Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 3 | MUNGU MWANA : YE SU, MAS I H I NA BWANA WA WOT E – AL I KUFA / 223
Mungu Mwana Yesu, Masihi na Bwana wa Wote – Alikufa
S OMO L A 3
Ukurasa wa 121 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuelezea, kwa kutumia Maandiko na mifano halisi, umuhimu wa kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo, yaani, kushuka kwake kutoka katika uungu na utukufu mbinguni kuja duniani na kufa kwa niaba yetu. • Kuonyesha na kutaja mambo muhiumu kuhusiana na kunyenyekezwa kwa Yesu kupitia kuvaa mwili na maisha na huduma yake. • Kuelezea, kwa kutumia Maandiko na sababu zilizo wazi, jinsi kunyenyekezwa huku kwa Yesu kunavyodhihirishwa hasa katika kifo chake. • Kupanua ufahamu kuhusiana na baadhi ya dhana muhimu za kihistoria kuhusu kifo cha Yesu na jinsi kweli hizi zinatuwezesha kuelewa ni kwa kiwango gani kifo cha Bwana wetu kilikuwa baraka kwa wanadamu. • Dhana hizi ni pamoja na mtazamo wa kifo chake kama fidia kwa ajili yetu, kama upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, kama dhabihu mbadala badala yetu, kama ushindi dhidi ya shetani na kifo chenyewe, na kama upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. • Kueleza jinsi Kanuni ya Imani ya Nikea inavyokiri wazi wazi kwamba Bwana wetu Yesu Kristo alikufa na kuzikwa, na jinsi tendo hili lilivyokuwa kilele cha kunyenyekezwa kwa Bwana wetu duniani kunakoanzia na kushuka kwake kutoka mbinguni, akiuacha utukufu wake wa kimbingu aliokuwa nao hapo awali. UovuWetu Sote Isaya 53:1-12 - Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? 2 Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. 3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na
Malengo ya Somo
3
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Ibada Ukurasa wa 122 2
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker