Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | MUNGU ROHO MTAKAT I FU : NAF S I YA ROHO MTAKAT I FU / 253
hai kwenye safina. Wanapongojea maji yapungue, wanatuma njiwa ili waone kama anaweza kupata mahala penye nchi kavu. Hapo awali, kama vile Roho Mtakatifu wakati wa uumbaji, njiwa “anaruka juu ya maji” lakini hawezi kupata mahali pa kutua, na kwa sababu hiyo anarudi kwenye safina. Anatumwa mara ya pili na safari hii anarudi na jani la mzeituni linaloashiria kwamba kiwango cha maji kimepungua. Mara ya tatu anapotumwa hakurudi tena na hivyo Nuhu anajua kuwa nchi kavu imeonekana na ni salama kutoka kwenye safina na kuanza maisha tena duniani. Katika hadithi ya Nuhu, njiwa anakuwa ishara ya uumbaji mpya na matumaini mapya kwa dunia. (1) Mungu anapomtuma Yesu duniani yeye pia anaingia ndani ya maji, si ya gharika, bali ya mto Yordani katika ubatizo, Luka 3:22. (2) Tukio hilo ni muhimu sana kiasi kwamba limeandikwa katika vitabu vyote vinne vya Injili. Kuonekana kwa Roho Mtakatifu kama hua kunawakumbusha hadhira ya Kiyahudi wanaomwona Yesu akibatizwa kwamba, kama Nuhu, mtu huyu ni mpendwa wa Mungu na njia ya tumaini jipya na uumbaji mpya.
Ibid . uk. 79.
3. Majina na vyeo vya Roho Mtakatifu katika Biblia vinamfunua yeye kama Mpaji wa Uzima.
4
a. Anaitwa Roho wa Kweli (Yoh. 14:16-17; 15:26; 16:13). Yeye ndiye anayetufundisha maneno ya uzima.
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
b. Anaitwa Roho wa Utakatifu (Rum. 1:4). Yeye ndiye anayetuwezesha kushinda dhambi na kifo.
c. Anaitwa Roho wa Neema (Ebr. 10:29). Yeye ndiye anayeleta bure maisha mapya kwa wale ambao wasingeweza kuyapata kupitia juhudi zao wenyewe.
d. Anaitwa “Roho wa Uzima” (Rum. 8:2). Ana huduma ya kuleta uzima na ndiye chanzo cha ufufuo.
Ibid . uk. 105, 123, 127, 131, 191.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker