Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 7 5

M U N G U B A B A

Mungu katika Utatu Ukuu wa Mungu

S O M O L A 3

page 287  1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuonyesha kupitia Maandiko muhtasari wa fundisho la Biblia kuhusu fundisho la Utatu , yaani Mungu katika nafsi tatu. • Kuelezea namna ambavyo Biblia inatufundisha kwamba kuna Mungu mmoja tu, na bado Mungu huyo mmoja anajifunua kwetu kama Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. • Kuonyesha kutokana na Maandiko namna Mungu anavyozungumziwa kama Mungu mmoja, huku pia akizungumziwa katika lugha ya wingi, yaani, zaidi ya nafsi moja, ambayo ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ambazo ni nafsi katika Uungu Mtakatifu. • Kuzinukuu baadhi ya fahamu (tafsiri) kuu za kihistoria kuhusu Utatu. • Kutambua maana ya asili ya Mungu kama Utatu, pia kuthibitisha kwamba washiriki wote wa utatu ni umoja, tofauti, na sawa, Mungu mmoja wa kweli, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. • Kuonyesha ufahamu wa vipengele mbalimbali vya ukuu wa Baba, yaani, hali yake ya kiroho, uzima wake, haiba yake, asili yake isiyo na ukomo, na hali yake ya kutobadilika. 2 Wakorintho 13:14 – Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Haipaswi kutushangaza kabisa kwamba Mungu ni zaidi ya ufahamu wetu, siri hiyo, ajabu, na kicho vinahusishwa na nafsi ya kiroho, Yeye asiye na kikomo ambaye alizungumza na pasipo kutumia chochote ila Neno lake, akazungusha mamilioni ya nyota na magimba mengine na kuyarushia kwenye giza la anga. Watu wa kisasa hawawezi kustahimili mambo ya kushangaza namna hii; sayansi na maarifa lazima (inadaiwa) vivute na kufunua mapazia ya kila mwana mazingaombwe wa uwongo anayevuta kamba na kuongea katika vipaza sauti kama vile mwana mazingaombwe Utatu Mbarikiwa

Malengo ya Somo

3

Ibada

page 288  2

Made with FlippingBook - Share PDF online