Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 5 9
M U N G U B A B A
(1) Baba Mwenyezi ndiye Muumba wa mbingu na nchi. (2) Mungu hapaswi kulinganishwa na ulimwengu alioufanya. (3) Uhai wote juu ya uso wa nchi upo na una asili yake katika Mungu. (4) Pasipo upaji na utunzaji wa Mungu, hakuna ambacho kingedumu au kuendelea; vitu vyote vina asili yake ndani ya Mungu.
2. Ilichukua muda gani hasa Mungu kuumba ulimwengu? – Juma moja au mabilioni ya miaka?
2
a. Kwa sababu Biblia haitoi taarifa za kina sana kuhusu “sayansi” ya uumbaji, tunaweza kukisia kwamba lengo kuu la Bwana halikuwa ufafanuzi wa kisayansi wa “namna” uummbaji ulivyofanyika. (Ni dhahiri kwamba lengo lilikuwa juu ya “nani” na si juu ya maelezo ya kina ya “namna gani” ).
b. Lazima tuukubali ukweli wa Biblia kuhusu ukichwa wa Adamu (ukweli ambao unathibitishwa kila mahali katika Maandiko, na vile vile na Bwana Yesu mwenyewe).
c. Hatima ya ulimwengu haitegemei nadharia za kisayansi za hivi karibuni kuhusu chimbuko la ulimwengu, bali inategemea mpango wa kiutawala wa Mungu Baba Mwenyezi!
II. Kazi Maalum ya Uangalizi na Utunzaji wa Mungu Inafunuliwa Zaidi katika Utawala wake juu ya Vitu vyote.
A. Ufafanuzi wa utawala wa Mungu juu ya ulimwengu
Made with FlippingBook - Share PDF online