Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
This is the Swahili edition of the Cornerstone Mentor Guide.
Inajumuisha Kazi yaKiukombozi dhidi yaUmaskini cha Dk. Alvin Sanders
Mtaala wa Cornerstone
The Urban
Mini s t r y I ns t i tute huduma ya Wor ld Impac t , I nc .
Toleo Rasmi la Ithibati
Alvin Sanders | Mch. Dk. Don L. Davis Mch. Terry G. Cornett | Mch. Ryan Carter
Mwongozo wa Mkufunzi
SWAHILI
Mtaala wa Cornerstone Toleo Rasmi la Ithibati Mwongozo wa Mkufunzi
Mtaala wa Cornerstone, Toleo Rasmi la Ithibati – Mwongo wa Mkufunzi
© 2023. The Urban Ministry Institute. All Rights Reserved. © 2024 Toleo la Kiswahili, kimetafsiriwa na Mch. Samuel Gripper na Mch. Eresh Tchakubuta.
Tunatambua na kuheshimu utumishi uliotukuka wa Mtume K. E. Kisart kwa kujitolea kwake bila kukatishwa tamaa kuwafundisha viongozi katika Injili.
Haki Zote Zimehifadhiwa. Kunakili, usambazaji, na/au uuzaji wa nyenzo hizi, au uhamishaji wowote ambao haujaidhinishwa, isipokuwa kama inavyoweza kuruhusiwa waziwazi na Sheria ya Hakimiliki ya 1976 au kwa maandishi kutoka kwa mchapishaji ni marufuku. Maombi ya idhini yanapaswa kuelekezwa kwa maandishi kwa:
The Urban Ministry Institute 3701 East 13th Street North Suite 100 Wichita, KS 67208
ISBN: 978-1-62932-070-0
Imechapishwa na TUMI Press Kitengo cha World Impact, Inc.
The Urban Ministry Institute ni huduma ya World Impact, Inc.
Nukuu zote za Maandiko, isipokuwa kama imeonyeshwa vinginevyo, zimechukuliwa kutoka katika SWAHILI BIBLE UV050(MCR) series® Haki Miliki © 1997, iliyochapishwa na The Bible Society of Tanzania. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote za kimataifa zimehifadhiwa.
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Mtaala wa Cornerstone Toleo Rasmi la Ithibati
T h e U r b a n
M i n i s t r y I n s t i t u t e h u d u m a y a W o r l d I m p a c t , I n c .
Alvin Sanders | Mch. Dkt. Don L. Davis Mch. Terry G. Cornett | Mch. Ryan Carter
Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
~ Waefeso 2:19-22
TUMI Press 3701 East 13th Street North Suite 100 Wichita, Kansas 67208
Yaliyomo
9 Utangulizi wa Mtaala wa Cornerstone, Toleo Rasmi la Ithibati
Sehemu ya I: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini
13 Kufundisha Sehemu ya I: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini 17 Cornerstone Sehemu ya I: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini – Ratiba ya Kozi 21 Cornerstone Sehemu ya I: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini – Muhtasari wa Kozi 25 Somo la 1 Tafakari Fupi ya Kitheolojia 31 Somo la 2 Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini 37 Somo la 3 Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini 45 Somo la 4 Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini
Sehemu ya II na ya III: Mtaala wa Cornerstone
55
Kufundisha Sehemu ya II na ya III: Mtaala wa Cornerstone
Sehemu ya II: Biblia na Theolojia
Fungu la Kwanza: Masomo ya Biblia
Somo la 1 Uongofu na Wito: Neno Liumbalo Somo la 2 Ufasiri wa Biblia: Mbinu ya Hatua Tatu
69
75
Somo la 3 Ushahidi wa Agano la Kale Kuhusu Kristo na Ufalme wake: Kutolewa kwa Ahadi Somo la 4 Ushahidi wa Agano la Kale Kuhusu Kristo na Ufalme wake: Kupingwa kwa Masihi
81
93
Fungu la Pili: Theolojia na Maadili
Somo la 1 Ufalme wa Mungu: Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu Somo la 2 Mungu Baba: Mungu wa Utatu – Ukuu wa Mungu Somo la 3 Mungu Mwana: Yesu, Masihi na Bwana wa Wote – Alikufa Somo la 4 Mungu Roho Mtakatifu: Nafsi ya Roho Mtakatifu
105
113
121
127
Sehemu ya III: Huduma na Utume
Fungu la Kwanza: Huduma ya Kikristo
Somo la 1 Theolojia ya Kanisa: Kanisa katika Ibada
141
Somo la 2 Misingi ya Uongozi wa Kikristo: Kiongozi wa Kikristo kama Mchungaji – Poimenes Somo la 3 Kutekeleza Uongozi wa Kikristo: Uongozi Bora wa Ibada
151
155
Somo la 4 Huduma ya Kukamilisha Watakatifu: Huduma ya Mahubiri – Kerygma
163
Fungu la Pili: Utume katika Miji
Somo la 1 Misingi ya Utume wa Kikristo: Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo
171
Somo la 2 Uinjilisti na Vita ya Kiroho: Kufungwa kwa Mtu Mwenye Nguvu Somo la 3 Mkazo kuhusu Uzazi: Ukuaji wa Kanisa – Kuongezeka katika Idadi na Ubora
177
183
Somo la 4 Kutenda Haki na Kupenda Rehema: Haki na Ishuke – Maono na Theolojia ya Ufalme
191
U T A N G U L I Z I / 9
Utangulizi wa Mtaala wa Cornerstone, Toleo Rasmi la Ithibati
Karibu kwenye Mtaala wa Cornerstone , fursa yako mpya ya kuandaliwa kwa ajili ya huduma bora katika Kanisa!
Changamoto: Uhitaji Mkubwa, Hakuna Muda , Fedha Chache Ukweli mchungu anaoukabili mtu yeyote anayewaandaa wachungaji na wahudumu walei wanaotumika katika jamii zilizo hatarini, ni ule wa uhaba. Pesa na muda ni adimu na finyu sana kwa viongozi hawa hodari wanaomtumikia Mungu katika jamii maskini kuweza kujihusisha katika masomo ya muda marefu katika mfumo ulio rasmi. Wanafanya kazi isiyo ya kawaida huku mara nyingi wakiwa katika ajira za kudumu na wakipambania huduma inayokua. Maelfu ya wafanyakazi wa Kikristo walioko mijini ambao wangenufaika na mitaala yetu bora na yenye kina cha kiwango cha seminari kama Mtaala wa Capstone , hawana ama muda au fedha za kuikamilisha. (Muda wa wastani kwa wanafunzi wanaosoma na kufanya kazi kumaliza moduli kumi na sita za Capstone ni miaka mitatu hadi minne). Kukabiliana na Changamoto: Mtaala wa Cornerstone Ili kukabiliana na hitaji hili kuu, tumebuni mtaala huu wa kipekee, Mtaala wa Cornerstone . Ukiwa umechaguliwa kutoka kwenye masomo maalum ya kimkakati ya Capstone , na kuongezewa moduli ya “Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini” ya Dkt. Alvin Sanders, tuliunda kozi hii kwa ajili ya wale ambao hawana uhakika wa kuwa na muda au fedha za kukamilisha mtaala wetu mkubwa zaidi wa Capstone . Muda wa kukamilisha sehemu tatu za Cornerstone ni sawa na moduli tatu pekee za Capstone . Tuliunda nyenzo hii ili kuwasaidia wanafunzi hawa kuzifikia nyenzo muhimu pasipo kudhabihu ubora au fursa za huduma zao. Cornerstone itapunguza kwa kiasi kikubwa muda na gharama zinazohitajika kwa ajili ya shule ya kawaida ya Biblia au masomo ya seminari au hata Mtaala wa Capstone , pasipo kupoteza uaminifu wetu ama kwa Kweli ya kibiblia au kwa mafunzo ya huduma kwa vitendo.
1 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Kuandaliwa Kupanda, Kuchunga, na Kutumikia Kanisa! Nyenzo za mtaala wa Cornerstone zinajumuisha kozi ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini na nyenzo zilizotolewa moja kwa moja kutoka kwenye moduli za Capstone , zikitoa kweli zake muhimu kutoka kwenye maeneo manne ya idara zake (Masomo ya Biblia, Theolojia na Maadili, Huduma ya Kikristo, na Utume katika Miji). Tumeweka pamoja masomo ya Cornerstone ili kukupatia utaratibu thabiti wa mafunzo kwa wakati unaofaa na gharama nafuu. Mafunzo yetu yatakupatia ithibati, yataboresha ujuzi wako wa Maandiko, na kukuwezesha kuhudumu vyema kama mchungaji, kiongozi mlei, au Mkristo mtenda kazi mahali unapoishi na kufanya kazi. Mungu amekuita na kukupa karama, na tunatumaini kukuona ukitimiza wito wake kwenye maisha yako, ili upate kumletea heshima Mwokozi wetu katika kila jambo ulifanyalo. Kwa hiyo, ninakupa changamoto ya kutimiza huduma ya Bwana kwa ajili yako, yote katika nia ile ile kama ya Paulo anapomuasa Timotheo, “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” (2 Tim. 2:15). Fahamu kwamba ukijitoa kwa Mungu kama mtu aliyekubaliwa, utatimiza wito wake na kuzaa matunda ya kiroho ambayo yanamtukuza Kristo na kumpendeza Mungu. Mungu akubariki sana katika masomo yako, ufuasi wako, na huduma yako! Kwa ujasiri mkubwa katika Neno la Mungu la milele lenye kuponya
na kubadilisha, Dkt. Don Davis Wichita, Kansas Februari 1, 2023
Sehemu ya I
Kazi ya Ukombozi dhidi ya Umaskini
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 3
Kufundisha Sehemu ya I: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini
Kipindi chako cha kwanza kitakuwa semina elekezi. Hii ni sehemu ya mahitaji ya darasa kwa wanafunzi, na mahudhurio ni ya lazima. Katika kipindi hiki utatoa matarajio ya darasa, sera ya upangaji madaraja, muda wa kukamilisha kazi, na namna mitihani itakavyosimamiwa, n.k. Ikiwa hii ni kozi ya mtandaoni kwa kutumia World Impact U (WIU), pia utawapa wanafunzi maelekezo kuhusu WIU, jinsi ya kujibu maswali ya jukwaa hili, na jinsi ya kuwasilisha kazi. Pia zipo video mbili za kulionyesha darasa wakati wa kipindi hiki: • Fursa ya Kujifunza Ukombozi dhidi ya Umaskini, Dkt. Don Davis • Siri Ndogo Isiyopendeza ya Kazi ya Kupambana na Umaskini, Dkt. Alvin Sanders Yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo ya mambo ya kufanya katika kipindi hiki cha kwanza: Karibu 1. Fungua kwa maombi. 2. Toa jina lako kamili na anwani ya Barua pepe ili wanafunzi wajue jinsi ya kukufikia. 3. Wakumbushe wanafunzi kwamba walipaswa wawe na nakala za vitabu vya kiada tayari: • Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini, Dkt. Alvin Sanders • Kanisa Lisilo la Kawaida: Badiliko la Jamii kwa Manufaa ya Wote, Dkt. Alvin Sanders 4. Ruhusu wanafunzi wajitambulishe, huduma zao, na kile wanachotarajia kupata kutoka darasani. Utangulizi Video: Tazama video ya Fursa ya Kujifunza Ukombozi dhidi ya Umaskini, ya Dkt. Don Davis, kuhusu namna tunavyohitaji mtazamo thabiti, wa kibiblia, na wenye nguvu kuhusu maana ya kuendesha huduma ya kuboresha hali za maisha katika jamii maskini. Tambulisha Dhana ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini 1. Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini ilitengenezwa kutokana na kupitia “Muundo wa Ukombozi” na kuutumia katika World Impact. Muundo wa Ukombozi unasema kwamba kuna namna tatu
1 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
unazofanya kazi ulimwenguni pote: Kwa unyonyaji, kwa maadili, na kiukombozi. Kwa hiyo unachukua muundo huu na kuuweka juu kwenye taasisi yako isiyo ya faida na kazi unayoifanya. Kwa kuwa World Impact hufanya Kazi ya Kupambana na Umaskini, ikifanya kazi na watu katika jamii maskini, tuna Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini (KKU). 2. Ukristo ulizaliwa katikati ya watu waliokuwa wakiishi katika hali za umaskini, na hadi leo idadi kubwa ya watu wanaojiunga na Ukristo wanaishi katika hali ya umaskini. Kwa hiyo ni muhimu sana kuelewa mtazamo wa Kristo kuhusu umaskini ulivyokuwa na jinsi alivyotarajia sisi kuhudumu kwa msingi wa mtazamo huo. 3. Sasa kwa kuwa tuna KKU (Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini), World Impact imegundua kwamba hii sio tu kwamba itasaidia watu ambao tayari tunahudumu nao, lakini pia inafungua milango kwa hadhira mpya kabisa ya watu ambao hawangeweza kutusikiliza au hata kuona sababu ya kutusikiliza hapo kabla. 4. Hapa kuna baadhi ya mifano: • Kuna kundi la watoa huduma za nishati katika eneo la Atlanta, Georgia, ambapo tulikuwa na uhusiano nao hapo awali. Dkt. Sanders alipo tambulisha KKU kwa hadhira hii isiyo ya kidini waliipenda kiasi kwamba wakurugenzi wakuu kadhaa wa Makampuni ya Huduma za Umma wamewasiliana nasi kujaribu kuona namna wanavyoweza kushirikiana na World Impact. • Dkt. Sanders alifanya mafunzo ya majaribio ya KKU kwa makanisa mawili makubwa zaidi huko Louisville, Kentucky, na waliipenda kwa sababu waligundua wamekuwa wakifanya kazi nyingi za kupambana na umaskini kwa namna ambayo ni hatarishi. • Mchungaji wa umisheni wa kanisa kubwa lenye matawi 5. Hii ni kwa ajili ya mtu yeyote ambaye anapenda kufuata kielelezo cha Yesu Kristo na kufanya kazi na watu walio katika mazingira ya umaskini, haijalishi kwamba uko katika umaskini sasa au haujawahi kuwa katika umaskini. Jambo pekee unalohitaji ni shauku ya kufanya kazi katika jamii zenye hali kadhaa alisema kuwa KKU ndiyo namna anavyoweza kushirikisha watu moyo wa utumishi katika kanisa lake.
