Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | KAZ I HATAR I SH I YA KUPAMBANA NA UMASK I N I / 43
Soma yafuatayo: • Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini
– “Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini wa Sumu” (uk. 23-30) • Kanisa lisilo la kawaida: Mabadiliko ya Jamii kwa Manufaa ya Wote – Sura ya 2: Yesu Angefanya Nini? Umaskini Ni Hali, Sio Utambulisho – Sura ya 7: Mitaa Inavyoharibiwa: Kuelewa Nguvu za Uharibifu Zitendazo Kazi Andika muhtasari wa kila usomaji wa kitabu kwa maneno yasiyozidi aya moja au mbili kwa kila muhtasari. Katika muhtasari huu, tafadhali toa uelewa wako bora zaidi wa kile unachofikiri kilikuwa jambo kuu katika usomaji. Usijali sana juu ya kutoa maelezo; andika tu kile ambacho unaona kuwa jambo kuu linalozungumziwa katika sura hiyo ya kitabu. Tumia Fomu ya Ripoti ya Usomaji. Wasilisha Fomu uliyojaza kwa ajili ya kila kitabu (ikiwa unasoma kozi hii kwa kutumia World Impact U, tumia upau wa kijani wa “Wasilisha Kazi” juu ya ukurasa wowote katika kozi yako ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini katika WIU). Ongoza Mjadala juu ya Mfano Halisi: Baadhi ya marafiki wanakuomba utembelee ghala la Kikristo la kugawa chakula kwa wahitaji, ambapo wanafanya kazi kwa kujitolea. Kama mtu wanayemwamini, wanataka uangalie na utoe maoni yako juu ya utendaji wa ghala hiyo. Jambo la kwanza unaloona unapotembea ni baadhi ya watu walio vifua wazi wakicheza kamari, kuvuta sigara na kunywa pombe karibu na mlango. Unapoingia ndani, unashangazwa na jinsi ndani palivyo giza na pachafu. Mambo yanaonekana yamekaa shaghalabaghala na huwezi kujua ni kwa namna gani watu wanavyopokea mahitaji yao. Watu wanachoka kusubiri. Kisha mhubiri kijana anakuja katika eneo la kungojea na kutoa mahubiri. Anapomaliza, kila mtu anainua mkono wake kumpokea Kristo. Baada ya kama saa moja hivi, mtu wa kwanza anaenda mbele kuchukua mfuko wa vyakula, jambo hilo linageuka kuwa mzozo mkubwa kati ya mtoa huduma na mteja juu ya uchaguzi wa chakula. Mtoa huduma anamwambia kwamba alichokipata ndicho kilichotolewa, na anapaswa kufurahiya. Baadaye, unatoka kwenda kula chakula cha mchana na marafiki zako ili kujadili uchunguzi wako. Unaweza kuwaambia nini?
2
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
KUJENGA DARALA
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker