Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 2 8 7
M U N G U B A B A
Mungu katika Utatu Ukuu wa Mungu
MAELEZO YA MKUFUNZI 3
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 3, Mungu katika Utatu: Ukuu wa Mungu. Lengo la jumla la somo lina sehemu mbili. Katika sehemu ya kwanza tutalitambulisha wazo la Utatu kwa wanafunzi, dhana ya kibiblia inayohusiana na asili ya Utatu wa Mungu kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Sehemu ya pili inajikita kwenye ukuu wa nafsi ya kwanza ya Utatu, Mungu Baba Mwenyezi. Ndani yake tunachunguza sifa mbalimbali zinazohusishwa na utukufu wa milele na adhama ya Mungu Baba. Mada hizi zote mbili ni za kina, na haziwezi kushughulikiwa kikamilifu katika muda tuliokadiriwa katika fundisho la video. Kinachowezekana, hata hivyo, ni kwamba tunatoa muhtasari wa masuala makuu yanayohusiana na mafundisho haya mawili ambayo yatawawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza mada hizi muhimu katika miezi na miaka ijayo. Unapowaongoza wanafunzi wako katika fundisho la Utatu, zingatia sana mawazo manne rahisi ambayo yanaweza kukuongoza unapojadili fundisho hili muhimu pamoja nao. Kwanza, kumbuka kwamba Mungu ni Mungu mmoja. Hakuna Miungu wawili katika Biblia, mmoja katika Agano la Kale na mwingine katika Agano Jipya. Mungu ni yuleyule katika maagano yote mawili, na asili ya Mungu inapata ufunuo kamili na wa kina zaidi katika Agano Jipya kupita Yesu Kristo, ambaye ametoa ujuzi kamili na wa kina wa Baba kwetu (rej. Yoh. 1:14-18). Pili, Mungu anajifunua kwetu katika nafsi tatu tofauti na zote zinahusika katika shughuli ya wokovu, na bado Mungu anabaki kuwa mmoja asiyegawanyika. Kama utakavyoona unapochunguza maandiko katika somo hili, kwamba Baba amejidhihirisa katika Mwana na Roho pasipo, kwa namna yoyote, kuichanganya nafsi yake nao, au wao kama nafsi kuchanganyika na Baba. Uungu ni utofauti lakini bado ni umoja. Tatu, tunaweza kuuelewa Utatu kwa namna bora kabisa kama tutaelewa wajibu wa kila nafsi katika mpango wa wokovu. Baba anakusudia, Mwana anatekeleza, na Roho anashirikisha baraka ya ukombozi kwa mwamini na katika Kanisa. Agano Jipya halikisii kwa habari ya uhalisia wa Uungu, bali linafunua kile ambacho kila nafsi inafanya kuhusiana na wokovu tulioupata kwa njia ya Kristo. Nne, fundisho la kimaandiko la Utatu haliwezi kueleweka kwa kutumia mantiki na uchambuzi pekee; linabaki kwetu kuwa fumbo na siri ya ajabu kabisa. Ingawa kumekuwa na majaribio ya kuchambua fundisho la Biblia la Utatu, haipasi kutushangaza
1 Page 75 Utangulizi wa Somo
Made with FlippingBook - Share PDF online