume, wito wa kwenda kwa mataifa na kumtangaza Yesu wa Nazareti kama Bwana na Mfalme wa utawala wa Mungu.

16 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Baada ya kukamilisha Mtaala wa Cornerstone , utakuwa na uwezo wa: • Kufanya kazi ya ukombozi dhidi ya umaskini inayomtukuza Mungu na kusaidia kufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri zaidi, • Kutumia Neno la Mungu kwa usahihi na kwa ufanisi, • Kuelezea na kutetea kweli za msingi za Kikristo, • Kuchunga kwa ustadi kundi la Mungu, Kanisa, • Kumwakilisha Kristo kama balozi wa Ufalme wake. Tunaamini kwamba mafunzo utakayopokea kupitia Mtaala wa Cornerstone yatakuwezesha kumtukuza Mungu kwa kumtumikia Kristo na Kanisa lake.

MUHTASAR I / 17

Mahitaji ya Kozi

Sehemu ya I: Mahitaji ya Kozi ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini

Ili kukamilisha mafunzo haya ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini utahitaji nyenzo zifuatazo: • Biblia • Nakala ya kitabu cha Uncommon Church: Community Transformation for the Common Good , kilichoandikwa na Dk. Alvin Sanders • Nakala ya kitabu cha Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini , kilichoandikwa na Dk. Alvin Sanders • Ratiba ya kozi (Mshauri wako atatoa hii) • Orodha ya Kukagua Kazi (Angalia kiambatisho. Mshauri wako atatoa hii) • Fomu ya Ripoti ya Usomaji (Angalia kiambatisho. Mshauri wako atatoa hili) • Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko (Ona kiambatanisho. Mshauri wako atatoa hili). Mahudhurio na ushiriki darasani . . . . . . 30% Alama 60 Mistari ya Kukumbuka . . . . . . . . . . . 10% Alama 20 Majaribio . . . . . . . . . . . . . . . 15% Alama 30 Maswali ya kujadili . . . . . . . . . . . 10% Alama 20 Usomaji na kazi za kufanyia nyumbani . . . . . 15% Alama 30 Mtihani wa Mwisho . . . . . . . . . . . . 20% Alama 40 Jumla: 100% Alama 200 Mambo ya Kuzingatia katika Utoaji Maksi Kuhudhuria kila kipindi ni moja ya masharti ya msingi ya kozi hizi. Kukosa kipindi kutaathiri matokeo yako. Ikiwa una dharura isiyoepukika itakayokulazimu kukosa kipindi, tafadhali mjulishe mkufunzi wako mapema. Ukikosa kipindi ni jukumu lako kutafuta taarifa kuhusu kazi na mazoezi yaliyotolewa, na kuongea na mkufunzi wako pale inapobidi kufanya na kukabidhi kazi kwa kuchelewa. Sehemu kubwa ya mafunzo yanayohusiana na kozi hii Muhtasari wa Mfumo wa Kutunuku Matokeo na Uzito wa Gredi

Vitabu na Nyenzo Zinazohitajika

Mahitaji ya Kozi

Mahudhurio na Ushiriki Darasani

18 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

hufanyika kupitia mijadala. Kwa hivyo, unahimizwa na kutarajiwa kushiriki kikamilifu katika kila kipindi cha kozi hii. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika jumbe zake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa mdomo au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. (Ona Kiambatisho husika kupata Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko. Mkufunzi wako atakupatia fomu hii)* Baada ya kila somo kutakuwa na maswali matano ya kujadili ambayo mshauri wako atatoa. Ikiwa mnakutana mtandaoni, utajadili maswali haya kwenye jukwaa na wanafunzi wenzako katika WIU. Ikiwa darasa lako ni la ana kwa ana, Mshauri wako ataamua jinsi gani/lini mjadala utafanyika darasani kwako. Mkufunzi wako anaweza kutoa kazi za darasani na kazi za nyumbani za aina mbalimbali wakati wa vipindi vya masomo au anaweza kuziandika katika Kitabu cha Mwanafunzi ulichonacho. Ikiwa una swali lolote kuhusu kile kinachohitajika kuhusiana na kazi hizi au muda wa kuzikusanya, tafadhali muulize mkufunzi wako. Ni muhimu kwa kila mwanafunzi kusoma maeneo yote ambayo inampasa kusoma katika vitabu husika vya kozi hii au katika Maandiko Matakatifu ili kujiandaa kwa ajili ya mijadala darasani. Tafadhali hakikisha unajaza na kukabidhi kwa Mkufunzi wako “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” kila wiki. Kutakuwa pia na fursa ya kupata alama za ziada endapo utasoma zaidi ya ulivyoagizwa. (Angalia Kiambatisho husika kupata Fomu ya Ripoti ya Usomaji. Mkufunzi wako atakupatia fomu hii).* Mwishoni mwa kila somo, utapewa jaribio. Baada ya Somo la 4, utapewa Mtihani wa Mwisho (huruhusiwi kutumia vitabu wala madokezo) ambao una maswali kuhusiana na maudhui ya kozi nzima. Mshauri wako atakupa tarehe za kuukamilisha na taarifa nyingine utakapopokea nakala ya Mtihani wa Mwisho. Gredi za Ufaulu Kozi ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini ni ya ama kufaulu au kufeli, ambapo kufaulu ni kupata maksi kuanzia 70% na kuendelea. Kufanya kazi kwa kuchelewa bila ruhusa au kushindwa kuwasilisha kazi kutaathiri daraja lako, kwa hivyo tafadhali pangilia muda wako mapema na, endapo utapata changamoto yoyote inayoweza kupelekea kuchelewesha kazi, uwasiliane na mkufunzi wako mapema iwezekanavyo.

Kukariri Mistari ya Biblia

Maswali ya Kujadili

Kazi za Darasani na za Nyumbani

Kazi za Usomaji

Majaribio na Mtihani wa Mwisho

* Washauri wanaweza kupakua Orodha ya Kukagua Kazi, Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko, na Fomu ya Ripoti ya Usomaji kutoka kwenye Dashibodi ya WIU.

MUHTASAR I / 19

Sehemu ya II na ya III: Mahitaji ya Kozi ya Mtaala wa Cornerstone

• Biblia (kwa madhumuni ya kozi hii, Biblia yako inapaswa kuwa tafsiri [mf. BHN, SUV, NEN, SRUV, au NIV, NASB, RSV, KJV, NKJV, n.k. ikiwa utatumia Biblia ya Kiingereza], na sio Biblia iliyofafanuliwa [mf. The Living Lible, The Message ]). • Kila fungu katika mtaala wa Cornerstone limeainisha vitabu vya kiada ambavyo vinatakiwa visomwe na kujadiliwa katika muda wote wa kujifunza kozi hiyo. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya mtaala wa Cornerstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumientree.com ili kupata orodha ya sasa ya vitabu vya kiada na vitabu vya rejea vinavyohitajika kwa ajili ya fungu hili mahususi la kozi hii. • Davis, Don L., Terry Cornett na Don Allsman. Theolojia Katika Picha: Orodha ya A-Z ya Vielelezo, Chati, Michoro na Makala Muhimu za TUMI . Wichita, KS: TUMI Press, 2019. • Daftari na kalamu kwa ajili ya kuchukua maelezo na kufanyia kazi za darasani. Mahudhurio na ushiriki darasani . . . . . . 30% Alama 90 Mazoezi . . . . . . . . . . . . . . . 20% Alama 60 Mistari ya Kukumbuka . . . . . . . . . . . 20% Alama 60 Kazi za ufafanuzi wa Maandiko . . . . . . . 10% Alama 30 Kazi za huduma . . . . . . . . . . . . . 10% Alama 30 Usomaji na kazi za kufanyia nyumbani . . . . . 10% Alama 30 Jumla: 100% Alama 300 Mambo ya Kuzingatia katika Utoaji Maksi Kuhudhuria kila kipindi ni moja ya masharti ya msingi ya kozi hizi. Kukosa kipindi kutaathiri matokeo yako. Ikiwa una dharura isiyoepukika itakayokulazimu kukosa kipindi, tafadhali mjulishe mkufunzi wako mapema. Ukikosa kipindi ni jukumu lako kutafuta taarifa kuhusu kazi na mazoezi yaliyotolewa, na kuongea na mkufunzi wako pale inapobidi kufanya na kukabidhi kazi kwa kuchelewa. Sehemu kubwa ya mafunzo yanayohusiana na kozi hii Summary of Grade Categories andWeights

Vitabu vya Kiada

Mahitaji ya Kozi

Mahudhurio na Ushiriki Darasani

20 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

hufanyika kupitia mijadala. Kwa hivyo, unahimizwa na kutarajiwa kushiriki kikamilifu katika kila kipindi cha kozi hii. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika jumbe zake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa mdomo au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. (Ona Kiambatisho husika kupata Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko. Mkufunzi wako atakupatia fomu hii)* Tafadhali, ona Utangulizi wa kifa fungu kupata Maandiko mahususi ya Kukariri kwa fungu husika. Neno la Mungu ni zana yenye nguvu ambayo Mungu anaitumia ili kuwaandaa watumishi wake kwa kila kazi ya huduma aliyowaitia (2 Tim. 3:16-17). Ili kutimiza matakwa ya kozi hii, lazima uchague kifungu cha Biblia na kufanya uchambuzi wa kina (yaani, eksejesia au ufafanuzi wa Maandiko) kwa kila kifungu . Kazi yako iwe na kurasa tano ziliyochapwa kwa kuacha nafasi mbili kati ya mistari au kuandikwa vizuri kwa mkono, na iweze kushughulikia mojawapo ya vipengele mbalimbali vya nafsi na kazi ya Mungu Baba vilivyoangaziwa katika kozi hii. Ni shauku na matumaini yetu kwamba utashawishika kikamilifu na kuamini juu ya uwezo wa Maandiko kuleta badiliko na athari chanya katika maisha yako na ya wale unaowahudumia. Unapoendelea kujifunza kozi hii, uwe huru kuongeza mistari kadhaa katika uchambuzi wako (takriban mistari 4-9) kuhusu jambo ambalo ungependa kujifunza kwa kina. Maelezo ya kazi hii yanapatikana kwenye ukurasa wa 23, na yatajadiliwa katika kipindi cha utangulizi cha kozi hii. Pia tazama Utangulizi wa kila fungu kwa maelekezo zaidi kuhusu Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko. Matarajio yetu ni kwamba wanafunzi wote watatumia mafunzo haya kivitendo katika maisha yao na katika majukumu yao ya kihuduma. Mwanafunzi atakuwa na jukumu la kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo kwa kutumia kanuni alizojifunza katika mazingira halisi ya huduma. Maelezo ya kazi hii yanapatikana kwenye ukurasa wa 25, na yatajadiliwa katika kipindi cha utangulizi cha kozi hii. Mkufunzi wako anaweza kutoa kazi za darasani na kazi za nyumbani za aina mbalimbali wakati wa vipindi vya masomo au anaweza kuziandika katika Kitabu cha Mwanafunzi ulichonacho. Ikiwa una swali lolote kuhusu kile kinachohitajika kuhusiana na kazi hizi au muda wa kuzikusanya, tafadhali muulize mkufunzi wako.

Kukariri Mistari ya Biblia

Kazi za Ufafanuzi wa Maandiko

Kazi za Huduma

Kazi za Darasani na za Nyumbani

MUHTASAR I / 21

Kila fungu katika mtaala wa Cornerstone limeainisha vitabu vya kiada ambavyo vinatakiwa visomwe na kujadiliwa katika muda wote wa kujifunza kozi hiyo. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya mtaala wa Cornerstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumientree.com ili kupata orodha ya sasa ya vitabu vya kiada na vitabu vya rejea vinavyohitajika kwa ajili ya fungu hili mahususi la kozi hii. Ni muhimu kwa kila mwanafunzi kusoma maeneo yote ambayo inampasa kusoma katika vitabu husika vya kozi hii au katika Maandiko Matakatifu ili kujiandaa kwa ajili ya mijadala darasani. Tafadhali hakikisha unajaza na kukabidhi kwa Mkufunzi wako “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” kila wiki. Kutakuwa pia na fursa ya kupata alama za ziada endapo utasoma zaidi ya ulivyoagizwa. (Angalia Kiambatisho husika kupata Fomu ya Ripoti ya Usomaji. Mkufunzi wako atakupatia fomu hii).* Mwishoni mwa kila fungu, Mshauri wako atakupa mtihani wa fungu husika la kozi (huruhusiwi kutumi vitabu vya kiada wala madokezo) ambao utaufanyia nyumbani. Utaulizwa swali ambalo litakusaidia kutafakari juu ya kile ulichojifunza katika fungu husika na jinsi kinavyoathiri jinsi unavyofikiria au kufanya huduma kwa vitendo. Mshauri wako atakupa tarehe za kuukamilisha na taarifa nyingine utakapopokea nakala ya Mtihani wa fungu husika. Fomu ya Kukagua Kazi inapatikana katika Viambatisho. Gredi za ufaulu Mwishoni mwa kozi hii, gredi zifuatazo zitatolewa na kuhifadhiwa kwenye mbukumbu za kila mwanafunzi. A – Kazi Bora D – Inaridhisha (Wastani) B – Nzuri Sana F – Hairidhishi (Feli) C – Nzuri I – Isiyokamilika Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako

Kazi za Usomaji

Mtihani wa Mwisho wa kila Fungu

Fomu ya Kukagua Kazi

* Washauri wanaweza kupakua Orodha ya Kukagua Kazi, Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko, na Fomu ya Ripoti ya Usomaji kutoka kwenye Dashibodi ya WIU.

22 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote.

Masharti ya Cheti cha Cornerstone Ili kupata Cheti cha Cornerstone, mwanafunzi lazima atimize masharti yafuatayo: • Kukamilisha mahitaji yote ya kozi kwa kila fungu la Mtaala wa Cornerstone na kupata ufaulu wa angalau 70% katika kila fungu. • Kukamilisha kozi ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini . Credit kwa ajili ya Cheti cha TUMI Mwanafunzi analiyekamilisha masomo ya ngazi ya Cheti ya Cornerstone anaweza kuendelea na masomo yake ya TUMI na kufanyia kazi mojawapo ya kozi zetu za ngazi ya cheti zenye credit hours 32. Kazi iliyofanywa kwa ajili ya cheti cha Cornerstone itamnufaisha mwanafunzi huyo kwa njia zifuatazo: • Cheti cha Mafunzo ya Kitheolojia ya Mijini (yaani, Certificate in Urban Theological Studies, kwa ufupi CUTS) - Cheti cha Cornerstone kitahesabiwa kama credit hours 6 kuelekea CUTS. • Cheti katika Mafunzo ya Uongozi wa Kikristo ( Christian Leadership Studies , CLS) - CLS ni cheti kinachotunukiwa wale wanaokamilisha moduli zote 16 za Capstone. Cheti cha Cornerstone kitahesabiwa kama credit hours 6, au sawa na moduli 3, kuelekea CLS. Mwanafunzi anaweza kutimiza muda wa mafunzo uliosalia kwa kukamilisha moduli 13 zozote atakazochagua kutoka katika mtaala wa Capstone.

MUHTASAR I / 23

Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko Kama sehemu ya ushiriki wako katika Mtaala wa Cornerstone, kwa kila fungu la kozi hii utahitajika kufanya ufafanuzi, yaani eksejesia (uchambuzi wa ndani wa andiko) juu ya kifungu fulani cha Neno la Mungu. Kusudi la kazi hii huu ya ufafanuzi wa Maandiko ni kukupa fursa ya kufanya uchambuzi wa kina wa kifungu muhimu kuhusu asili na kazi ya Neno la Mungu. Unapojifunza mojawapo ya vifungu vya Maandiko yaliyoorodheshwa chini ya “Kazi za Fungu la Kozi” mwanzoni mwa kila Sehemu, tunatumaini kwamba utaweza kuonyesha jinsi andiko hicho kinavyoangazia au kuweka wazi umuhimu wa Neno la Mungu kwa ajili ya hali yetu ya kiroho na kwa ajili ya maisha yetu pamoja katika Kanisa. Pia tunatamani kwamba Roho akupe ufahamu kuhusu jinsi unavyoweza kuhusianisha maana yake moja kwa moja na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, pamoja na jukumu la uongozi ambalo Mungu amekupa kwa sasa katika kanisa na huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya eksejesia , ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika ? 2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa ni pamoja na sisi leo ? 3. Ni kitu gani Roho Mtakatifu ananiagiza kufanya kupitia kanuni hii, leo, katika maisha na huduma yangu ? Baada ya kuwa umeyajibu maswali haya katika kujifunza kwako kibinafsi, hapo sasa utakuwa tayari kuendelea kuandika ulichokigundua katika kazi uliyopewa . Angali hapa chini mfano wa muhtasari wa kazi yako: 1. Eleza kile unachoamini kuwa ndio mada kuu au wazo kuu la andiko ulilochagua. 2. Eleza kwa muhtasari maana ya andiko hilo (unaweza kufanya hivi katika aya mbili au tatu, au, ukipenda, kwa kuandika ufafanuzi mfupi wa mstari kwa mstari juu ya kifungu husika).

Dhumuni

Mpangilio na Muundo

24 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

3. Eleza kanuni kuu moja hadi tatu au maarifa ambayo kifungu hiki kinatoa kuhusu Yesu Kristo na kazi yake. 4. Eleza jinsi kanuni moja, kadhaa, au zote zinaweza kuhusiana na yafuatayo: a. Kiroho chako binafsi na namna unavyotembea na Kristo b. Maisha na huduma yako katika kanisa lako la mahali pamoja c. Hali au changamoto katika jamii yako kwa ujumla. Kwa msaada au mwongozo, tafadhali uwe huru kusoma vitabu vya rejea vya kozi hii na/au vitabu vya mafafanuzi ( commentaries ), na kutumia maarifa yaliyomo katika vyanzo hivyo katika kazi yako. Unapotumia maarifa au mawazo ya mtu mwingine kujenga hoja zako, hakikisha unatambua kazi za waandishi husika kwa kutaja vyanzo vya taarifa hizo. Astahiliye heshima apewe heshima yake. Tumia marejeleo ya ndani ya maandishi ( in-text-refences ), tanbihi ( footnotes ), au maelezo ya mwisho ( endnotes ). Njia yoyote utakayochagua kutaja rejea zako itakubalika, ilimradi 1) utumie njia hiyo moja katika kazi nzima, na 2) uonyeshe pale unatumia mawazo ya mtu mwingine, na umtambue mwandishi husika kwa kumtaja. (Kwa maelezo zaidi, angalia katika Kiambatisho cha Namna ya Kuandika Kazi Yako: Mwongozo wa Kukusaidia Kutambua Waandishi wa Vitabu vya Rejea ). Kabla hujakabidhi kazi yako, hakikisha inasifa zifuatazo: • Imeandikwa au kuchapwa vizuri na inasomeka na kueleweka. • Ni uchambuzi wa mojawapo ya vifungu hapo juu. • Imekusanywa kwa wakati (haijacheleweshwa). • Ina urefu wa kurasa 5. • Inafuata muhtasari au mpangilio uliotolewa hapo juu, na imeandikwa kwa namna ambayo msomaji ataweza kuelewa. • Inaonyesha jinsi kifungu husika kinavyohusiana na maisha na huduma leo. Usiruhusu maagizo haya yakuogopeshe; hii ni kazi ya kujifunza Biblia! Unachohitaji kuonyesha katika kazi hii ni kwamba ulisoma andiko husika, umeeleza kwa muhtasari maana yake, ukaweza kupata kanuni chache muhimu kutoka katika andiko hilo, na kuzihusianisha na maisha na huduma yako mwenyewe. Kazi ya ufafanuzi inabeba alama 60 na inawakilisha 20% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha kwamba unaifanya kazi yako kuwa bora na yenye maarifa ya kutosha ya Neno la Mungu.

Utoaji Maksi

MUHTASAR I / 25

Kazi ya Huduma Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo (Waebrania 4:12). Mtume Yakobo anaweka msisitizo zaidi juu ya kuwa watendaji wa Neno la Mungu, sio wasikiaji tu, tukijidanganya wenyewe. Tunahimizwa kulifanyia kazi, kulitii. Anaongeza kusema kwamba kupuuza nidhamu hii ni sawa na sisi kujitazama sura zetu za asili katika kioo na mara tunapoondoka tunasahau asili yetu (sis ni nani) na tulichokusudiwa kuwa. Katika kila hali, mtendaji wa Neno la Mungu atabarikiwa katika kila atendalo (Yakobo 1:22-25). Shauku yetu ya dhati ni kwamba uweze kutumia maarifa unayojifunza kwa vitendo, ukiihusianisha elimu hii na masuala na mahitaji halisi katika maisha yako binafsi, na huduma yako ndani ya kanisa lako na kupitia kanisa lako. Kwa hivyo, kama sehemu mojawapo muhimu kwa ajili ya kukamilisha Mtaala wa Cornerstone utatakiwa kubuni namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo kwa ajili ya kila fungu la kozi hii, ambapo utaweza kuwashirikisha wengine sehemu ya maarifa ambayo umejifunza. Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia kutimiza takwa hili la kujifunza kwako. Unaweza kuchagua kuwa na muda wa kujifunza na mtu binafsi, kutumia madarasa ya Shule ya Jumapili, vikundi vya vijana au watu wazima, au hata kwa kupata nafasi ya kuhudumu mahali fulani. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unajadili na hadhira baadhi ya maarifa uliyojifunza kutoka darasani. (Bila shaka, unaweza kuchagua kuwashirikisha baadhi ya maarifa kutoka katika kazi yako ya Kieksejesia ya moduli hii). Uwe huru na tayari kubadilika na kuendana na mazingira yoyote unapofanya kazi yako. Ifanye iwe yenye ubunifu na inayoruhusu kusikiliza mitazamo tofauti kwa nia ya kujifunza. Fanya uchaguzi mapema kabisa kuhusu aina ya muktadha ambao unatamani kutumia kushirikisha watu wengine maarifa haya na kisha mshirikishe Mkufunzi wako juu ya maamuzi hayo. Panga hayo yote mapema na epuka kusubiri dakika za mwisho kuamua na kutekeleza kile unachotaka katika kazi yako. Baada ya kutekeleza kazi yako, andika kwa ufupi (ukurasa mmoja) tathmini ya kazi yako na umkabidhi mkufunzi wako. Mfano wa muhtasari wa Kazi ya Huduma ni kama ifuatavyo: 1. Jina lako 2. Eneo ulilolitumia na hadhira uliyowashirikisha.

Dhumuni

Mpangilio na Muhtasari

26 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

3. Muhtasari wa namna muda wako ulivyoenda, namna ulivyojisikia na namna watu walivyoitikia. 4. Ulijifunza nini kupitia mchakato mzima wa kazi yako. Kazi ya huduma inabeba alama 30 ambazo zinawakilisha 10% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha unashirikisha yale uliyojifunza kwa ujarisi na ripoti yako iwe yenye kueleweka vizuri.

