Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
MUHTASAR I / 11
Mchungaji Terry Cornett (B.S., M. A., M.A.R.) ni Mkuu wa Taaluma wa Heshima wa The Urban Ministry Institute huko Wichita, Kansas. Ana digrii kutoka Chuo Kikuu cha Texas huko Austin, Chuo cha Uzamivu cha Wheaton, na Chuo cha Theolojia ya C. P. Haggard katika Chuo Kikuu cha Azusa Pacific. Terry alihudumu kwa miaka 23 kama mmisionari wa mjini chini ya World Impact kabla ya kustaafu mwaka wa 2005. Wakati huo alihudumu Omaha, Los Angeles, na Wichita ambako alihusika katika huduma za upandaji makanisa, elimu, na mafunzo ya uongozi. Mchungaji Ryan Carter ni Mkuu wa Taaluma wa The Urban Ministry Institute. Yeye ni mzaliwa wa Houston, Texas. Kabla ya kujiunga na wafanyakazi wa World Impact Wichita mwaka wa 2008, yeye na mke wake, Amber, walihudumu miongoni mwa jamii maskini za mijini huko Houston na Dallas. Mnamo Septemba 2018, baada ya miaka kumi ya kuhudumu kama mmishonari huko Wichita, Ryan alijiunga na jopo la wafanyakazi wa TUMI kama Msanidi wa Nyenzo zetu. Ryan ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Houston (BA katika Falsafa) na Seminari ya Theolojia ya Dallas (ThM katika Mafunzo ya Agano la Kale na Elimu ya Kikristo). Uzoefu wake wa huduma unajumuisha huduma za kimishenari, watoto na vijana, mchungaji mshiriki, upandaji makanisa, na mchungaji. Carter na mkewe wana watoto wawili wa kiume, Benjamin (3/10/09) na Nathaniel (12/09/10).
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker