Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
18 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
hufanyika kupitia mijadala. Kwa hivyo, unahimizwa na kutarajiwa kushiriki kikamilifu katika kila kipindi cha kozi hii. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika jumbe zake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa mdomo au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. (Ona Kiambatisho husika kupata Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko. Mkufunzi wako atakupatia fomu hii)* Baada ya kila somo kutakuwa na maswali matano ya kujadili ambayo mshauri wako atatoa. Ikiwa mnakutana mtandaoni, utajadili maswali haya kwenye jukwaa na wanafunzi wenzako katika WIU. Ikiwa darasa lako ni la ana kwa ana, Mshauri wako ataamua jinsi gani/lini mjadala utafanyika darasani kwako. Mkufunzi wako anaweza kutoa kazi za darasani na kazi za nyumbani za aina mbalimbali wakati wa vipindi vya masomo au anaweza kuziandika katika Kitabu cha Mwanafunzi ulichonacho. Ikiwa una swali lolote kuhusu kile kinachohitajika kuhusiana na kazi hizi au muda wa kuzikusanya, tafadhali muulize mkufunzi wako. Ni muhimu kwa kila mwanafunzi kusoma maeneo yote ambayo inampasa kusoma katika vitabu husika vya kozi hii au katika Maandiko Matakatifu ili kujiandaa kwa ajili ya mijadala darasani. Tafadhali hakikisha unajaza na kukabidhi kwa Mkufunzi wako “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” kila wiki. Kutakuwa pia na fursa ya kupata alama za ziada endapo utasoma zaidi ya ulivyoagizwa. (Angalia Kiambatisho husika kupata Fomu ya Ripoti ya Usomaji. Mkufunzi wako atakupatia fomu hii).* Mwishoni mwa kila somo, utapewa jaribio. Baada ya Somo la 4, utapewa Mtihani wa Mwisho (huruhusiwi kutumia vitabu wala madokezo) ambao una maswali kuhusiana na maudhui ya kozi nzima. Mshauri wako atakupa tarehe za kuukamilisha na taarifa nyingine utakapopokea nakala ya Mtihani wa Mwisho. Gredi za Ufaulu Kozi ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini ni ya ama kufaulu au kufeli, ambapo kufaulu ni kupata maksi kuanzia 70% na kuendelea. Kufanya kazi kwa kuchelewa bila ruhusa au kushindwa kuwasilisha kazi kutaathiri daraja lako, kwa hivyo tafadhali pangilia muda wako mapema na, endapo utapata changamoto yoyote inayoweza kupelekea kuchelewesha kazi, uwasiliane na mkufunzi wako mapema iwezekanavyo.
Kukariri Mistari ya Biblia
Maswali ya Kujadili
Kazi za Darasani na za Nyumbani
Kazi za Usomaji
Majaribio na Mtihani wa Mwisho
* Washauri wanaweza kupakua Orodha ya Kukagua Kazi, Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko, na Fomu ya Ripoti ya Usomaji kutoka kwenye Dashibodi ya WIU.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker