Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
190 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
2. Kuzaliwa kwake kunawakilisha uvamizi wa utawala wa Mungu katika utawala wa Shetani, Luka 1:31-33.
3. Ujumbe wake ulikuwa kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia, Mk 1:14-15.
4. Mafundisho yake yanawakilisha maadili ya Ufalme, Mt. 22.37-38.
5. Miujiza yake inafunua kwa watu wote wapate kuona mamlaka na uweza wake wa kifalme, Mk 2:8-12.
1
6. Kutoa kwake pepo kunawakilisha “kufungwa kwa mtu mwenye nguvu,” Lk 11:14-20.
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
7. Maisha yake na matendo yake yanaonyesha utukufu wa Ufalme, Yohana 1:14-18.
8. Kifo chake kinawakilisha kushindwa kwa Shetani, na adhabu ya dhambi, Kol. 2:15.
II. Pili, Utawala wa Mungu Unazinduliwa na Kutambuliwa kupitia Yesu akiwa Christus Victum , Shujaa Ambaye Kifo Chake Kimezishinda Nguvu za Uovu, na Kulipia Adhabu ya Dhambi.
A. Yesu Kristo kama Mwanakondoo wa Pasaka wa Agano.
1. Kama vile mwana-kondoo asiye na waa alivyokuwa ishara ya rehema ya agano la Mungu, vivyo hivyo Yesu sasa amekuwa Mwana-Kondoo wa Pasaka wa agano jipya, 1 Kor. 5:7-8.
2. Katika Yesu wa Nazareti, Pasaka ya Mungu, utimilifu wa adhabu ya Mungu juu ya dhambi na msamaha kwa watu wake umekamilika.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker