Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
1 7 0 /
M U N G U B A B A
Mila (muendelezo)
ile mitaguso ambayo inaendelea kutumiwa na Kanisa zima imekamilishwa na baraza la Kalsedoni katika mwaka 451. Ni vyema kufahamu kwamba kila mtaguso katika hii mitaguso minne Kiekumene ulifanyika kabla ya muktadha wa utamaduni wa Ulaya na hakuna hata mmoja ambao ulifanyika Ulaya. Ilikuwa mitaguso ya Kanisa zima na ilikuwa ina akisiwa muda ambao Ukristo ulikuwa kimsingi ni dini ya mashariki katika kiini chake cha kijiografia. Kwa kuchunguza kwa sasa, washiriki wao walikuwa Waafrika, Waasia na watu wa ulaya. Mitaguso iliakisi Kanisa ambalo “. . .lina mizizi katika utamaduni ulio tofauti kabisa na Ulaya na kutangulia maendeleo ya utambulisho wa Ulaya ya leo, na [ambayo] baadhi ya michango mikubwa kabisa imetoka kwa Waafrika” (Oden, The Living God , San Francisco: HarperSanFrancisco , 1987, uk. 9). Labda mafanikio ya muhimu zaidi ya mitaguso hii yamekuwa ni kutengenezwa kwa kile ambacho kwa sasa kinaitwa Kanuni ya Imani ya Nikea. Inafanya kazi kama muhtasari wa tamko la imani ya kikristo ambayo inaweza kukubaliwa na wakristo wa Kikatoliki, Kiothodoksi, na Kiprotestanti.
Mitaguso minne ya Mwanzo imefafanuliwa katika chati ifuatayo:
Jina/tarehe /mahali
Dhumuni
Mtaguso wa Kwanza wa Kiekumene 325 B.K Nikea, Asia Ndogo Mtaguso wa Pili wa Kiekumene 381 B.K Konstantinopoli, Asia Ndogo
Utetezi dhidi ya: Uariani Swali lililojibiwa: Je Yesu alikuwa Mungu? Hatua iliyochukuliwa: Kutengeneza mfumo wa awali za Kanuni ya Imani ya Nikea kuwa kama muhtasari wa imani ya Kikristo. Utetezi dhidi ya: Umakedonia Swali lililojibiwa: Je Roho Mtakatifu ni nafsi na ana hadhi sawa katika Uungu (Utatu)? Hatua iliyochukuliwa: Kanuni ya Imani ya Nikea uliokamilika kwa kupanua maelezo yanayohusiana na Roho Mtakatifu Utetezi dhidi ya: Unestoria Swali lililojibiwa: Je Yesu Kristo ni Mungu na Mwanadamu katika nafsi moja ? Hatua iliyochukuliwa: Kristo alifafanuliwa kama Neno lililofanyika mwili na kumthibitisha mama yake Mariamu kama theotokos (mzazi wa Mungu). Kutetea dhidi ya: Umonofizimu Swali lililojibiwa: Kwa jinsi gani Yesu ana kuwa Mungu na Mwanadamu? Hatua iliyochukuliwa: Uhusiano uliolezewa wa kati ya asili mbili za Yesu (asili ya kibinadamu na ya kimungu)
Mtaguso wa Tatu wa Kiekumene 431 B.K Efeso, Asia Ndogo Mtaguso wa Nne wa Kiekumene 451 B.K Kalsedonia, Asia Ndogo
Made with FlippingBook - Share PDF online