Utoaji Maksi

Sehemu ya I

Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini

UTANGUL I Z I WA KAZ I YA K I UKOMBOZ I DH I D I YA UMASK I N I / 29

Utangulizi wa Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini

Karibu kwenye mafunzo ya Dk. Alvin Sanders kuhusu dhana ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini. Iwe unafanya kazi ya kujitolea au unahudumu katika huduma ya wakati wote, mafundisho haya yanatoa mtazamo mpya wa jinsi ya kuwawezesha wale wanaoishi katika hali ya umaskini. Njia hii ya kujifunza itakuwezesha kuchunguza mawazo yako kuhusu wale wanaoishi katika hali ya umaskini na jinsi ya kufanya kazi yenye ufanisi miongoni mwao. Mtazamo huu unatoa njia mpya na ya kimapinduzi ya kushirikiana na kuingiliana na wale wanaoishi katika jumuiya zenye mazingira duni, hapa Marekani na duniani kote. Tazama video ya Dk. Don Davis, Fursa ya Kuishi Mtazamo wa Kiukombozi dhidi ya Umaskini , inayozungumzia jinsi tunavyohitaji mtazamo wa wazi, wa kibiblia na wenye mvuto kuhusu maana ya kuendesha huduma yenye kuleta tumaini la maisha katika jumuiya zenye umaskini. Maelezo ya Kozi Kusudi la kozi hii ni kukusaidia ili uweze kufanya aina ya kazi katikati ya jamii maskini ambayo itampa Mungu heshima na kukusaidia kutimiza shauku yako ya kufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri. • Somo letu la kwanza, Tafakari Fupi ya Kitheolojia , linatoa theolojia rahisi na ya vitendo kwa ajili ya kazi ya kupambana na umaskini. Tutazungumza juu ya mada tatu ambazo zinafafanua kwa nini tunafanya kile tunachofanya. • Somo la pili, Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini , linaonyesha aina ya kazi ya kupambana na umaskini ambayo kwa kawaida hutokana na asili yetu ya dhambi. Tutazungumza juu ya kile ambacho kazi yetu itazalisha ikiwa hatuzingatii kujitambua. • Somo la tatu, Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini , inafafanua lengo la shughuli zetu. Tutachunguza aina tatu za kazi ya kupambana na umaskini zilizopo na jinsi mwitikio wetu kwa kazi ambayo Kristo amefanya msalabani unapaswa kututamanisha kujielekeza katika ukombozi wa maisha ya watu na mitaa yetu.

30 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

• Somo la nne, Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini , linaweka wazi hali ya kiroho ya Mapokeo Makuu ya Kanisa. World Impact inakualika kutendea kazi maarifa haya katika maisha yako kama njia ya kukabiliana na kazi hatarishi ya kupambana na umaskini, na kuyafanya kuwa kichocheo cha kukua katika imani yako. Malengo ya Kozi Baada ya kukamilisha kozi hii ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini, utakuwa na uwezo wa: • Kueleza theolojia fupi ya kibiblia kuhusu kazi ya kupambana na umaskini. • Kuchambua kazi ya kupambana na umaskini na kubaini mazoea na mitazamo yenye sumu (hatarishi). • Kuwa na tafakuri tunduizi na ya kina juu ya kazi ya kupambana na umaskini ili kuioanisha na kazi ya ukombozi ya Mungu katika Kristo. • Kutekeleza dhamira ya kujenga kazi ya kupamana na umaskini katika msingi wa nidhamu thabiti za kiroho ambazo zinawakilisha Mapokeo Makuu ya Kanisa.

SOMO LA 1 | TAFAKAR I FUP I YA K I THEOLOJ I A / 31

Tafakari Fupi ya Kitheolojia

S OMO L A 1

Ukurasa wa 25  1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maarifa ya somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kufanya upya fikra na mtazamo wako kuhusu watu wanaoishi katika umaskini. • Kutafakari jinsi mawazo yako ya awali kuhusu wale walio katika umaskini yanahusiana na mada kuu za Biblia. • Kutoa theolojia fupi ya vitendo kuhusiana na kazi ufanyayo ya kupambana na umaskini. Omba sala ifuatayo: Yesu, wewe ni Mfalme wa Utukufu na Mfalme wa Uumbaji. Utufundishe kutambua njia za ufalme wako ili tuweze kushiriki kama wakaaji waaminifu na wacha Mungu katika kipindi hiki cha kati ya ulimwengu uliovunjika na ufalme ujao wa Mungu. Amina. Hitimisha kipengele hiki kwa kusikiliza wimbo ya “Pendo Kuu la Mungu” na utafakari Maandiko ambayo umesoma hivi punde. Ningekuwa na uwezo wa kubadilisha hali iliyopo, ningefanya hivyo ili kumpa kila Mkristo shauku ya kujifunza Biblia yake. Katika miongo kadhaa ya huduma, nimeamini kuwa tatizo namba moja tunalokabiliana nalo ni kukosa ufahamu wa Biblia. Ninajua nilipoanza kusoma Biblia na kuipa thamani yake stahiki, ilibadili mwelekeo wa imani yangu. Natumai kila Mkristo atakuwa na ushuhuda huu wakati fulani katika maisha yake. Hali ya umaskini ni mada kubwa tunayokutana nayo katika Maandiko yote. Jambo moja kuhusu mada hii ambayo kwa kawaida hupuuzwa ni ukweli kwamba wahusika wengi wa Biblia waliyaishi maisha yao ya imani wakiwa katika umaskini. Kitabu kizima cha Kutoka kinahusu jinsi Mungu alivyolikomboa taifa maskini la watumwa, akionyesha ukarimu kwa kuwapa nchi kuwa milki yao wenyewe. Yesu alizaliwa katika umaskini, aliishi na kufanya kazi katikati ya watu maskini, na alikemea matumizi mabaya ya mali. ~ Common Prayer: A Liturgy for Ordinary Radicals. Soma Mathayo 25:31-46. Tafakari na andika kanuni zinazoweza kutendewa kazi katika maisha.

