Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 6 9

M U N G U B A B A

Mungu wa Mzungu

Watu wengi wanaamini leo kwamba imani ya Kikristo ni mila ya kidini ambayo imeundwa na kuamuliwa na utamaduni wa Ulaya, kwamba iliundwa na wazungu kwa ajili ya watu weupe. Si ngumu kuona namna walivyopata wazo la namna hiyo: Mapokeo ya Ukristo yanahusishwa na tamaduni za Ulaya, ambapo liturujia nyingi, sanaa, na vyanzo vya maandishi vinatokana na mizizi ya Ulaya, na Mungu mara zote anahusishwa na mataifa ya Magharibi, zaidi ya “Kusini” na “Mashariki.” Ama kwa hakika, wengi huishia kukataa Ukristo kwa sababu wanachanganya imani katika Baba Mwenyezi na uidhinishaji huu wa utamaduni na mtindo wa maisha wa Ulaya na Marekani. Kama ukikutana na mtu anayedai kwamba Mungu wa Ukristo anaonekana kuwapendelea watu weupe duniani, na kupuuzia vilio vya watu weusi katika historia, ungepingaje hoja hii? Je, fundisho la utunzaji, uhifadhi na utawala wa Mungu linatupa mwanga wowote juu ya tatizo letu leo ili kuonyesha kwamba Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo si Mungu wa Wazungu? Mungu Baba Mwenyezi ni Mungu wa utunzaji, Bwana mwenye enzi kuu ambaye ndiye chanzo na mtegemezaji wa vitu vyote, anayehifadhi na kutawala vitu vyote kwa hekima yake. Vitu vyote vipo kwa sababu ya mapenzi yake kama Muumba wa vyote, na vitu vyote vitaleta utukufu kwa jina lake, ambalo ndilo kusudi moja linalounganisha uhai wote kila mahali. “Uangalizi na utunzaji” wa Mungu unarejelea ukweli kwamba “Mungu ndiye afanyaye mapenzi yake makuu ulimwenguni ambamo matukio yote yamepangwa naye ili kutimiza kusudi lake jema kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya uumbaji.” “Uhifadhi” unarejelea ukweli kwamba vitu vyote vipo na vimeshikamana kwa nguvu kuu ya utunzaji na upaji wa Mungu, na “usimamizi” unarejelea ukweli kwamba Mungu ndiye mkuu juu ya ulimwengu wote, ana mamlaka yote ya kufanya chochote anachokusudia katika uumbaji, na ataurejesha uumbaji wote kwenye utukufu wake halisi wakati wa kurudi kwa Kristo. Bila kujali nadharia zinazotolewa kuhusu chimbuko la ulimwengu, hakuna mtu na hakuna kitu kinachoweza kudai kwa namna yoyote kuwa na uwezo wa kujitegemea mbali na Mungu aliye chanzo cha viumbe vyote. Uelewa sahihi wa uangalizi na utunzaji wa Mungu hutatua baadhi ya makosa ya kisasa ya falsafa na theolojia, kama vile pantheism, deism, falsafa ya jaala (fatalism), na ile ya bahati (chance).

3

2

Marudio ya Tasnifu ya Somo

page 284  8

Made with FlippingBook - Share PDF online