Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

1 4 0 /

M U N G U B A B A

Maswali yaliyo hapa chini yatakurahisishia kupitia yale uliyojifunza hivi punde katika sehemu ya pili ya video. Ghadhabu ya Mungu, ingawa ni fundisho muhimu sana la Maandiko, linaelekea kutoeleweka na kutumiwa vibaya, au mbaya zaidi, kupuuzwa kabisa. Tafakari kwa makini unapotoa majibu yako kwa maswali yafuatayo, na ujenge hoja zako kwa kutumia Neno la Mungu. 1. Elezea ufafanuzi wa Packer wa ghadhabu ya Mungu Baba Mwenyezi: “Mungu kuingia katika tendo la kulipiza kisasi, kwa namna yoyote, dhidi ya wale waliomkaidi.” Je, ghadhabu ya Mungu ina umuhimu gani kwa ufahamu kamili na wa kibiblia kuhusu nafsi ya Baba? 2. Kwa nini ni muhimu kuona ghadhabu ya Mungu kama mwitikio wake kwa mambo yasiyoendana na mapenzi yake mema, ya kupendeza, na ya ukamilifu ? Je, ghadhabu ya Mungu imewahi kufanywa kwa njia ya kiholela au isiyo ya haki? Elezea. 3. Ni zipi baadhi ya njia ambazo Maandiko yamefafanua kiini na udhihirisho wa hasira ya Mungu? Inawezekana kuepuka adhabu na kukumbana na ghadhabu na hasira ya Mungu? Toa jibu lenye maelezo ya kina. 4. Tunapaswa kuuelewaje uhusiano kati ya rehema na haki ya Mungu, ghadhabu na upendo wake? Je, kuna mgogoro gani hasa kati ya sifa hizi ambazo zinaonekana kukinzana? 5. Je, ukweli kwamba Mungu ni mmoja unatusaidiaje kutatua aina hizi za maswali kuhusu migogoro inayodhaniwa kuwepo katika asili ya Mungu? 6. Ni kwa njia gani Kalvari (kifo cha Yesu msalabani) ni taswira kamili na kielelezo cha ghadhabu na upendo wa Mungu, kwa wakati mmoja? 7. Kipi ni kiini cha mwisho cha mambo katika kutafakari juu ya ghadhabu ya Mungu? Je, ufahamu wa kibiblia wa ghadhabu ya Mungu unapaswa kuzalisha nini katika maisha yetu?

Sehemu ya 2

Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu page 298  5

4

MUUNGANIKO

Mungu huonyesha wema wake kupitia sifa zake za kiadili za usafi, uadilifu, ukamilifu, na upendo kamili usio na mipaka. Ufahamu wa ghadhabu ya Mungu ni muhimu ili kuutambua kikamilifu utukufu wa Mungu Baba Mwenyezi. Tunaweza tu kuielewa ghadhabu ya Mungu kwa kuihusianisha na wema wake, na japokuwa tunaweza kupata ugumu wa kimantiki kutatua mvutano katika akili zetu kuhusu mambo hayo mawili, hakuna mvutano uliopo katika asili ya kupendeza ya Mungu mmoja wa kweli.

Muhtasari wa Dhana Muhimu

Made with FlippingBook - Share PDF online