Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 4 7

M U N G U B A B A

vitu vyote, huvitegemeza vyote, na atavitimiliza vyote kwa ajili yake mwenyewe. Ndiye mwenye kuhifadhi vitu vyote, na kuvisimamia, na ataviongoza vyote kwenye mwisho wake aliouweka, na hakuna chochote wala yeyote awezaye kumzuia kutimiza kusudi lake. Yeye ni Mungu! Kwa sababu Mungu huyu mkuu ni Mungu wetu, tunapaswa kumpa haki yake, kama Paulo asemavyo, “Heshima na uweza una yeye hata milele, Amina!” Ni ibada pekee na kujisalimisha kwa hiari kabisa mbele za Mungu ndizo zawadi zinazomstahili Mungu mkuu aliye juu sana. Na tufanye hili kuwa lengo letu; kujipatanisha na kusudi la juu, lililotukuka la Mungu huyu mkuu, na kumpa utukufu na sifa ambazo kwa hakika anastahili. Hakika, Mungu wetu ni wa aina yake! Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Utuongoze, Ee Mungu, kutoka kuvitazama vitu vipendezavyo vya ulimwengu hadi kukuwaza wewe Muumba wa vyote; na utujalie kupendezwa na mambo mema ya uumbaji wako ili tufurahi katika wewe, mwanzilishi wa kwanza wa uzuri na Bwana Mkuu wa kazi zote, mwenye kuhimidiwa milele. Bwana wa nguvu na uweza wote, mwanzilishi na mpaji wa vitu vyote vyema: Pandikiza mioyoni mwetu upendo wa Jina lako; ongeza ndani yetu dini ya kweli; tustawishe kwa wema wote; na kuzaa ndani yetu tunda la matendo mema; kwa Yesu Kristo Bwana wetu, anayeishi na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele na milele. Amina. ~ The Episcopal Church. The Book of Common Prayer and Administrations of the Sacraments and Other Rites and Ceremonies of the Church, Together with the Psalter or Psalms of David. New York: The Church Hymnal Corporation, 1979. uk. 233. ~ Appleton, George, mhariri. The Oxford Book of Prayer. Oxford; New York: Oxford University Press, 1988. uk. 62.

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

2

Weka kando vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ufanye jaribio la Somo la 1, Prolegomena: Fundisho kuhusu Mungu na Kuenea kwa Ufalme.

Jaribio page 281  3

Mazoezi ya kukariri maandiko

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: Zaburi 19:1-3.

Made with FlippingBook - Share PDF online