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 5
ya umaskini kama Kristo alivyofanya. Yawezekana ni mfadhili, mchungaji mwenye kanisa katikati ya jiji, mfanyakazi wa kujitolea kwenye ghala ya chakula au kituo cha kutolea misaada ya kibinadamu, mwalimu, n.k. 6. Mtazamo tunaoujenga kwa ajili ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini ni kuweza kutazama na kutenda kama Yesu alivyotufanyia sisi katika urejesho wa ajabu kupitia dhabihu. Kwa watu tunaofanya nao kazi, tunataka kuwa na uwezo wa kutoa njia za fursa, na kuwasaidia kuelewa kwamba wanaweza kutumiwa na Mungu na kuishi katika hali na mazingira walimojikuta. Baadhi wanaweza kuchagua kujaribu kuboresha maisha yao na wengine wasiweze kabisa kutoka katika hali waliyomo. Jambo ambalo hatuwezi kusahau ni kwamba pasipo kujali kwamba wanamiliki mali au la, Mungu anawapenda, na Mungu yuko pamoja nao ili kuwatumia. 7. Lengo la kozi hii ni kuwa na theolojia ya vitendo ya jinsi ya kufanya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini yenye mafanikio. Maelezo ya Kozi na Silabasi Pitia Maelezo ya Kozi, Malengo, na Silabasi (vinavyopatikana kwenye kurasa nambari 15-18 katika Kitabu cha Mwanafunzi). Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu kuhusu kila somo: • Somo la 1: Tafakari Fupi ya Kitheolojia Somo hili halikusudiwi kutoa ufahamu wa kila kitu ambacho Biblia inasema kuhusu watu walio katika umaskini na hali ya umaskini. Badala yake, kama tukiulizwa ni Kwa nini tunafanya haya, utakuwa na jibu la kitheolojia kwa vitendo. • Somo la 2: Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini Katika somo hili, tunazungumzia tatizo la Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini, ambayo inatokana moja kwa moja na mtazamo wa kinyonyaji. Tutajadili jinsi hii inavyoweza kutokea pasipo kujitambua, na kwamba kuwa na nia nzuri pekee haitoshi. Kila mtu lazima ahoji mienendo na mtazamo wake wa kimaadili kwa habari ya Kwa nini anafanya Kazi ya Kupambana na Umaskini na kujiuliza, “Je, ninafanya katika misingi ya kibiblia?”
1 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
• Somo la 3: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini Katika somo hili tunafafanua hasa Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini ni nini, inahusu nini, na jinsi inavyotofautiana na Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini. • Somo la 4: Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini Somo letu la mwisho linaonyesha jinsi tunavyoweza kutumia nidhamu nane za kiroho ili kuimarisha mwenendo wetu kama waamini katika Yesu Kristo na kuzuia uchovu kinaifu na msongo. Jukwaa na Fomu Mbalimbali Hakikisha wanafunzi wana uwezo wa kulifikia jukwaa na fomu watakazohitaji ili kukamilisha kazi zao. (Fomu hizi zinaweza kupatikana mtandaoni kwenye Dashibodi ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini ya WIU). • Fomu ya Tathmini ya Kumbukumbu ya Maandiko • Ratiba ya Darasa yenye Kazi na Tarehe za Kukamilisha Pitia pamoja na wanafunzi fomu, matumizi ya jukwaa, na mahitaji ya kozi. Utangulizi wa Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini Kama hatua ya mwisho katika kipindi hiki cha darasa, tazama Siri Ndogo Isiyopendeza ya Kazi ya Kupambana na Umaskini ambayo inatoa muhtasari wa mbinu tatu kuu za kuwahudumia watu binafsi na familia katika jamii zilizo hatarini, k.m mbinu ya Kinyonyaji, mbinu ya Kimaadili, na mbinu ya Kiukombozi, na kuweka msingi kwa ajili ya mafunzo yako yote. Kuelewa kanuni na utendaji wa Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini ni muhimu kwa wale wote wanaotafuta haki na amani katika jamii za umaskini. Wakumbushe wanafunzi juu ya kukutana kwao katika kipindi kijacho na kazi yoyote inayohitaji kukamilishwa kabla ya kukutana kwenye kipindi cha somo la 1. • Orodha ya Ukaguzi wa Kazi • Fomu ya Ripoti ya Usomaji
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 7
Cornerstone Sehemu ya I: Kazi ya Kiukombozi dhidi yaUmaskini – Ratiba ya Kozi Msimu, Mwaka (mf. Vuli 2021) Jina la Mkufunzi Tarehe ya Darasa (mf. Nov. 17 - Des. 22, 2021)
Taarifa za Kipindi
Somo na Kazi
Kipindi cha Semina Elekezi
Kipindi cha Semina Elekezi: Utangulizi wa Kozi Shiriki katika Mkutano wa ana kwa ana kwa ajili ya Utangulizi wa Kozi.
Mkutano wa ana kwa ana Tarehe Muda Kipindi cha 1 Mkutano wa ana kwa ana Tarehe Muda
Somo la 1, Tafakari Fupi ya Kitheolojia Wanafunzi wanapaswa kukamilisha yafuatayo kabla ya mkutano huu: 1. Kamilisha somo la 1 la Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. 2. Pitia maswali mwishoni mwa sehemu ya yaliyomo ya somo la 1. Jiandae kujadili majibu yako katika mkutano wetu wa ana kwa ana wa Somo la 1. 3. Kamilisha kazi kwenye sehemu ya Kazi za Kukamilisha kwa ajili ya somo la 1 kabla ya mkutano wa ana kwa ana wa somo la kwanza. Kazi hizo ni kama zifuatazo: a. Soma yafuatayo kutoka katika Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini: • Utangulizi (uk.11-15) • Tafakari fupi ya Kitheolojia (uk. 17-22) b. Soma yafuatayo kutoka katika Kanisa Lisilo la Kawaida: • Dibaji na Efrem Smith • Sura ya 3: Yesu Alifanya, Sio Yesu Angefanya: Yesu na Hali ya Umaskini • Sura ya 6: Imani na Matendo: Kuondoa Mvutano kati ya Uinjilisti na Haki c. Kamilisha muhtasari wako wa usomaji kwenye Fomu ya Ripoti ya Usomaji kwa kila usomaji ulioorodheshwa hapo juu. d. Kariri Mathayo 25:45 na ujisahihishe kwa kutumia Fomu ya Tathmini ya Kumbukumbu ya Maandiko. Baada ya mkutano wa ana kwa ana: Fanya Jaribio la Somo la 1.
1 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Taarifa za Kipindi
Somo na Kazi
Somo la 2, Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini Wanafunzi wanapaswa kukamilisha yafuatayo kabla mkutano huu: 1. Kamilisha somo la 2: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini katika Kitabu cha Mwanafunzi. 2. Pitia maswali mwishoni mwa sehemu ya yaliyomo ya somo la 2. Jiandae kujadili majibu yako katika mkutano wetu wa ana kwa ana wa Somo la 2. 3. Kamilisha kazi kwenye sehemu ya Kazi za Kukamilisha kwa ajili ya somo la 2 kabla ya mkutano wetu wa ana kwa ana wa somo la 2. Kazi hizo ni zifuatazo: a. Soma yafuatayo katika somo la Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini: • Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini (uk. 23-30). b. Soma yafuatayo katika somo la Kanisa Lisilo la Kawaida : • Sura ya 2: Yesu Angefanyaje? Umaskini ni Hali, Sio Utambulisho • Sura ya 7: Matatizo katika Mitaa: Kuelewa Nguvu Zilizopo c. Kamilisha muhtasari wako wa usomaji katika Fomu ya Ripoti ya Usomaji kwa kila usomaji ulioorodheshwa hapo juu. d. Kariri Luka 4:18-19 na ujisahihishe kwa kutumia Fomu ya Tathmini ya Kumbukumbu ya Maandiko. Baada ya mkutano wa ana kwa ana: Fanya Jaribio la Somo la 2.
Kipindi cha 2
Mkutano wa ana kwa ana Tarehe Muda
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 9
Taarifa za Kipindi
Somo na Kazi
Somo la 3, Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini Wanafunzi wanapaswa kukamilisha yafuatayo kabla ya mkutano huu: 1. Wanafunzi wanapaswa kukamilisha yafuatayo kabla ya mkutano huu: 2. Pitia maswali mwishoni mwa sehemu ya yaliyomo ya somo la 3. Jiandae kujadili majibu yako katika mkutano wetu wa ana kwa ana wa Somo la 3. 3. Kamilisha kazi katika sehemu ya Kazi za Kukamilisha kwa ajili ya somo la 3 kabla ya mkutano wetu wa ana kwa ana wa somo la 3. Kazi hizo ni zifuatazo: a. Soma yafuatayo katika Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini: • Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini (uk. 31-36) b. Soma yafuatayo katika Kanisa Lisilo la Kawaida: • Sura ya 4: Watu wa Mungu: Mpango wa Mungu kwa Ulimwengu Uliovunjika • Sura ya 8: Kupigania Jamii: Kuwawezesha Viongozi na Wafanyakazi wa Ngazi ya Chini. • Sura ya 10: Ufalme U Ndani Yetu c. Kamilisha muhtasari wako wa usomaji katika Fomu ya Ripoti ya Usomaji kwa kila usomaji ulioorodheshwa hapo juu. d. Kariri Yohana 1:14 na ujisahihishe kwa kutumia Fomu ya Tathmini ya Kumbukumbu ya Maandiko. Baada ya mkutano wa ana kwa ana: Fanya Jaribio la Somo la 3.
Kipindi cha 3
Mkutano wa ana kwa ana Tarehe Muda
2 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Taarifa za Kipindi
Somo na Kazi
Somo la 4, Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini Wanafunzi wanapaswa kukamilisha yafuatayo kabla ya mkutano huu: 1. Kamilisha somo la 4 la Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini kwenye Kitabu cha Mwanafunzi. 2. Pitia maswali mwishoni mwa sehemu ya yaliyomo ya somo la 4. Jiandae kujadili majibu yako katika mkutano wetu wa ana kwa ana wa Somo la 4. 3. Kamilisha kazi kwenye sehemu ya Kazi za Kukamilisha kwa ajili ya somo la 4 kabla ya mkutano wetu wa ana kwa ana wa somo la 4. Kazi hizo ni zifuatazo: a. Soma yafuatayo katika “ Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini” : • Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini (uk. 37-50) b. Soma yafuatayo katika “Kanisa Lisilo la Kawaida” : • Sura ya 1: Utetezi Hautoshi • Sura ya 5: Ushirika Wenye Afya katika Kanisa: Tabia Saba Kuelekea Ukomavu wa Kiroho • Sura ya 9: Kufuata Maono Yasiyo ya Kawaida: Mifano ya Imani, Tumaini, na Upendo katika Matendo c. Kamilisha muhtasari wako wa usomaji katika Fomu ya Ripoti ya Usomaji kwa kila usomaji ulioorodheshwa hapo juu. d. Kariri Matendo 2:42 na ujisahihishe kwa kutumia Fomu ya Tathmini ya Kumbukumbu ya Maandiko. Baada ya mkutano wa ana kwa ana: a. Fanya Mtihani wa Mwisho. b. Kamilisha Fomu ya Tathmini ya Kozi Kazi za Mwisho za Kukamilisha 1. Mtihani wa Mwisho 2. Fomu ya Tathmini ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini
Kipindi cha 4
Mkutano wa ana kwa ana Tarehe Muda
Date
Kumbuka: Pata toleo linaloweza kuhaririwa la ratiba hii hapo juu kwenye dashibodi ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini yaWorld Impact U. Hariri maelezo kwa ajili ya darasa lako na uwasambazie wanafunzi wako.
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 2 1
Cornerstone Sehemu ya I: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini Muhtasari wa Kozi
Tunathamini sana mchango wako na tuko hapa kukuhudumia! Tafadhali jibu maswali yafuatayo ili kutoa mrejesho kuhusu mafunzo uliyoyapata na utambulisho wako. Kadiri tunavyoelewa wewe ni nani na unahitaji nini, ndivyo tunavyoweza kutengeneza nyenzo na mipango yetu kwa manufaa yako.
1. Kanisa, Mtandao wa Huduma, au Shirika Taasisi iliyoasimamia kozi hii inaitwaje?
Ingawa tunapendelea fomu hii ijazwe mtandaoni, mazingira yanaweza kuzuia hili kuwezekana. Tafadhali tambaza (scan) fomu zilizojazwa na utume kwa msimamizi wa Cornerstone.
2. Je, kuna uwezekano kiasi gani wa wewe kupendekeza kozi hii kwa marafiki zako na watu wako wa karibu? Tafadhali chagua 1-5 5 = Kwa hakika ningependekeza
4 = Pengine ningependekeza 3 = Ninaweza kupendekeza 2 = Pengine nisingependekeza 1 = Nisingependekeza kabisa
Tafadhali jibu swali la 3, 4, na 5 kwa kuzingatia viwango vifuatavyo: 5 = Imezidi matarajio yangu 4 = Juu kidogo ya matarajio yangu 3 = Imekidhi matarajio yangu 2 = Chini kidogo ya matarajio yangu 1 = Haikukidhi matarajio yangu
2 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
3. Je, unaweza kukadiriaje maudhui katika kozi uliyomaliza? (Pima kwa kiwango cha 1-5) _______ Je, ungependa kutoa maoni kuhusu ukadiriaji wako wa “maudhui ya kozi”?
4. Je, unaweza kumkadiriaje mkufunzi wako (kiwango cha 1-5)? _____ Je, ungependa kutoa maoni kuhusu ukadiriaji wa mkufunzi wako?
5. Kwa ujumla, je, kozi ilikidhi matarajio yako (kiwango cha 1-5)? _____ Je, ungependa kutoa maoni kuhusu ukadiriaji wako wa “matarajio ya kozi”?
6. Je, tunawezaje kuboresha mchakato huu wa kujifunza?
7. Jina la Mkufunzi wa kozi hii: (Tafadhali USIWEKE jina lako hapa). ____________________ ____________________ Jina la Kwanza Jina la Mwisho
Barua pepe ya mkufunzi wako: _____________________________
Mkufunzi atapokea ripoti juu ya ukadiriaji pasipo mkadiriaji kujulikana. Majina yote na maelezo ya kina hayatawekwa wazi kwake.
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 2 3
Taarifa Binafsi
Hakuna taarifa yoyote kati ya hizi itakayowekwa wazi ikiwa imeambatanishwa na taarifa zako binafsi. Hii ni kwa ajili ya ukusanyaji wa data tu.
Jina la Kwanza:
Jina la Mwisho:
Barua Pepe:
Je, wewe ni mfungwa kwa sasa (tafadhali zungushia duara kimojawapo)? Ndio / Hapana
Jinsi/Jinsia (tafadhali zungushia duara kimojawapo): Me/Ke
Asili (tafadhali chagua mojawapo ya yafuatayo):
a. Mwa-Asia/Mkazi wa Kisiwa cha Pasifiki
b. Mwenye asili-mbili, Chotara wa asili zaidi ya mbili
c. Mweusi
d. Mlatino
e. Mzaliwa wa Amerika
f. Mweupe
Mwaka wa kuzaliwa (mf. 1976): _______
Asante kwa kukamilisha utafiti huu!
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 2 5
Tafakari Fupi ya Kitheolojia
S OMO L A 1
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini, Somo la 1: Tafakari Fupi ya Kitheolojia . Somo hili linatoa theolojia rahisi ya vitendo kwa ajili ya Kazi ya Kupambana na Umaskini. Kimaalum kabisa, somo hili linasisitiza mada tatu za kibiblia ambazo zinaweka msingi wa kwa nini tunafanya kile tunachofanya. Unapowaongoza wanafunzi wako kupitia mada hizi za kibiblia, hakikisha unatoa muda wa kutosha kwa Maandiko yenyewe. Wanafunzi wanapaswa kuelewa wazi kwamba Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini imejikita katika Maandiko. Wasaidie kuhusisha kanuni za uwezeshaji za Agano la Kale na msisitizo wa kweli kuhusu namna Yesu mwenyewe alivyowapa upendeleo wa pekee watu maskini na kutoa maonyo dhidi ya utajiri. Wakristo wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuuona umaskini kama matokeo ya kushindwa kibinafsi kuliko wasio Wakristo. Mtazamo huu hupelekea walio katika umaskini kuchukuliwa kama “miradi” badala ya watu wa kuwatumikia, jambo ambalo silo alilokusudia Mungu. Ni lengo la somo hili kutoa marekebisho ya kibiblia kwa mitazamo na mawazo haya. Biblia inatoa maagizo muhimu kuhusu namna tunavyopaswa kuwatendea walio maskini. Katika somo hili lote, na masomo yajayo, weka Maandiko yawe msingi kwa ajili ya wanafunzi wako. kuyatumia, huku msisitizo mkubwa ukiwekwa juu ya utetezi na utetezi pekee kuwa ndilo jibu lifaalo kwa kile kinachowasumbua watu wanaoishi katika hali ya umaskini. 2. Hatupaswi kujaribu kutenganisha mambo haya mawili: • Amini katika uinjilisti NA haki. • Amini katika dhambi ya mtu binafsi na dhambi katika mifumo ya kitaasisi. 3. Tunataka kuwa wapambanaji wa mstari wa mbele na wasambazaji wa kweli hiyo ya kitheolojia. Sisitiza umuhimu wa ufahamu wa Biblia. 1. Pamekuwa na badiliko hasi kubwa la kimtazamo na kivitendo katika uwezo wa watu kujishughulisha na Maandiko na
1 Ukurasa wa 31 Utangulizi wa Somo
1
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
2 Ukurasa wa 34 Muhtasari
2 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
4. Kukosa ufahamu wa Biblia kumefikia kiwango cha juu sana kwa waamini makanisani. Hata kwa hadithi za kawaida za kibiblia kama ya Nuhu na safina au ya Yusufu na ndugu zake, nusu ya wale walio kanisani wasingeweza kujua kuhusu haya. Usidhani kwamba watu wanajua Biblia. Ikiwa watu kwa ujumla hawaijui Biblia, basi kwa hakika hawajui inachosema kuhusu umaskini au hali ya umaskini. I. Umaskini ni Mada Inayopatikana Katika Agano la Kale na Agano Jipya Yafuatayo ni maarifa muhimu ya kuzingatia unapojadili sehemu hii na wanafunzi wako. 1. Biblia ni kitabu cha maskini wafanyao kazi. 2. Umaskini ni ukosefu wa rasilimali fedha kwa ajili ya watu kuweza kuhudumia mahitaji waliyonayo katika maisha yao. 3. Biblia inatupa sababu nyingi za ukosefu wa rasilimali hizi. • Dhambi binafsi – mfano ni mwana mpotevu. Alikuwa na pesa nyingi lakini alizimaliza zote kwa sababu ya mtazamo na tabia yake. • Dhambi ya Kijamii/Kitaasisi – watu wako katika umaskini kwa sababu tu ya jamii wanamoishi; mambo ambayo jamii hufanya ili kuweka makundi fulani ya watu katika umaskini na kuwakomboa wengine kiuchumi. 4. Sio ama/au; inaweza kuwa vyote/na. 5. Nchini Marekani, kitakwimu watu wengi katika umaskini walizaliwa humo na wengi wao hawabadili tabaka za umaskini. (KUMBUKA: Hii inaweza kuwa tofauti katika nchi yako). 6. Masikini wafanyao kazi ni mada ambayo imefumwa vema katika Biblia nzima. Lengo halikuwa juu ya jinsi watu walivyoingia katika hali hiyo, lakini ni jinsi gani tunaweza kutengeneza njia za fursa.
1
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
3 Ukurasa wa 34 Muhtasari wa Kipengele cha I
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 2 7
A. Kanuni za Uwezeshaji za Agano la Kale Wasaidie wanafunzi wako kuelewa yafuayo: 1. Agano la Kale lilijikita katika kutengeneza njia za fursa. 2. Biblia si lazima izingatie sababu. Agano la Kale lililenga katika kutengeneza njia za fursa kwa watu kuweza kustahimili hali zao au kuvuka hali zao na kuelewa kwamba Mungu ni mkuu kuliko hali wanazojikuta ndani yake. • Mfano wa hili ni kanisa ambalo lilitoa ufadhili kamili wa masomo kwa watoto wampendao Mungu walio katika umaskini, ambao walikuwa na uwezo na shauku ya kwenda chuo kikuu, lakini sio fursa. Kwa kupata shahada ya chuo kikuu, wamekuwa wanajamii wenye tija na hawako tena katika umaskini. 3. Tungeweza hata kusema kwamba muktadha wa Biblia katika ujumla wake ni wa hali ya umaskini kwa sababu karibu katika kila utamaduni, unadharauliwa ikiwa hauna rasilimali za kutosha (raia wa daraja la pili). • Katika Biblia, taifa la Israeli halikuonekana kama taifa lenye nguvu, bali kama kundi la watu wakorofi waliokuwa utumwani. Hata hivyo, Mungu alisema wao, watu wa chini, wangekuwa watu wake. Msingi mzima wa kitabu cha Kutoka ni kwamba Mungu aliwatoa Misri.
4 Ukurasa wa 34 Muhtasari wa Kipengele A
1
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
• Pia, kulikuwa na watu/mataifa mengine huko Misri, na walipoona kile Mungu wa Waisraeli alichofanya,
walikwenda pamoja na wana wa Israeli. Waliona kile Mungu alichofanya kwa taifa “lenye nguvu” la Misri na jinsi Mungu alivyomnyenyekeza mungu wa Misri.
B. Yesu Alipendelea Maskini / C. Yesu Alionya dhidi ya Utajiri Angazia yafuatayo kuhusu vipengele hivi viwili vya muhtasari: 1. Yesu na wahusika wengi wa Biblia walikuwa maskini wafanyao kazi.
5 Ukurasa wa 35 Muhtasari wa Kipengele B na C
2 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
2. Yesu alichagua kuishi katika hali duni ya kufanya kazi. 3. Yesu alikuwa anaweka mkazo mkubwa sana kwa kuonyesha kwa vitendo kwamba tunahitaji kuwathamini watu walio katika umaskini. 4. Yesu alichagua kuwa rabi ambaye hakuwa na heshima nyingi na mamlaka nyingi za kidunia. Alifanya hivyo akiweka kielelezo cha unyenyekevu. 5. Mungu anaweza kuvuka mipaka ya popote ulipo kama mtu, au kama kanisa, kama ilivyo katika Kitabu cha Matendo. 6. Uwezeshaji ni muhimu zaidi kuliko sababu. • Lenga katika kuunda njia za fursa. • Kwa watu wanaoishi katika hali ya umaskini, wajue huo si utambulisho wao, bali ni hali wanayoishi. • Tunapaswa kuheshimu talanta na uwezo wao na kuelewa kwamba Mungu atazitumia. Sasa waruhusu wanafunzi watoe maoni yao juu ya kile kilichowasilishwa. Hapa kuna baadhi ya mada ambazo zinaweza kujadiliwa ikiwa unahitaji kuendeleza mjadala. (KUMBUKA: Haulazimiki kuzitumia. Ikiwa darasa lako linakwenda vizuri, waruhusu wanafunzi wajadili kwa uhuru). • World Impact hutoa mafunzo ya ngazi ya seminari yenye ufanisi, nafuu, na rahisi kuyapata, jambo ambalo ni njia ya fursa. Hili linatokana moja kwa moja na Maandiko. • Sababu kuu inayosababisha wachungaji wasipate mafunzo rasmi ni ukosefu wa pesa. • Shirika lisilo la kiimani linaweza kuchukua baadhi ya kanuni za Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini na kufanya mambo mazuri; wanaweza kuifanya dunia kuwa mahali pazuri zaidi. Sehemu ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini ni Kazi ya Kupambana na Umaskini kwa misingi ya kimaadili.
1
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
6 Ukurasa wa 37 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 2 9
• Jadili kuhusu wafanya kazi maskini katika huduma. Mungu amemuumba kila mmoja wetu kwa kusudi na ametupa karama na talanta ili tuweze kutoka na kuifanya dunia kuwa mahali pazuri zaidi. Kwa hivyo, ikiwa tutatoka na kujaribu kufanya yale tuliyoumbwa kufanya na kueneza Ufalme, kutakuwa na upaji wa kutosha kukidhi mahitaji yetu. • Mwanzo 3 inaweka wazi kabisa kwamba tunaishi katika ulimwengu ulioanguka, kwa hiyo tutegemee kukutana na magumu katika maisha yetu. Mungu atatumia magumu hayo tunaposhughulika na wengine. Mungu atageuza mitihani yetu kuwa ushuhuda. Amini katika ahadi za Mungu kwamba hatimaye, kila kitu kitakuwa sawa ingawa unaweza usione hayo katika wakati wa maisha YAKO. • Walio wengi hawafanikiwi kuondokana na umaskini. • Sababu kubwa kwa nini watu wako katika umaskini ni kwamba walizaliwa humo. • Au tumia yafuatayo kwa ajili ya majadiliano darasani: 1. Kwa nini watu hawana ufahamu wa Kibiblia 2. Mbali na kuwa kipaumbele cha ufalme, ni sababu zipi tatu kuu za kujihusisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini katika mtazamo wa kibiblia? 3. Je, kuna sababu halali za kutojihusisha nayo? Jadili Mfano Halisi Mtumishi kijana wa mjini ambaye anasimamia watu wanaojitolea kutoa mafunzo kwa ajili ya programu ya kufundisha shule katika mtaa maskini amekuja kuomba ushauri. Kazi yake ni kutoa semina elekezi kabla ya wanaojitolea kupewa watoto wa kufanya nao kazi. Amegundua kuwa mara kwa mara anaingia kwenye shida. Kila semina elekezi mjadala unazuka miongoni mwa watu wapya wanaojitolea kuhusu sababu za umaskini. Kundi moja linasema kwamba watu ni maskini kwa sababu walifanya maamuzi mabaya katika maisha yao. Wengine wanadai kuwa watu ni maskini kwa
1
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
7 Ukurasa wa 38 Mfano Halisi
3 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
sababu ya kukosa haki ya kiuchumi. Ni nadra sana kusikia kundi lolote likinukuu Maandiko ili kuunga mkono hoja zake. Utatoa ushauri gani?
• Baada ya wengine kutoa maoni yao, wajulishe kwamba inaongeza thamani kujua mazingira waliyotokea ili tuweze kuwa na taarifa. • Ukizungumza na watu katika namna ya kitheolojia kutokana na kile ambacho Biblia inasema kuhusu umaskini, utashughulikia wasiwasi wa watu wale wanaojitolea. • Tengeneza njia ya fursa, bila kujali walifikaje huko – wapende kama vile Mungu alivyotuamuru kuwapenda, wawezeshe kufanya hali zao kuwa bora zaidi ikiwa wana shauku, na uwawezeshe kufanya hivyo kwa kazi bora ya urejesho kupitia dhabihu.
1
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 3 1
Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini
SOMO LA 2
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini , Somo la 2: Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini . Somo hili linaonyesha aina ya Kazi ya Kupambana na Umaskini ambayo kwa asili hutokana na asili yetu ya dhambi. Chukua muda kufafanua jambo hili la kitheolojia. Kama waliobeba sura ya Mwenyezi Mungu na wafuasi wa Kristo, mara nyingi tunatafuta kufanya mema kwa wale walio maskini. Hata hivyo, ikiwa tunafuata misukumo yetu ya asili na vitendo vya “huduma” visivyo na umakini, mara nyingi tunazalisha Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini . Ile nia njema ya kimungu ya kuwajali na kuwatunza maskini inaweza kupindishwa kwa namna ambazo ni za ubinafsi na uharibifu. Kwa kuzingatia mazingira haya, chunguza njia ambazo tunaweza kujikuta katika aina za kazi ambazo ni kama sumu kwetu na kwa wale tunaowahudumia ikiwa hatutajifunza kujitambua. Sehemu kubwa ya somo hili itawakumbusha baadhi ya wanafunzi uzoefu fulani walioupitia kuhusiana na mada hii. Inawezekana baadhi yao wamefanya Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini na huenda wengine wamehudumiwa kupitia kazi ya aina hiyo. Ruhusu wanafunzi wako kushirikisha na kujadili uzoefu wao wenyewe kuhusiana na tabia za “ugonjwa wa mwokozi,” ubaba, uchovu wenye msongo, na ubeuzi. Kazi ya Kupambana na Umaskini yenye afya huanza tunapokabiliana na udhaifu wa msingi uliojengeka katika kazi zetu – dhana kwamba tunaweza kuwaokoa watu kutoka katika hali zao. Mtazamo hupelekea tabia, na tabia huathiri malengo 1. Tunakutana na mtu au mazingira fulani tukiwa na maadili, mitazamo, na imani fulani kuhusu mtu au mazingira husika (mtazamo wetu). 2. Hilo litasababisha tabia fulani ambazo zitaathiri malengo yetu. 3. Kwa mfano, mawazo ya unyonyaji yanaweza kusababisha tabia ambazo ni sumu. 4. Mwanzo 3 inatuonyesha kwamba sisi sote tunatenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Kwa sababu hiyo, ikiwa
1 Ukurasa wa 41 Utangulizi wa Somo
2
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
2 Ukurasa wa 44 Muhtasari
3 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
hatubadili mifumo yetu ya fikra, tutafanya mambo ambayo yanaweza kuwa mazuri kutokana na utu wetu wa asili, lakini mambo mengine tutajaribu kufanya kwa sababu za ubinafsi.
I. Ugonjwa wa Mwokozi: Kuchukua jukumu ambaloMungu hakukusudia tulichukue. 1. Tunataka kuingia na kuokoa watu na jamii zao. 2. Hakuna hata mmoja wetu aliye na uwezo wa kuokoa mtu yeyote. Hatuwezi kujiokoa. Tunaweza tu kutumiwa na Mungu ili tuweze kufanya hali kuwa bora zaidi. 3. Hatuna nia ya makusudi ya kuwanyonya watu waishio katika umaskini, wala hatukusudii kwenda mitaani na kufanyika sumu kwa watu. 4. Pamoja na kukujulisha kwamba hutakiwi kwenda kuwaokoa watu, lakini bado uko nje kujaribu kuokoa watu. 5. Ikiwa hatutashughulikia uwezo wetu au dhana yetu ya kwenda na kujaribu kuokoa watu, tutaishia kwenye maumivu mengi ya moyo, majeraha, na mateso. Kitu pekee ambacho watu wanahitaji kuona kutoka kwetu ni kwamba Yesu yu ndani yetu. II. Ubaba: Suala la matumizi ya nguvu na mamlaka 1. Katika kutoa msaada, tunahisi kama sisi ni wazazi na wale walio katika umaskini ni watoto na kwa hiyo hawawezi kujitunza wenyewe na hawana sauti ya kujihusisha au kutoa mchango katika ndoto, matumaini, malengo yao wenyewe, nk. 2. Tunadhani tunajua kilicho bora zaidi. 3. Usiwe dikteta. Usiingie, ukachukua nafasi, na kuamuru nini kifanyike na jinsi kinavyopaswa kufanyika. Ikiwa tunajua kilicho bora zaidi, basi tunapaswa kufanya kazi pamoja na mtu binafsi au jamii kutafuta njia bora zaidi na maoni yao na hivyo kujenga mambo pamoja.
3 Ukurasa wa 44 Muhtasari wa Kipengele cha I
2
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
4 Ukurasa wa 45 Muhtasari wa Kipengele cha II
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 3 3
III. Uchovu, Msongo na Ubeuzi: Kuteseka kutokana na Uchovu na Kukatishwa tamaa Uchovu: Mateso yatokanayo na kuchoka kwingi. 1. Unajumuisha mambo matatu: • Kuwa na mtazamo usio sahihi • Kuendelea kujaribu kuwaokoa watu kutoka kwenye hali zao • Kujaribu kudhibiti mambo kila wakati (ubaba) 2. Ni sawa na kwenda maili 100/saa na kutojitunza. 3. Kufahamu kwamba sio kila kitu kitaenda vizuri kama tunavyotaka, inawezakuwa tiba ya ukweli yenye afya iwezayo kuzuia uchovu na msongo. Tunafikiri kwamba tunachofanya kitakuwa cha ajabu na cha kimuujiza katika jamii hii, na kisipotokea hivyo, kinaweza kusababisha uchovu, kukata tamaa, na msongo. 4. Tunahitaji kuchukua muda wa sabato ili kujitia nguvu upya badala ya kupatikana masaa 24, siku 7 za wiki. Ikiwa tunapatikana kila wakati, kuna kitu hakipo sawa. 5. Uchovu unaweza kusababisha watu kuacha kanisa, kutilia shaka imani yao na kwenda mbali na Bwana. Ubeuzi: hali inayosababishwa na kukatishwa tamaa. 1. Kimsingi, ubeuzi hutokea pale tunapopoteza matumaini. Tunaweza kujisikia fahari kufanya kazi ya huduma, lakini tukawa wabeuzi kuhusiana na kila kitu na kila mtu aliye karibu nasi; tunafikiri kwamba hakuna matumaini tena kwa watu au mitaa iliyo katika umaskini. Kweli, tumevunjika moyo. 2. Ubeuzi ni binamu wa uchovu. 3. Kila kitu kinaonekana kuwa cha hovyo na kisicho na maana, kana kwamba hakuna kitu kizuri ulimwenguni au kwa watu.
5 Ukurasa wa 45 Muhtasari wa Kipengele cha III
2
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
3 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
4. Kila mwenye hali ya ubeuzi aliwahi kuwa mtu mwenye kuwaza makubwa zaidi ya uhalisia. 5. Kazi ya Kupambana na Umaskini inaweza kutuchochea kuwa watu wa wenye ubeuzi kwa sababu kuna utata mwingi ambao tunajihusisha nao tunaposhughulika na watu, hasa wale walio katika hali ya umaskini.
Kwa muhtasari, tunakuwa na mtazamo usiofaa tunapoingia katika hali ambazo zinasababisha tabia zenye sumu ambazo hatimaye zinasababisha malengo yasiyo sahihi.
6 Ukurasa wa 47 Hitimisho
2
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
Sasa waruhusu wanafunzi watoe maoni yao juu ya kile kilichowasilishwa. Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya mada ambazo zinaweza kujadiliwa ikiwa unahitaji kuendeleza mjadala. (KUMBUKA: Haulazimiki kuzitumia. Ikiwa darasa lako linakwenda vizuri, waruhusu wanafunzi wajadili kwa uhuru). • Huenda kuna baadhi ya watu ambao wako tayari kupokea ukweli huu. Kwa wengine wasio tayari unaondoka tu. Usibishane nao. Watu kwa kawaida wamegawanyika katika kambi hizi mbili: 1. Wale ambao wanataka kujifanya kama wanaelewa, na wanataka kubishana na wewe siku nzima. 2. Wale ambao wanajaribu kubaini mambo na unaweza kujadiliana nao. • Tunapomsaidia mtu na akayatoa maisha yake kwa Kristo, huo ni mwanzo tu. Tunapaswa kujiandaa na mfumo au mkakati maalum ili mtu anapotoa maisha yake kwa Kristo, tujue hatua ambazo zitatusaidia kuwekeza ndani yake na kumtia moyo kukua katika imani yake. • Tunapaswa kujaribu kuiga kile ambacho Yesu alitufanyia katika Maandiko. Yesu alipokutana na watu katika uhitaji wao, aliwajulisha nia yake ilikuwa nini.
7 Ukurasa wa 47 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 3 5
• Au tumia maswali ya majadiliano yafuatayo: 1. Je, umewahi kuishi katika umaskini? Je, uzoefu wako huo (au kutokuwa na uzoefu huo) unaathiri vipi uelewa wako wa umaskini? 2. Je, ni rahisi au ngumu kiasi gani kwako kukubali kwamba ikiwa umeshiriki katika Kazi ya Kupambana na Umaskini, wakati fulani, umefanya Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini? 3. Je, ni masuala gani ambayo unahitaji kuyashughulikia kibinafsi baada ya kujifunza kuhusu Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini? Jadili Mfano Halisi: Baadhi ya marafiki wanakuomba utembelee ghala la Kikristo la kugawa chakula kwa wahitaji, ambapo wanafanya kazi kwa kujitolea. Kama mtu wanayemwamini, wanataka uangalie na utoe maoni yako juu ya utendaji wa ghala hiyo. Jambo la kwanza unaloona unapotembea ni baadhi ya watu walio vifua wazi wakicheza kamari, kuvuta sigara na kunywa pombe karibu na mlango. Unapoingia ndani, unashangazwa na jinsi ndani palivyo giza na pachafu. Mambo yanaonekana yamekaa shaghalabaghala na huwezi kujua ni kwa namna gani watu wanavyopokea mahitaji yao. Watu wanachoka kusubiri. Kisha mhubiri kijana anakuja katika eneo la kungojea na kutoa mahubiri. Anapomaliza, kila mtu anainua mkono wake kumpokea Kristo. Baada ya kama saa moja hivi, mtu wa kwanza anaenda mbele kuchukua mfuko wa vyakula, jambo hilo linageuka kuwa mzozo mkubwa kati ya mtoa huduma na mteja juu ya uchaguzi wa chakula. Mtoa huduma anamwambia kwamba alichokipata ndicho kilichotolewa, na anapaswa kufurahiya. Baadaye, unatoka kwenda kula chakula cha mchana na marafiki zako ili kujadili uchunguzi wako. Unawaambia nini?
2
8 Ukurasa wa 48 Mfano Halisi
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
3 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Waache wanafunzi wajibu hili, lakini hapa kuna mapendekezo ya baadhi ya vipengele vya kuanza navyo: 1. Ningeingia ndani zaidi katika uchunguzi wangu, hadi kwenye mpango wenyewe. Nia ya mpango huo ni nini? Kwa nini walianza? 2. Nini ni sumu katika hali hii: • Mazingira ya mlango wa mbele • Wale wanaohudumu (mafunzo yanahitajika) • Ujumi (uzuri na ubora) • Kuwashikilia watu kwa muda mrefu • Kutokuwa na utaratibu – utaratibu wa ghala unasababisha matatizo mengi badala ya kuleta suluhu au kuwafanya watu wajisikie vizuri wanapopokea chakula. • Inaonyesha kuwa watu wanaokuja kuomba msaada hawathaminiwi. 3. Ni muhimu kwamba watu wanaohudumiwa wawe na umiliki. Wanapaswa kuamini kuwa unachofanya/kutoa kinawanufaisha sana. 4. Tunapaswa kutoa msaada kwa nia ya uendelevu. Toa msaada kwa kuzingatia mahitaji halisi yanayobainishwa na wanufaika wenyewe na fanya hivyo pamoja na watu ambao watakuwa katika jamii husika kwa muda mrefu, jambo ambalo litaweza kuimarisha programu na wito ambao Mungu ameweka juu ya maisha na mioyo yao. Hilo ndilo litakaloleta mabadiliko ya kudumu.
2
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 3 7
SOMO LA 3
Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini , Somo la 3: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini. Somo hili linafafanua lengo la shughuli yetu kwa kuchunguza aina tatu za mitazamo katika Kazi ya Kupambana na Umaskini zinazofanyika kwetu. Aina ya kwanza kati ya hizo tatu ni Mtazamo wa Unyonyaji , hii inajengwa moja kwa moja kwenye mjadala uliopita wa Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini. Kwa namna fulani, mtazamo wa kinyonyaji ni kupuuza uwezekano wa sumu katika Kazi ya Kupambana na Umaskini. Wasaidie wanafunzi wako kuuona muunganiko huu na uwaonyeshe jinsi Kazi Hatarishi ya Kupambana na Umaskini inavyoenda pamoja na mtazamo wa kinyonyaji. Mtazamo wa pili ni Mtazamo wa Kimaadili . Huu unatambua mema ambayo mtu yeyote anaweza kufanya katika jamii. Si kila hatua ya wafanyakazi wa kupambana na umaskini itakuwa sumu au itakuwa na matokeo ya uharibifu. Hata mbali na mtazamo wa kiukombozi, mara nyingi watu hufanya kazi kwa manufaa ya wote kwa njia za kimaadili. Wasaidie wanafunzi wako kufikiria mashirika na watu wanaofanya Kazi ya Kupambana na Umaskini kwa misingi ya kimaadili. Mashirika na watu kama hao wanaweza kuwa washirika wenza halali na wenye manufaa kwetu tunapofanya kazi ya kukomboa watu kutoka katika umaskini. Mtazamo wa tatu, Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini , inafuata kielelezo cha kazi ambayo Kristo amefanya msalabani tunaposhughulika na ukombozi wa maisha ya watu na mitaa yao. Ni muhimu kwamba wanafunzi wako waone uhusiano kati ya kazi ya ukombozi ya Kristo mwenyewe na kazi tunayotafuta kufanya. Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini si mkakati mpya au wazo lililovumbuliwa. Ni kuifanya tu kazi yetu ya umaskini ifuate kielelezo cha kazi ya ukombozi ya kujitolea ya Kristo. Hakuwezi kuwa na mbinu ya kutegemewa zaidi ya ile ambayo Mungu ametumia katika Kristo.
1 Ukurasa wa 51 Utangulizi wa Somo
3
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
3 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
I. Mitazamo Mitatu Tofauti katika Namna Tunavyoiendea Kazi ya Kupambana na Umaskini Kuna aina tatu za kazi zinazofanyika duniani ambazo ulisoma au kuona kwenye video.
2 Ukurasa wa 54 Muhtasari wa Kipengele cha I
Kazi ya kiukombozi Kazi ya kimaadili Kazi ya kinyonyaji
3
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
A. Tabaka la nje la kujitambua kwetu ni Mtazamo wa Kinyonyaji katika Kazi ya Kupambana na Umaskini. 1. Hupelekea mtazamo wa ugonjwa wa mwokozi. 2. “Niko hapa kukuokoa wewe na mtaa wako.” 3. Hali ya umimi inatawala. 4. Sio makusudi, lakini hutokea kwa sababu hatujitambui na jinsi tunavyoingia katika maisha ya mtu fulani au katika jamii fulani. 5. Unajaribu kupata kitu kutoka kwa mtu au kutoka kwa jamii husika. 6. Swali linakuwa, “Je, tunafikia ukomavu na kutambua kwamba hatupo hapa kwa ajili yetu, badala yake tuko hapa kumwakilisha Mungu? Watu katika jamii hii hawanihitaji mimi, wanamhitaji Yesu aliye ndani yangu. Wanahitaji kusikia Habari Njema.”
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 3 9
B. Hatua inayofuata katika kujitambua kwetu ni Mtazamo wa Kimaadili wa Kazi ya Kupambana na Umaskini. 1. Hiki ndicho kiwango cha juu ambacho mtu anaweza kufikia bila kumjua Kristo. 2. Hakuna ubaya katika Kazi ya Kupambana na Umaskini ya kimaadili 3. Kuna mageuzi makubwa; kutoka “Niko hapa kwa ajili yangu” hadi “Niko hapa kwa ajili ya watu hawa.” 4. Ni mtazamo unaolenga kila upande kunufaika. “Nataka kushinda, unataka kushinda, kwa hivyo tufanye kazi kwa pamoja na tushirikiane ili kila mtu ashinde katika hali hii.” 5. Kazi ya Kupambana na Umaskini kwa misingi ya kimaadili ndio msingi wa kile ambacho Mungu ameiita World Impact kufanya, ambayo ni Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini. C. Hatimaye, kuna Mtazamo wa Kiukombozi wa Kazi ya Kupambana na Umaskini. 1. Urejesho bora kupitia dhabihu. 2. Inahusiana sana na nia na kiwango cha urejesho kupitia dhabihu. Ni kufuata mtindo ambao Kristo alifuata ili kutukomboa. 3. Kuhamasishwa kudhabihu muda na hazina zetu kwa sababu Kristo alifanya vivyo hivyo kwa ajili yetu. 4. Sisi sio mwokozi wa jamii hii (tunamofanya kazi) bali Kristo ndiye Mwokozi. Tunataka kuwatambulisha kwenye njia za Kristo ili waweze kuchukua fursa inapotokea kwao wakati wakiwa katika umaskini.
3
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
4 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
II. Kazi ya Kiukombozi katika Biblia Sifa za Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini: • Uwezeshaji wa kimaadili.
3 Ukurasa wa 55 Muhtasari wa Kipengele cha II
• Urejesho bora kupitia dhabihu. • Mungu ni mkuu kuliko mazingira. • Umaskini ni hali, si utambulisho. • Enenda kwa imani huku ukipanga upya nguvu za kimfumo za binadamu. 1. Uwezeshaji wa kimaadili • Ninajidhabihu, unashinda. Namna tunavyofanya kazi zi muhimu. Mwitikio wa watu ni wa muhimu na wa kuzingatiwa sana. • Haihusiani na sisi tu, haihusiani na wao tu, ni kuhusu kufanya kazi pamoja kwa ushirikiano ili Mungu aweze kupokea utukufu wote. 2. Urejesho bora kupitia dhabihu • Kielelezo ambacho Kristo alitumia kutukomboa. • Kwa sababu ya yale ambayo Yesu ametufanyia, tunataka kufanya hivyo kwa ajili ya wengine. • Unafanya hivi na unajaribu kufanya kazi ili kufanya hali kuwa bora kwa watu wanaoishi katika hali ya umaskini, kwamba inakunufaisha au la. Utajitolea na kujaribu kufanya maisha yao kuwa bora, kama vile Kristo alivyofanya kwa ulimwengu mzima. 3. Mungu ni mkubwa kuliko mazingira. • Hii ni dhahiri lakini inasahaulika kwa urahisi. • Mungu ni mkubwa kuliko mazingira tunayoyaona, na Mungu ni mkubwa licha ya mazingira.
3
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online