Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 1 0 7

M U N G U B A B A

Fundisho la Utatu na ukuu wa Mungu Baba sio mada tu za kitheolojia za kujifunza na kuwekwa kando. Kinyume chake, hizi ndizo kweli kuu za imani, na wale wanaozitafakari kwa muda mrefu hubadilishwa milele kutokana na kutafakari huko. Kuzihusisha kweli hizi katika maisha na huduma yako kunaweza kukabadilisha maisha na huduma yako; gharama ni utendaji makini wa Neno la Mungu kwenye maisha yako mwenyewe. Unapoendelea kutafakari juu ya mafundisho ya somo hili, muulize Bwana ni kwa namna gani angekutaka utajirishe, ubadilishe, na kugeuza namna yako ya kufanya huduma kupitia kweli hizi ambazo Roho mtakatifu amekuonyesha hapa. Unapozitafakari kweli hizi, na kufikiri kuhusu maisha yako mwenyewe na huduma iliyo unganishwa nazo, tafuta kutambua kile ambacho Roho anaweza kuwa anakuita kufanya sasa hivi, kama kuna chochote, kuhusu kweli hizi. Tumia muda mbele za Bwana ukitafakari juu ya kweli kuhusu asili na ukuu wa Mungu, na umuulize ni jinsi gani au kwa namna gani unaweza ukafanyia kazi kikamilifu fundisho hili. Pia, unapofikiria kuandika kazi yako ya Huduma kwa Vitendo kwa ajili ya moduli hii, unaweza kuunganisha kazi yako na mada fulani hapa. Mtafute Bwana ili akupe mwelekeo wake, na urudi juma lijalo ukiwa tayari kuwashirikisha wanafunzi wengine darasani kwako kuhusu mawazo yako. Katika kutafakari kweli hizi juu ya asili ya Mungu kama Bwana wa utatu na juu ya ukuu wa Mungu Baba Mwenyezi, mtu huanza kuona utoshelevu wa Mungu wetu kukidhi kila hitaji, si tu katika maisha binafsi ya mtu lakini katika maisha ya wale tunaowapenda na kuwatumikia. Labda katika kipindi cha somo hili, wakati ukitafakari juu ya ukuu wa Baba, kuna hitaji fulani muhimu ambalo limefunuliwa kwako. Roho Mtakatifu amekufanya, pengine, kuzingatia suala, hitaji, au jambo fulani, na unahitaji kumtafuta Bwana kwa ajili ya uweza na msaada wake katika jambo hilo. Sasa ni wakati wa kushirikishana mahitaji yenu na kuombeana. Kama muda hautawaruhusu kuomba pamoja sasa hivi, tafuteni mshirika wa maombi ambaye mtamshirikisha mizigo yenu na ambaye atayapeleka maombi yenu mbele za Bwana. Bila shaka, tambueni kuwa mwalimu wenu atakuwa tayari na wazi kabisa kuomba nanyi, pamoja na viongozi wenu wa kanisa, hasa mchungaji wako. Msikilize Bwana na umruhusu Roho Mtakatifu akuongoze katika kumshirikisha haja zako Baba Mwenyezi, Mungu wetu mkuu na mwenye enzi na Bwana wa wote.

Kuhusianisha Somo na Huduma

3

Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook - Share PDF online