Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 7 9

Wape changamoto wanafunzi wako ili kufikia hali ya kuwa makini, kuwa na kiasi na shauku katika maono yao kuhusiana na Neno ambalo Ezra alilishikilia, na labda Roho Mtakatifu atakuwa wa neema sana kwetu na kutupa aina hiyo hiyo ya matokeo kama aliyokuwa nayo kwa watu wa Mungu, kwa ajili ya utukufu wake. Chunguza ufafanuzi, dhumuni, vipengele na faida za Mbinu ya Hatua Tatu kupitia maswali haya hapa chini. Shabaha yako hapa inatakiwa iwe ni kuwasaidia wanafunzi wako kuwa mahiri katika kufahamu dhana muhimu na ujuzi kuhusiana na mbinu hiyo kama ilivyowasilishwa katika video ya kwanza. Pia, weka shabaha kwenye uchambuzi wao wa maelezo kulingana na malengo ya somo yaliyowasilishwa mwanzoni mwa somo hili. Bila shaka, weka umakini mkubwa katika muda pia, na ujikite sana katika maswali haya hapa chini na yale yatakayo ulizwa na wanafunzi wako ambayo yanaenda katika kiini kabisa cha somo. Hakikisha pia, unakuwa macho kugundua wazo lolote lililotofauti ambalo linaweza kukutoa kutoka kwenye kupima kweli muhimu na dondoo zinazohusiana na kufahamu mantiki ya Mbinu ya Hatua Tatu ya utafsiri wa Biblia. Wape changamoto wanafunzi ili kutendea kazi Neno la Mungu katika jamii zao na pale wanapokuwa na wanafunzi wenzao pamoja na marafiki. Nguvu ya maombi ya pamoja kugusa moyo wa Bwana na kufanya mkono wake utende imeandikwa vizuri sana katika maeneo yote ya Maandiko, na hivyo hilo ni jambo muhimu sana katika utendeaji kazi wa Neno la Mungu kwenye maisha yetu. Kamwe usionyeshe katika kipindi hiki kwamba unafanya hili kwa mazoea na kama utaratibu peke yake. Badala yake, wahimize wanafunzi kutia bidii na kwa moyo wafanye haja zao zijulikane na Mungu, na kutarajia kwamba atafanya sawasawa na wao, wawili au watatu, walivyokusanyika na katika jina lake na kuomba (Mt. 18:20).

 3 Ukurasa wa 120 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu

2

M A F U N Z O Y A B I B L I A

 4 Ukurasa wa 129 Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online