Malengo ya Somo

1

Ibada

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

32 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Moja ya sababu kwa nini nadhani mada hii haitambuliwi ni unyanyapaa ambao mara nyingi unaelekezwa kwa wale walio katika hali ya umaskini. Unyanyapaa huu ni imani ya kawaida (lakini si ya kibiblia) kwamba wale walio katika umaskini wanastahili kuwa huko. Sote tumeathiriwa na dhana kali ya maadili ya kazi ya waprotestanti. Hii ni imani kwamba ikiwa tutakuwa tumeandaliwa vizuri, ikiwa tutakuwa makini, na waangalifu vya kutosha katika matumizi yetu ya fedha umaskini hautatupata. Lakini hiyo si picha ambayo Biblia inatoa. Bila shaka, mojawapo ya sababu za umaskini ni maamuzi yasiyo ya hekima kimaadili. Lakini sio sababu pekee. Kwa mfano, Luka 16:19 31 inaonyesha kwamba mtu anaweza kuwa maskini kwa sababu ya kupuuzwa. Si vigumu kupata mifano ambapo wananchi wanafanya kazi kwa bidii, lakini watu wananyonywa na viongozi mafisadi na wala rushwa wa viwanda, taasisi na/au serikali. Miongoni mwa sababu nyingine za umaskini tunazopata katika Maandiko ni hali ya hewa, magonjwa, uzee, kupoteza mwenzi wa maisha bila kutarajia – orodha ni ndefu. Sisi sote tumeathiriwa na anguko linaloelezewa katika Mwanzo 3, na umaskini ni mojawapo ya matokeo ya anguko hilo. Hatua ya kwanza katika kuwawezesha watu waishio katika umaskini ni kutambua kwamba Biblia inazungumzia umaskini kama hali, si utambulisho. Kuangalia umaskini kwa njia hii ni muhimu kwa sababu ni msingi wa kazi ya kiukombozi dhidi ya umaskini. Tunaweza kufanya kazi katikati ya watu washio katika umaskini kwa namna isiyo hatarishi kwa sababu Ufalme wa Mungu uko hapa. Acha muhtasari huu mfupi ukuingize katika utafiti wa kina, huku ukifanya upya mawazo ambayo unaweza kuwa nayo kuhusu watu waishio katika umaskini na mitaa yao.

1

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

Tamka na/au imba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho).

Kanuni ya Imani ya Nikea

Kariri Mathayo 25:45 kwa kutumia Biblia ya kawaida (si toleo lililofafanuliwa), kisha ujisahihishe mwenyewe kwa kutumia Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko.

Kukariri Maandiko

Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, rejelea ratiba ya kozi hii ili kuona kazi zinazopaswa kufanyika kabla ya mkutano wako ujao wa darasa na ukamilishe kazi zilizo hapa chini: Soma yafuatayo: • Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini – “Utangulizi” na “Tafakari Fupi ya Kitheolojia” (uk. 11-22)

Kazi

SOMO LA 1 | TAFAKAR I FUP I YA K I THEOLOJ I A / 33

• Kanisa lisilo la kawaida: Mabadiliko ya Jamii kwa Manufaa ya Wote – Dibaji na Efrem Smith – Sura ya 3: Yesu Alifanya, Sio Yesu Angefanya: Yesu na Hali ya Umaskini – Sura ya 6: Imani na Matendo: Kuondoa Mvutano Kati ya Uinjilisti na Utetezi wa Haki Andika muhtasari wa kila usomaji wa kitabu kwa maneno yasiyozidi aya moja au mbili kwa kila muhtasari. Katika muhtasari huu, tafadhali toa uelewa wako bora zaidi wa kile unachofikiri kilikuwa jambo kuu katika usomaji. Usijali sana juu ya kutoa maelezo; andika tu kile ambacho unaona kuwa jambo kuu linalozungumziwa katika sura hiyo ya kitabu. Tumia Fomu ya Ripoti ya Usomaji. Wasilisha Fomu uliyojaza kwa ajili ya kila kitabu (ikiwa unasoma kozi hii kwa kutumia World Impact U, tumia upau wa kijani wa “Wasilisha Kazi” juu ya ukurasa wowote katika kozi yako ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini katika WIU). Mfano Halisi Mtumishi kijana wa mjini ambaye anasimamia mafunzo ya watu wanaojitolea kwa ajili ya programu ya kufundisha masomo ya ziada kwa niaba ya shule mojawapo katika mtaa maskini amekuja kwako kutafuta ushauri. Kazi yake ni kutoa semina elekezi kabla ya watenda kazi hao wa kujitolea kupewa watoto wa kufanya nao kazi. Amegundua kuwa mara kwa mara anaingia kwenye shida. Katika kila semina elekezi mjadala unazuka miongoni mwa watenda kazi wapya wa kujitolea kuhusu sababu za umaskini. Kundi moja linasema kwamba watu ni maskini kwa sababu walifanya maamuzi mabaya katika maisha yao. Wengine wanadai kuwa watu ni maskini kwa sababu ya ukosefu wa haki za kiuchumi. Ni nadra sana kuona kundi lolote likinukuu Maandiko ili kujenga hoja zao. Utampa ushauri gani?

