Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
MUHTASAR I / 25
Kazi ya Huduma Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo (Waebrania 4:12). Mtume Yakobo anaweka msisitizo zaidi juu ya kuwa watendaji wa Neno la Mungu, sio wasikiaji tu, tukijidanganya wenyewe. Tunahimizwa kulifanyia kazi, kulitii. Anaongeza kusema kwamba kupuuza nidhamu hii ni sawa na sisi kujitazama sura zetu za asili katika kioo na mara tunapoondoka tunasahau asili yetu (sis ni nani) na tulichokusudiwa kuwa. Katika kila hali, mtendaji wa Neno la Mungu atabarikiwa katika kila atendalo (Yakobo 1:22-25). Shauku yetu ya dhati ni kwamba uweze kutumia maarifa unayojifunza kwa vitendo, ukiihusianisha elimu hii na masuala na mahitaji halisi katika maisha yako binafsi, na huduma yako ndani ya kanisa lako na kupitia kanisa lako. Kwa hivyo, kama sehemu mojawapo muhimu kwa ajili ya kukamilisha Mtaala wa Cornerstone utatakiwa kubuni namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo kwa ajili ya kila fungu la kozi hii, ambapo utaweza kuwashirikisha wengine sehemu ya maarifa ambayo umejifunza. Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia kutimiza takwa hili la kujifunza kwako. Unaweza kuchagua kuwa na muda wa kujifunza na mtu binafsi, kutumia madarasa ya Shule ya Jumapili, vikundi vya vijana au watu wazima, au hata kwa kupata nafasi ya kuhudumu mahali fulani. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unajadili na hadhira baadhi ya maarifa uliyojifunza kutoka darasani. (Bila shaka, unaweza kuchagua kuwashirikisha baadhi ya maarifa kutoka katika kazi yako ya Kieksejesia ya moduli hii). Uwe huru na tayari kubadilika na kuendana na mazingira yoyote unapofanya kazi yako. Ifanye iwe yenye ubunifu na inayoruhusu kusikiliza mitazamo tofauti kwa nia ya kujifunza. Fanya uchaguzi mapema kabisa kuhusu aina ya muktadha ambao unatamani kutumia kushirikisha watu wengine maarifa haya na kisha mshirikishe Mkufunzi wako juu ya maamuzi hayo. Panga hayo yote mapema na epuka kusubiri dakika za mwisho kuamua na kutekeleza kile unachotaka katika kazi yako. Baada ya kutekeleza kazi yako, andika kwa ufupi (ukurasa mmoja) tathmini ya kazi yako na umkabidhi mkufunzi wako. Mfano wa muhtasari wa Kazi ya Huduma ni kama ifuatavyo: 1. Jina lako 2. Eneo ulilolitumia na hadhira uliyowashirikisha.
Dhumuni
Mpangilio na Muhtasari
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker