Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

Kuandaliwa Kupanda, Kuchunga, na Kutumikia Kanisa! Nyenzo za mtaala wa Cornerstone zinajumuisha kozi ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini na nyenzo zilizotolewa moja kwa moja kutoka kwenye moduli za Capstone , zikitoa kweli zake muhimu kutoka kwenye maeneo manne ya idara zake (Masomo ya Biblia, Theolojia na Maadili, Huduma ya Kikristo, na Utume katika Miji). Tumeweka pamoja masomo ya Cornerstone ili kukupatia utaratibu thabiti wa mafunzo kwa wakati unaofaa na gharama nafuu. Mafunzo yetu yatakupatia ithibati, yataboresha ujuzi wako wa Maandiko, na kukuwezesha kuhudumu vyema kama mchungaji, kiongozi mlei, au Mkristo mtenda kazi mahali unapoishi na kufanya kazi. Mungu amekuita na kukupa karama, na tunatumaini kukuona ukitimiza wito wake kwenye maisha yako, ili upate kumletea heshima Mwokozi wetu katika kila jambo ulifanyalo. Kwa hiyo, ninakupa changamoto ya kutimiza huduma ya Bwana kwa ajili yako, yote katika nia ile ile kama ya Paulo anapomuasa Timotheo, “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” (2 Tim. 2:15). Fahamu kwamba ukijitoa kwa Mungu kama mtu aliyekubaliwa, utatimiza wito wake na kuzaa matunda ya kiroho ambayo yanamtukuza Kristo na kumpendeza Mungu. Mungu akubariki sana katika masomo yako, ufuasi wako, na huduma yako! Kwa ujasiri mkubwa katika Neno la Mungu la milele lenye kuponya

na kubadilisha, Dkt. Don Davis Wichita, Kansas Februari 1, 2023

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online