Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 1 0 3

M U N G U B A B A

³ Maandiko yanasisitiza kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine isipokuwa Mungu mmoja, na bado yanasisitiza kwamba Mungu huyu mmoja amejifunua kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. ³ Kila mshiriki wa Utatu (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu) anazo sifa za Mungu, anafanya kazi ya Mungu, anaitwa Mungu, na hutumia mamlaka kama Mungu. ³ Biblia inathibitisha umoja wa Mungu, na wingi wa Mungu (kwamba Uungu ni zaidi ya nafsi moja), na nafsi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu zinatajwa kwa pamoja kama nafsi katika Ukamilifu wa Uungu Mtakatifu. ³ Fundishola Utatu linasisitiza kwamba Mungu yuko katika nafsi tatu, na kwamba washiriki wote wa utatu wanashiriki asili moja, wanatofautiana katika haiba na kazi zao, na bado wanalingana katika utukufu, kwa pamoja wakimkamilisha Mungu mmoja wa kweli, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. ³ Mungu Baba Mwenyezi ni Mungu, na anadhihirisha sifa zote za kiungu za ukuu. ³ Mungu Baba Mwenyezi ni roho, hatokani na kitu au asili ya kimwili. ³ Mungu Baba Mwenyezi ni uzima na ana uzima, amekuwapo daima na hawezi kuharibika wala kufa. ³ Mungu Baba Mwenyezi ni nafsi hai, anao ufahamu, anaweza kujua, kuhisi, na kuchagua, na anaweza kuhusiana na viumbe hai wenye ufahamu na uumbaji kwa ujumla. ³ Mungu Baba Mwenyezi hana ukomo: kuhusiana na nafasi yuko kila mahali, kwa habari ya wakati ni wa milele, kuhusu ufahamu anajua yote, na kwa habari ya nguvu, anaweza yote. ³ Mwisho, Mungu Baba mwenyezi habadiliki na anadumu: hataacha kuwa, daima amekuwa vile atakavyokuwa, na hatabadilika katika ukamilifu wake wowote, utukufu, au ubora wake.

3

Made with FlippingBook - Share PDF online