1

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

KUJENGA DARALA

34 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Tafakari Fupi ya Kitheolojia

Dk. Alvin Sanders

MAUDHUI

Somo hili linatoa theolojia rahisi ya vitendo kuhusu kazi ya kupambana na umaskini. Tutazungumza juu ya mada tatu ambazo zinafafanua kwa nini tunafanya kile tunachofanya. Malengo yetu ya somo hili la Tafakari Fupi ya Kitheolojia ni kukuwezesha wewe: • Kufanya upya fikra na mtazamo wako kuhusu watu wanaoishi katika umaskini. • Kutafakari jinsi mawazo yako ya awali kuhusu wale walio katika umaskini yanahusiana na mada kuu za Biblia. • Kutoa theolojia fupi ya vitendo kuhusiana na kazi ufanyayo ya kupambana na umaskini. Wakristo wana uwezekano mkubwa zaidi kuliko wasio Wakristo kuuona umaskini kama matokeo ya kushindwa kwa mtu binafsi. Mtazamo huu hupelekea walio katika umaskini kuchukuliwa kama “miradi” badala ya watu wa kutumikia, jambo ambalo silo Mungu alilokusudia. Biblia inatoa maagizo muhimu kuhusu jinsi tunavyopaswa kuwatendea walio katika umaskini. Tutachunguza kanuni za Agano la Kale za uwezeshaji na kisha kuangazia mambo mawili tunayoyajua kuhusu Yesu: aliwapendelea maskini, na alionya dhidi ya utajiri.

Muhtasari Ukurasa wa 25  2

1

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

I. Umaskini ni Mada Inayopatikana katika Agano la Kale na Agano Jipya Kadhalika.

Muhtasari wa Maudhui ya Video

Ukurasa wa 26  3

A. Kanuni za Uwezeshaji za Agano la Kale

Ukurasa wa 27  4

1. Ufafanuzi: Kumwezesha mtu ni kutoa njia za fursa ya kuboresha hali yake.

2. Katika Agano la Kale tunaona kwamba:

a. Uangalifu usio wa kawaida ulipaswa kutolewa katika kuhakikisha kwamba haki inatendeka kuhusu wale waliokuwa maskini (Kut. 23:6; Am. 5:12; Zab. 10:2, 9).

SOMO LA 1 | TAFAKAR I FUP I YA K I THEOLOJ I A / 35

b. Nyakati zote, baadhi ya matunda na mboga zilipaswa kuachwa mashambani ili maskini wakusanye (Law. 19:9-10).

c. Hakuna riba ambayo iliyoruhusiwa kutozwa kwenye mikopo kwa ajili ya wale walioishi katika umaskini (Kut. 22:25).

d. Kila baada ya miaka mitatu zaka ilitolewa kwa yatima na wajane (Kum. 14:28-29).

e. Kila baada ya miaka saba mashamba yalipumzishwa ili yasitumike kwa faida ya wamiliki bali kwa ajili ya wahitaji wapate kuvuna mazao ambayo yaliota yenyewe (Kut. 23:10-11; Law. 25:3-6).

1

f. Watumwa walipaswa kuachiliwa baada ya miaka sita ya utumishi (Kut. 21:2).

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

g. Kila mwaka wa hamsini (Mwaka wa Yubile) ardhi zilipaswa kurejeshwa kwa wamiliki wake wa awali (Law. 25:8-17).

B. Yesu aliwapendelea maskini.

Ukurasa wa 27  5

1. Tunaona namna ambavyo Kristo alionyesha kuwajali kipekee maskini katika huduma yake duniani (Luka 4:18-20).

a. Yesu alifanya huduma yake kama mtu wa maisha ya kawaida (Mk 2:15-17)

b. Mji wa Nazareti alimozaliwa haukuwa na hadhi katika jamii (Yohana 1:44-45).

c. Kuzaliwa kwake katika zizi la ng’ombe ilikuwa tabia ya watu walio katika umaskini (Luka 2:7).

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker