Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

9 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

1 Yoh. 3:5 – Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Ufu. 20:2-3 – Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; 3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache. Ufu. 20:10 – Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele Tafadhali, angalia tena katika malengo kwamba kweli hizi zimeelezwa kwa uwazi. Kama kawaida, jukumu lako kama Mkufunzi na mshauri ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa majadiliano na muda wa kukaa kwako pamoja na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo uwezekano wa wanafunzi kufahamu ukubwa wa malengo haya unavyozidi kuwa mkubwa. Ili kuelewa asili ya mgogoro, mwanafunzi ni lazima alipokee hili kama sehemu ya safari yake ya kawaida, ya kiroho. Kwa sababu Bwana wetu aliteseka mikononi mwa wale ambao hawakumjua Mungu wala yeye, na kwa sababu tumeungamanishwa na Kristo kwa imani (Rum. 6:1-6), hakuna mwamini au kiongozi wa Kikristo anayepaswa kushtushwa na mateso, kana kwamba kitu fulani kinatokea ambacho hakikutarajiwa au hakikupangwa. Ibada hii inakazia kule kutoepukika kwa mateso kwenye maisha ya wale wanaofuata nyayo za Yesu. Na ushuhuda wa Neno la Mungu unathibitisha haya: 1 Pet. 4:12-14 – Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. 13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. 14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.

 2 Ukurasa wa 159 Malengo ya Somo

4

M A F U N Z O Y A B I B L I A

 3 Ukurasa wa 159 Ibada

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online