Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 1 7 5

M U N G U B A B A

K I A M B A T I S H O C H A 1 5 Maono na Mbinu za Kitheolojia The Urban Ministry Institute

Muhtasari ufuatao unatoa mtazamo kwa ufupi wa baadhi ya mbinu za kifalsafa za ufahamu kuhusiana na Mungu na uhusiano wake na ulimwengu. Watu binafsi hutoa hoja tofauti za kuwepo kwa Mungu na uhusiano kati ya Mungu na ulimwengu wake kulingana na 1) uelewa wao wa Maandiko, 2) mawazo ya msingi juu ya kuwepo kwa Mungu, 3) mtazamo wa ulimwengu na dunia inayoonekana, na 4) uwezo wa mwanadamu kumjua Mungu (ikiwa yupo), na mambo ambayo ujuzi huo unahusisha. Mbinu nyingi za kisasa hufikiria uwepo wa Mungu na hotuba zote kuhusu Mungu kama uwezekano wa dini katika mipaka ya maarifa. A. Hoja za Kiontolojia – Anselm Proslogion 1. Umuhimu wa kimantiki wa kuwepo kwa Mungu kwa ufahamu wa kawaida pekee 2. Mungu = kile ambacho hakuna kikubwa zaidi yacho kinachoweza kufikiriwa 3. Kuwepo katika uhalisia ni jambo kubwa kuliko kuwepo kwenye mawazo tu. 4. “Kile ambacho hakuna kikubwa zaidi yacho kinachoweza kufikiriwa” lazima kiwepo katika uhalisia na katika mawazo. 5. Tautolojia – (hoja katika duara) kufafanua tu kitu kama kipo hakutoi misingi ya kukisia uwepo wake. 6. Kant – mfanyabiashara hawezi kuongeza utajiri wake kwa kuongeza sufuri kwenye tarakimu katika akaunti zake. B. Hoja ya Kikosmolojia – kuwepo kwa sababu ya kwanza ya ulimwengu. 1. Mambo yote tunayoyaona ulimwenguni yana sababu zilizotangulia. Hakuna kinachojisababisha chenyewe, lazima kuwe na sababu ya kwanza. 2. Mungu ndiye Mtendaji Mkuu na Sababu ya Kwanza. I. Kanuni za Theolojia ya asili

Made with FlippingBook - Share PDF online