Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
1 9 4 /
M U N G U B A B A
K I A M B A T I S H O C H A 2 6 Tahariri Ralph D. Winter
Makala haya yamechukuliwa kutoka Mission Frontiers: The Bulletin of the US Center for World Mission, Buku la 27, Na. 5; Septemba-Oktoba 2005; ISSN 0889-9436. Copyright 2005 ya taasisi ya U.S. Center for World Mission. Yametumiwa kwa idhini. Haki Zote Zimehifadhiwa.
Mpendwa Msomaji, Wakati huu lazima ujifunze msemo mpya: Harakati za Ndani.
Ralph D. Winter ni Mhariri wa
Mission Frontiers na Mkurugenzi Mkuu wa Frontier Mission Fellowship.
Wazo hili kama mkakati wa utume lilikuwa jipya na la kushangaza sana katika siku za Paulo kiasi ambacho karibia hakuna mtu aliyeelewa maana yake wakati huo au hata sasa. Ndiyo maana tunatoa makala hii yote kwa ajili ya “Harakati za Ndani.” Ndiyo maana mkutano wa kila mwaka wa International Society for Frontier Missiology kwa mwaka 2005 umelengwa kimahususi kwa mada hii pia. (Angalia www.ijfm.org/isfm ). Kwanza kabisa, pokea tahadhari: wafadhili wengi wa umisheni na mashujaa wa maombi, na hata baadhi ya wamishenari, wanapinga wazo hili kwa nguvu zote. Mmishenari mmoja mashuhuri aligundua kuwa hata mkurugenzi wake wa bodi ya misheni hakuwa tayari kukubaliana na wazo hili. Hatimaye aliombwa kutafuta taasisi nyingine ya kimisheni ambayo angefanya kazi chini yake. Kwa nini? Mkurugenzi wake alikuwa mchungaji mzuri wa zamani ambaye hakuwahi kuishi kati ya watu wageni kabisa. Baada ya miaka michache ya mawasiliano magumu kati ya mkurugenzi na familia ya mmishenari, uhusiano huo ulilazimika kumalizika. Naam, kwa hiyo hili ni jambo kubwa. Kwa nini Harakati za Ndani ni dhana ya kutatanisha? Vema, kila mahali Paulo alipoenda “Wayahudi” walimfuata na kujaribu kuharibu Harakati za Ndani alizokua akizianzisha. Baadhi ya wafuasi wa dini ya Kiyahudi walikuwa wafuasi halisi wa Kristo ambao hawakuweza kufikiri inawezekanaje Myunani – katika mavazi, lugha, na utamaduni – angeweza kuwa mwamini wa Yesu Kristo bila kuacha kiasi kikubwa cha utamaduni wake wa Kiyunani, kutahiriwa, kushikilia sheria za ulaji za “kosher” , na “miandamo ya mwezi”, nk. Lugha ya wazi ya barua ya Paulo kwa Wagalatia ni moja ya matokeo. Andiko zito sana la barua yake kwa Warumi pia ni sehemu ya matokeo hayo. Miaka mingi sana iliyopita magamba yalianguka machoni mwangu niliposoma kwamba “Israeli
Made with FlippingBook - Share PDF online