Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
MUHTASAR I / 9
Kuhusu Wakufunzi
Wakati ambapo watu katika jamii ambazo hazina rasilimali za kutosha wanafadhaishwa na hali ngumu za maisha, kanisa la mahali pamoja linaweza kuwa mwanga wa matumaini. Alvin Sanders alijifunza hili kutokana na uzoefu wa maisha yake binafsi. Wakati akihudumu kama kiongozi wa mjini katika kitongoji cha pili kwa vurugu nchini, msiba ulitokea. Ufyatulianaji risasi wa polisi ulioambatana na kauli za ubaguzi wa rangi ulitikisa mtaa huo. Kama jawabu, Alvin alianzisha kanisa bunifu ambalo linaendelea kutunza, kuhudumia, na kutia moyo watu kutoka katika matabaka yote ya maisha. Kupitia uzoefu huu aligundua utume wake binafsi: kumfuata Mungu kwa bidii, kupenda familia yake, na kuwekeza kwa wale wanaowekeza kwenye maisha ya watu maskini. Alvin ni mtu wa kanisa kutoka moyoni. Baada ya upandaji kanisa na uchungaji, alihudumu kama kiongozi wa dhehebu katika Kanisa la Evangelical Free Church of America (EFCA) kwa miaka saba. Akiwa huko aliongoza EFCA All People Initiative . Chini ya uongozi wake EFCA ilikua kutoka 13% ya makutaniko yao yaliyoainishwa kama ya mijini, ya kikabila, au yenye makabila mchanganyiko hadi 22%. Pia aliandika kitabu chake kiitwacho Bridging the Diversity Gap . Kutokana na mapenzi yake kwa viongozi wa kanisa, kuhamia kwake World Impact mwaka 2015 lilikuwa jambo la kawaida ambalo kila aliyemfahamu angelitarajia. Historia yake kitaaluma ni pamoja na Shahada ya Sayansi katika Masomo ya Biblia kutoka Chuo Kikuu cha Kikristo cha Cincinnati na Shahada ya Uzamili katika Dini na Huduma ya Mjini kutoka Chuo cha Trinity Evangelical Divinity . Alihitimu ngazi ya Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) katika Uongozi wa Kielimu kutoka Chuo Kikuu cha Miami. Tangu 2004 amehudumu kama profesa msaidizi katika seminari mbalimbali nchini kote. Katika wakati wake wa kupumzika, Alvin ni msomaji mwenye bidii na anapenda kufuatilia timu za michezo anazozipenda. Anamshukuru mke wake wa pekee sana, Caroline, ambaye amedumu katika huduma ya ushauri katika mji wao wa Cincinnati. Wamebarikiwa kuwa na binti wawili wazuri ajabu. Mnamo Novemba 2017, Alvin aliteuliwa kuwa Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa World Impact.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker