Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

32 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Moja ya sababu kwa nini nadhani mada hii haitambuliwi ni unyanyapaa ambao mara nyingi unaelekezwa kwa wale walio katika hali ya umaskini. Unyanyapaa huu ni imani ya kawaida (lakini si ya kibiblia) kwamba wale walio katika umaskini wanastahili kuwa huko. Sote tumeathiriwa na dhana kali ya maadili ya kazi ya waprotestanti. Hii ni imani kwamba ikiwa tutakuwa tumeandaliwa vizuri, ikiwa tutakuwa makini, na waangalifu vya kutosha katika matumizi yetu ya fedha umaskini hautatupata. Lakini hiyo si picha ambayo Biblia inatoa. Bila shaka, mojawapo ya sababu za umaskini ni maamuzi yasiyo ya hekima kimaadili. Lakini sio sababu pekee. Kwa mfano, Luka 16:19 31 inaonyesha kwamba mtu anaweza kuwa maskini kwa sababu ya kupuuzwa. Si vigumu kupata mifano ambapo wananchi wanafanya kazi kwa bidii, lakini watu wananyonywa na viongozi mafisadi na wala rushwa wa viwanda, taasisi na/au serikali. Miongoni mwa sababu nyingine za umaskini tunazopata katika Maandiko ni hali ya hewa, magonjwa, uzee, kupoteza mwenzi wa maisha bila kutarajia – orodha ni ndefu. Sisi sote tumeathiriwa na anguko linaloelezewa katika Mwanzo 3, na umaskini ni mojawapo ya matokeo ya anguko hilo. Hatua ya kwanza katika kuwawezesha watu waishio katika umaskini ni kutambua kwamba Biblia inazungumzia umaskini kama hali, si utambulisho. Kuangalia umaskini kwa njia hii ni muhimu kwa sababu ni msingi wa kazi ya kiukombozi dhidi ya umaskini. Tunaweza kufanya kazi katikati ya watu washio katika umaskini kwa namna isiyo hatarishi kwa sababu Ufalme wa Mungu uko hapa. Acha muhtasari huu mfupi ukuingize katika utafiti wa kina, huku ukifanya upya mawazo ambayo unaweza kuwa nayo kuhusu watu waishio katika umaskini na mitaa yao.

1

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

Tamka na/au imba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho).

Kanuni ya Imani ya Nikea

Kariri Mathayo 25:45 kwa kutumia Biblia ya kawaida (si toleo lililofafanuliwa), kisha ujisahihishe mwenyewe kwa kutumia Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko.

Kukariri Maandiko

Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, rejelea ratiba ya kozi hii ili kuona kazi zinazopaswa kufanyika kabla ya mkutano wako ujao wa darasa na ukamilishe kazi zilizo hapa chini: Soma yafuatayo: • Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini – “Utangulizi” na “Tafakari Fupi ya Kitheolojia” (uk. 11-22)

Kazi

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker